Waraka wa Waislam Kuhusu Uchaguzi Wakamilika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa Waislam Kuhusu Uchaguzi Wakamilika

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Junius, Jul 25, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ummy Muya

  KATIBU wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema waraka maalum utakaowaongoza waumini wa madhehebu hayo katika uchaguzi mkuu wa mwakani, umekamilika.

  Sheikh Ponda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam ambapo alisema waraka huo umesheheni ujumbe mzito kwa ajili ya Waislamu.

  Alisema waraka huo uko tayari kuanza kusambazwa kwa Waislamu wote nchini na huku ukitangazwa katika vyombo vya habari .

  "Waraka huu utakuwa mzito sana ukilinganishwa na ule ambao tuliutoa mwaka jana,"alisema.

  Kwa mujibu wa Sheikh Ponda waraka huo umeandaliwa na shura ya maimamu, inayojishughulisha na masuala ya siasa.

  Tayari Kanisa Katoliki nchini, limetoa waraka wake unaowataka wananchi kuchagua viongozi, waadilifu na wacha Mungu katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa mwakani.

  Hata hivyo, waraka huo umezua malumbano makali kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wakidai kuwa, unaweza kusababisha taifa kusarambaratika.

  Akizungumzia maandamano, Sheikh Ponda alisema wanasubiri kumalizika kwa kikao cha Bunge, ili kujiridhisha na hatua zilizofikiwa na chombo hicho katika kushughulikia suala la Mahakama ya Kadhi. "Maandamano ambayo tumepanga yana ujumbe hivyo hatuwezi kuyafanya mpaka kikao cha Bunge kiishe na kufahamu suala hili lipo katika hatua gani,"alisema

  SOURCE: MWANANCHI

   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Dini zinapoingia Siasa!
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Yeshakuwa hayo?
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nina hamu ya kuusoma huo waraka! Utolewe upesi huku uraiani tuanze kuuchambua.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Junius,
  Mkuu wangu navyoelewa mimi dini inatakiwa kuingilia siasa (sio Kuingia Siasa) ikiwa haki ya wananchi inakiukwa ama hakuna Uhuru wa kuabudu.. Lakini kama mambo haya yote yanatendeka kwa utashi wa waumini wenyewe na sii nguvu ya serikali (ambayo viongozi wake ni waumini wa dini hizo zhizo) basi bila shaka dini hazihitaji mguu wake ktk siasa. Dini wanatakiwa kushauri ama kuonya machafu yanayopingana na mafundisho ya dini hizo.

  Hakuna Aya, hadithi wala agano ambalo Mwenyezi Mungu amesisitiza tuwachague viongozi wa nchi zetu Mrengo wa siasa ikiwa nchi hizo zina Uhuru wote wa kuabudu Mungu huyo.
  Hii habari ya waraka na sijui MWONGOZO ni mwanzo wa serikali kuonyesha imekosa nguvu na mwelekeo. Hawa wote wanaoandaa waraka ni mawazo yao, ama niseme mawazo ya watu wachache ambayo hayawezi ku represent waumini wote wa dinin hizo kwa sababu hayatokani na Aya wala sura mojawapo ya dini hiyo.. Askofu au huyo Mufti ni viongozi wanaowakilisha sehemu ndogo sana ya wafuasi wa dini hizo...
  Kinachofanyika sasa hivi ni kama vile tunawaambia viongozi wa nchi yetu hawana dini ni makafir na sisi ndio waumini wa kweli.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ..viongozi wa Siasa nao waandike waraka wa jinsi ya kuchagua Maaskofu na Maimamu.

  ..watu wenye upeo wa kisiasa wangechukua huo Waraka wa Wakatoliki na kuchambua yale wanatokubaliana nayo na kuyaacha yale wasiokubaliana nayo.

  ..tatizo la CCM wanataka kila jambo walianzishe wao, kana kwamba wao ndiyo wenye hati miliki ya nia njema kwa taifa hili.

  ..WAISLAMU na WAKRISTO na siye tujifunze kutafuta COMMON-GROUND ktk masuala ya KITAIFA.

  ..pia dhana kwamba Mkristo/Muislamu safi ni yule anayepinga kila wazo/idea inayotolewa na Mkristo/Muislamu inapaswa kupigwa vita.

  ..nawasihi Maaskofu waonyeshe busara ktk kuupokea, kuutafakari, na kuuchambua waraka wa kina Sheikh Ponda.
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkandara
  Nafikiri maandiko yako yangekuwa sahihi kama hali halisi ingelikuwa hivyo.
  Ukiangalia pia uhalisia wa mambo wananchi wote waislamu kwa wakristu wazanzibari kwa watanganyika tunaishi kwa amani na upendo hatuna chuki binafsi.
  Sasa hizi kelele zinatoka wapi? ma Engineer wa siasa za Tanzania wamemaliza kazi.

  Kwa CHADEMA huku bara na hoja yao ya ufisadi imemalizwa umaarufu na hoja za kidini ,hoja ya ufisadi haina mshiko si tishio tena maana kuna hoja mbadala.

  Kwa CUF zanzibar nao hawana hoja tena ma Engineer wamefomulate hoja yenye mshiko yani ya muungano na gas sijui maafuta,kwa hoja hiyo cuf hawana hoja tishio zaidi wamekubali kunyongeka kwa tai lao wenyewe, ama wamejipeleka jela wenyewe kama kuku anavyojipeleka jela mwenyewe kwa kuhatamia mayayi.

  2010 itakuwa ccm hoyeeeee,kidumuuuuuu,fikra zidumuuuu
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wewe apo juu unapiga debe CCM oyee wakati wenzako maji shingoni ,hawajui wauwe wangapi ili waendelee kubaki madarakani.
   
 9. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Cuf mmeshatekwa na hoja zenu mmekubali kuziuuza ,kwa hiyo subirini kipigo kingine cha ballot.Mimi naomba msikatae kujaza fomu baada ya matokeo.

  Huku CHADEMA nao sijui wataibuka na hoja gani mpya? hii ya ufisadi haina mshiko tena.hapa tunahitaji mwanasiasa mwenye uwezo nafikiri wote waliopo uwezo wao umefika kikomo
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Vyama vya siasa, viongozi wa kisiasa, wasomi, wanaharakati na wapiga kura wote tunahangaika tu, tumeshaingizwa kwenye mifuko ya wanasiasa wala hatuna ujanja tena
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Haswa !!!hatuna ujanja ila tunajaribu kujihadaa wenyewe kwamba ujanja tunao.
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waraka wa waislam kwa mwelekeo tu na maneno ya akina Yahaya msoma nyota na wengineo hakika lazima utazungumzia waislam kuonewa na kutaka kuwachagua waislam hapo hakuna kitu na kama mnabisha mie nakaa kimya uletwe hapa watu watakimbia .Utakuwa aibu kwa nature tu ya jamaa zangu hawa pupa na papara .Mungu anawapigania watu na Mungu hapiganiwi na mwanadamu.Duh !! haya
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu, Mkuu kwa nini usiende Nyegezi ukasomee Upadre maanake siku hizi umeishiuwa vibaya vibaya..Wee nani lakini kufikiria watu wengine wana uwezo kuliko wewe.. mbona unaandika upupu mtupu (hasa siku hizi) kiasi kwamba nashindwa kuamini kama ulikwenda shule..
  Usitake kutukana watu na kufikiri wewe unajua zaidi kuwaita watu jamaa zako huku roho haikushuki kwa chuki zako binafsi.
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkandara mkuu wangu
  Wewe leo utasema upupu kwa kusema ukweli .Mimi sitaki kujitetea ila tuwape muda jamaa walete waraka hapa .Hutaona neno la National Unity hata moja na watataka OIC na Kadhi kwa kusema Kenya na Uganda na hata Zanzibar yupo na mengine .Kama huamini na bado ukadai naandika upupiu hata huwezi kusoma wakati unajibu hoja zangu basi tungoje .Mimi na wewe tukae ngoma italetwa jamvini .Nasema haya kwa ushahidi jamaa hawatakuja na hoja mbali na kuona Uislam unamalizwa maana ndiyo maneno yao akina Seif na Lipumba .Upupu hapa ni upi ? Haya ni mawazo yangu mkuu huna lazima ya kukubaliana nayo ila baada ya ngoma nitakutafuta uniombe msamaha kwa maneno haya uliyo nitolea .Wakija na waraka tofauti moderate na si wa kungoja Bunge liishe waje na hitimisho mie nitaomba msamaha .
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii ni kali!
  Kwa kifupi wananchi wanaonekana kukata tamaa kabisa... leo nimesikia mazungumzo ya watu tena wananchi wa kawaida kabisa wakisema:
  " Vyama vya upinzani ni kama deiwaka tu... chama tawala kinapata fungu kubwa na kuwagawia vyama pinzani kiduchu..hivyo hakuna namna wananchi watapata mbadala wa kuwapa nafuu ya maisha"...

  Mimi naona ni vema tu kila kikundi katika jamii wakafanya upembuzi wao na kuandika waraka/makabrasha na kuwaelimisha watu wao ..after all Civic education inapaswa kuwa mchakato endelevu na siyo kusubiri tu wakati wa uchaguzi.Badala ya kuwabeza viongozi wa dini na nyaraka zao nadhani ingekuwa vizuri tukawaunga mkono.
   
 16. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Civic education ni haki ya raia na inatakiwa itoelewe na serikali kwa lazima; lakini kumbuka civic education by nature huamsha ufahamu; wakati chama tawala hakitaki wanaofahamu maana wataanza kudai haki zao; so hakuna wa kutoa civic education endelevu hapo badala yake serikali itazidi kuwachanganya wananchi ili itawale vema; ndio njia pekee iliyobaki maana hawana mtaji mwingine- they are running their own shaddow; hili swala la civic ni jambo la wakati na si la haraka; mpaka mtanzania ateseke ndio itafikia wakati atasema; sasa basi; means TZ will be full or some times and not forever.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lunyungu,
  National Unity inajengwa na vitu gani?..kama wewe unaona OIC na mahakama ya kadhi ni upuuzi basi ya nini kuchangia ktk mada!.Mimi navyojua swala lolote zito ndilo mtu unaweka mawazo yako lakini upuuzi wa nini kuchangia ikwa nawe hutakuwa mpuuzi..

  Mkuu nasema haya kwa sababu hoja zako siku hizi zimekuwa Waioslaam hivi Waislaam vile.. wewe nani haswa kujiona kuwa una maamuzi yenye maana wakati mimi hatan unipe millioni sintajiunga na dini yako..Nayaona mapungufu mengi kama unagvyoyaoina wewe ktk Uislaam na ndio maana dini ni Choice ya mtu.. Huwezi kulinganisha na Jinsia wala rangi yamtu kwa sababu vitu hivi huwezi kuvibadilisha.
  Kinachokufanya wewe usipende mahakam ya kadhi na OIC kunadhihirishwa na wewe kuwa Mkristu. Ni madogo kati yamengi usiyokubaliana nayo ktk Uislaam hivyo ndio maana umekaa upande wa pili..Now why bother...
   
 18. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LUNYUNGU/MKANDARA mnaongea kwa manufa ya dini tu; mbona kuna misikiti na makanisa mnaweza kuwa wahubiri wazuri; nendeni huko; mie naona vema kila mmoja kwanza jua yafuatayo;
  1. humjui unayeabishana nae;
  2. Ila una uhakika ni Mtanzani
  3.Hujui ana mtazamo gani
  4. Ila unajua anao- ila haukuhusu

  Guys it means mmekosa kabisa point mnataka kuanza kuonyeshana nani anajua vema Biblia au Quran;

  Think critical and dont get biased guys otherwise mtakuwa maanalyst fake ( sure fake)
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hizi dini zinaelekea ''kutugawanya''...............!tukimaliza udini dhambi ya kubaguana itaendelea katika mfumo wa ukabila

  muda utafika tutaenda kufukua ''mwili-wa-hayati jk nyerere'' uje uongoze nchi,maanake ''wabia wake'' wameshindwa kuyatuliza haya machafuko
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mkuu Mkandara kweli unataka kugombana na Lunyungu kwa ibada yako ya Kadhi na chama chenu cha OIC ? Hivi Lunyungu hatakiwi kusema mawazo kwamba hataki Kadhi kwa kodi akaheshimiwa mawazo yake ? OIC hatuihitaji kama Nchi si kama Lunyungu.Kadhi awepo si kwa kodi yangu mimi na wazazi wangu mkubwa nendeni mkaanzishe kwa channels zenu za kiibada ni kosa kweli mie kusema msimamo wangu .Ibada yako wewe mie siijui tena unataka na pedsa yangu ikusaidie wewe kufanya ibada uende peponi ukifa mie niishie njiani ? Aalaaaaaaaaaaaaaaaaaa Mkandara Mkuu mbona udini sasa unalia lia na wewe naona mada zote dini unakuja kama Seif kuutetea Uislam ?

  Narudia Kadhi kwa kodi yangu sitaki na kwa kuwa ni ibada yenu ndugu zanguni endeleeni msihusishe dola na attention toka Serikalini .OIC haituitaki kama mnaona kuna haja waambieni CCM walio waahidi .
   
Loading...