Elections 2010 Waraka wa Waislam Kuhusu Uchaguzi Wakamilika

hakika wakatoliki wataleta balaa huko tanganyika. hebu tupeni Data.
1.hawa wakatoliki ni % ngapi ya wakristu huko Tanzania ( yaani Walutheri, waanglican,wasabato n.k).
2. Nini tamko la askofu mkuu wa KKKT kuhusu waraka wa kanisa katoliki?
3.Nini tamko la Askofu mkuu wa Anglican kuhusu waraka wa wakatoliki?
4. je Waandishi wenzangu mmewahoji hao viongozi wengine wa madhahebu mbali mbali za Wakristu, mbona hamtendi haki?
5. Je kwani tamko la wakatoliki ni tamko la wakristu wote huko Tanzania?


Mola ibariki nchi yangu niipendayo
 
naunga mkono waraka wowote au mpango wowote wa makundi ya watanzania kujitolea kufundisha watanzania wenzao wajibu wao wa kuchagua viongozi wanaoweza kutegemewa kufanya kazi wanayotumwa na wapiga kura.
Serikali yetu haiwezi kutoa elimu kwa watanzania wote, inabidi wasaidiwe jamani,
natumaini waajiriwa wa serikali wenye jukumu la kuelimisha umma wa wapigakura watakubali kuwa huu ni msaada mkubwa sana, tena bila malipo yoyote,

mimi kama mlipa kodi nashukuru sana madhehebu yaliokitolea, yakatoa sadaka ya waamini wao kuandaa haya maandishi.
Mungu awabariki,

TANZANIA INAAMINI KATIKA MUNGU, ILA HAIFUNGAMANI NA DINI YOYOTE.
 
Back
Top Bottom