Waraka wa wazi kwa mwanangu Koku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa wazi kwa mwanangu Koku

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bishanga, Nov 29, 2011.

 1. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mwanangu Koku,leo nakuandikia waraka huu nikiamini utakusaidia leo na siku za usoni hata kama sitakuwepo duniani.
  Mwanangu,najua unatamani uwe mtu mzima ikiwezekana hata leo ili uondoke nyumbani uwe 'huru' kufanya unavyotaka na kupanga muda wako unavyotaka.Ni kawaida kwa mtoto kuwa na hamu ya kuwa mtu mzima.Kumbuka kipindi utakachokuwa mtu mzima ni kirefu kuliko kipindi cha utoto,hivyo haina haraka,inshallah mola akujalie uhai mrefu.Kumbuka maamuzi unayoyafanya leo ndiyo yatakuamulia maisha yako ya baadae.
  Hakuna jipya chini ya jua hili,mbinu za kupata mafanikio zishajulikana,jifunze mbinu hizo,zitakusaidia.Usifanye jambo eti kwa kuwa wengine wanafanya hivyo,tenda jambo ambalo nafsi yako imekubaliana nalo,usifuate mkumbo,fuata dhamira yako.Kwepa vishawishi vinavyoweza kukutia aibu wewe,familia yako na jamii inayokuzunguka,miliki maisha yako.Kizazi chenu ni cha dot.com,kizazi cha facebook,twitter,bbm na kadhalika,kuwa macho katika ulimwengu wa cyber ,usiwe mwepesi wa kuzoeana na watu wala kutamani ukutane nao,inaweza kuwa hatari.Usijiruhusu kuwa 'addicted' na dunia hii ya mtandao,be real.Jifunze dunia inakwenda je na usitumbukie katika mtego wa kufuatilia maisha ya watu wengine.
  Mwanangu,litakapokuja suala la kutafuta kipato,kazi kwanza starehe baadae.Osha vyombo kabla ya kuangalia TV,fanya homework kabla ya ku chat na marafiki zako,hii itakujengea nidhamu siku za usoni,ila usiache kujiburudisha ukipata muda,msongo wa mawazo(stress) ni mbaya.Shibisha moyo wako kwa dua.
  Litakapokuja suala la kuchagua taaluma ,ikiwezekana chagua taaluma ambayo unaipenda,fuata moyo wako usijilazimishe kufuata mkumbo au kunifurahisha mimi mzazi wako.Katika taaluma yako fanya kazi kwa bidii na penda kazi yako.Hakuna mwajiri huwa anamlipa mwajiriwa stahiki yake,jifunze kudai unachostahili kulingana na uwezo na mchango wako kwa mwajiri.
  Nimekufundisha kuweka akiba,endelea kutunza unachokipata,usitumie zaidi ya kipato chako.Pesa zako ni zako,usiruhusu mtu mwingine akupangie matumizi ya pesa zako,labda iwe ni kwa majadiliano lakini si kwa shurti.Usicheze kamari,kuiba wala kujiunga na mipango kama ya DECI.Hakuna pesa ya bwerere,pesa hutafutwa kwa jasho,na kwa maana hiyo kamwe usiuze utu wako kwa ajili ya pesa,una uwezo wa kutafuta pesa kama walizonazo hao wengine na kwa njia halali.
  Utakapoingia kwenye mahusiano,usiangalie wengine wanasema nini,angalia wanafanya nini.Kuna siku utatumbukia kwenye lindi la mapenzi na utajiuliza 'hivi huyu ndo Mr Right?'.Ataweza kuwa ataweza asiwe.Akikuumiza usilie kupita kiasi ,jikusanye nyanyuka na usonge mbele.Muda ndo dawa ya machungu ya mapenzi,jipe muda utasahau,usijiue kwa sababu ya mtu mwingine mwenye baba yake na mama yake ambaye mmekutana ukubwani.Ukiolewa kumbuka mmeo kamwe hawezi kuwa baba yako,never.
  Kuwa na marafiki wachache lakini wa ukweli,kuna siku watakusaidia.Epuka kuwa na watu wanaokusifia tu,anayekukosoa ndiye bora zaidi hata kama inauma.Ogopa marafiki wambeya na wasengenyaji,hata wewe watakusengenya.
  Katika maisha yako utakutana na vikwazo vingi,jifunze kutokuwa na haraka ya kutoa maamuzi,tatizo lala nalo,litolee maamuzi ukiwa umetulia.Mwanangu,mdomo uliponza kichwa,chunga sana ulimi,neno likishatoka mdomoni ni kama cement ikisha kuwa zege hairudi kuwa cement.
  Mwanangu nakutakia maisha mema yenye baraka tele,na siku zote ujue ninakupenda sana hata kama kuna wakati huwa unaona nakukwaza,yote huwa ni kwa nia njema tu.
  Baba yako,
  Bishanga Abashaija
  Dar es salaam
  29/11/2011
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Safi kabisa. . . sasa umpe asome sio uuche hapa tu.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Duuuu! Aisee leo ndo nimejua kuwa mimi ni kilaaaaaaaaaaza. Hii kitu imetulia sana mkuu. Ulipoanza nusura niache kuendelea, maana ulipotaja Koku tu, nkajua unakuja na stori za 'katereroooooooooooooooooo'.

  Nakupa tano zako, halafu niruhusu nikopi na kui print tafadhali!
   
 4. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  nakopi fasta nakuprint sina uhakika na invisible ataichukuliaje..koku asisaau kujifunza kutunza senene ata kama ni mwaka bila kuchacha..pia wageni awape kahawa za kutafuna kila waingiapo kwake.
   
 5. Julieth Ms

  Julieth Ms Senior Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wosia mzuri sana kwa Koku, mama Koku nae vp umempa amsomee mwanae?
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Food for thought, nimeipenda sana.
   
 7. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  ruksa ndugu yangu.
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  we print tu Mkuu.
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Bishanga...Koku yuko Facebook au Twiitter nimu-add awe rafiki yangu.....:eyebrows:
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mama Koku? that is another story,tutaongea siku nyingine,naishi na binti yangu,anamaliza form 4.
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Bujibuji,hivi lile jambia langu nililisahau kwako jana? embu niletee fasta kuna katoto ka jirani hapa sikaelewielewi aisee.
   
 12. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Smart thinking brightens the future.
   
 13. Julieth Ms

  Julieth Ms Senior Member

  #13
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Form 4. atakuwa tayari ana boyfriend ni kheri ukawaisha huu ujumbe aweze kufanya maamuzi magumu
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280

  unautani na bishanga eeeh? atatafuta ak 47 kwa ajili yako
   
 15. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Nashukuru kwa huu waraka baba, nitafuata masharti yote na ninayazingatia kuanzia sasa. :eyebrows:
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  ushauri mzuri huu, akiufuata uatamsaidia. usiache kumsisitiza maneno haya kila leo usichoke
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  mmmmhhhh! usintie presha Jully tafadhali.
   
 18. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  we mwache tu au nitamwendea makorora nimshushe mshipa!
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  :lol::lol:....Mwambie Bishanga better the devil you know than the angel you don't know.
   
 20. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  huwa ninajitahidi Mkuu kuongea naye na wadogo zake,lakini ndugu yangu si unajua binadamu tunazaa mwili na si roho? yote ni kusali na kuomba tu.
   
Loading...