dalalitz
JF-Expert Member
- Sep 6, 2013
- 3,332
- 1,862
Heshima kwenu.
Huwa nashangaa yanapojiri baadhi ya matukio Nchini ambayo yanagusa maswala ya Imani, Waumini ama
Viongozi wengine wa Kiimani.
Huwa najiuliza ni kwa nini viongozi hawa wawili,
Yule wa Wakristu kwa upendo mmoja na yule wa Waislam kwa upendo mwingine, ambao naamini ndio wakubwa zaidi kwa taasisi za kiimani Nchini,
Wao hawa, wanakuwa wazito kujitokeza na kutoa maoni yao,
Misimamo au hata kuwa na kauli za kuionya au kuikaripia serikali hasa pale inapoonekana serikali inafanya ndivyo sivyo.
Sitaki kuamini kuwa siku zote serikali inapatia tu, kuwa hawa masheikh na wachungaji wanao-'shughulikiwa' kuwa siku zote ni wakosefu?
Nilidhani ninyi ndio viranja wa taasisi na viongozi walio chini yenu pale wanapokwenda kombo.
Simaanishi kuwa mjenge uadui au muwe wapinzani kwa serikali au kuwa muwe mtetezi wa viongozi wa taasisi zilizo chini yenu hata katika mambo ya hovyo,
-la hasha.
Ila ingetarajiwa ninyi muwe mtetezi na kimbilio la walio chini yenu wakati huohuo msiionee haya Wala uoga serikali inapokoroga mambo.
Matokeo yake wenzetu mmekuwa watu wa kauli nyepesi kwa mambo mazito.
Hii si sawa.
Kwa mamlaka mliyonayo ninyi ni baba wa serikali.
Kusema tu mnataka amani,
Mnataka amani ilhali inaoonekana wakati mwingine kuwa HAKI inavunjwa?
Kuota au kuhimiza amani pasi kusimamia HAKI ni bure.
Zama tulizonazo ni za kufuata Sheria lakini Sheria zenye kuzingatia HAKI Na UHURU.
Nawasilisha.