Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

Waraka wa Tambwe Hizza kwa watanzania

NA RICHARD TAMBWE HIZZA

WIKI hii waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali nchini waliandamana kulaani kuuawa kwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Chanel 10 huko Iringa, kifo cha mwandishi huyu kwa bahati mbaya na kwa mara nyingine tena kimewagawa wananchi katika makundi yanayotofautiana kifikra kuhusu chanzo na hatimaye kufariki kwake.

Wapo wanaoona na kuamini polisi wametumia nguvu kubwa katika kukabiliana na tatizo lililokuwepo, wapo wanaoamini kwamba jeshi la polisi lilikuwa linatimiza wajibu wake na madhara haya makubwa yaliyotokea yanatokana na CHADEMA kuendeleza ghasia katika nchi na kujaribu kuifanya isitawalike kama walivyoahidi baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi mkuu uliopita (walishinda viti 23 kati ya majimbo 239).

Hata hivyo, kabla ya kuingia katika tafakuri pana zaidi zinazotokana na msiba huu sina budi kutoa pole kwa familia ya Mwangosi, waandishi waliokuwa karibu naye katika kufanikisha majukumu yake ya uandishi wa habari, Kituo cha Channel 10 na Watanzania wote kwa ujumla, kwa kuondokewa na mwananchi mwenzetu katika mazingira ambayo wote hatukuyategemea.

Tumeshuhudia wakati taifa likiwa katika simanzi nzito kutokana na msiba huu, wapo wenzetu walioamua kuutumia kama turufu ya kuleta chuki baina ya jeshi la polisi na waandishi na zaidi umma wa Watanzania ambao usalama wao na mali zao unategemea sana uwepo wa jeshi hilo. Kuna mambo mengi ambayo nimekuwa najiuliza na ningependa Watanzania wote tujiulize, hivi ghasia zilizosababisha msiba huu zilisababishwa na nini/nani?

Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao? Na je, uhalali wa uwepo wa jeshi hilo ungeendelea kuwepo?

Wananchi wote tunapaswa kuheshimu sheria na polisi wana jukumu la kutulazimisha kufuata sheria tunapozikiuka vikiwemo vyama vya siasa, najua sheria ya vyama vya siasa inavipa fursa vyama kufanya maandamano na mikutano baada ya kutoa taarifa polisi, lakini sheria hiyo hiyo inasema vitafanya hivyo endapo tu kama havitapata amri pingamizi kutoka polisi (sheria ya vyama vya siasa 1992 kifungu cha 11).

Tujiulize kulikuwa na ulazima gani kwa CHADEMA ambao mwaka mzima wamekuwa wakiruhusiwa kufanya mikutano na maandamano kulazimisha kufanya mkutano uliosababisha kifo baada ya kupata amri pingamizi? Kama waliona polisi hawakuwafanyia haki je ilikuwa vyema kuandaa mapambano dhidi ya polisi? Jje walichukua hatua yoyote ya kisheria dhidi ya polisi au hawana imani na vyombo vya kisheria kama ambavyo Tundu Lissu anavyoziponda mahakama zetu bila kuheshimu kwamba zilimpa ushindi yeye binafsi katika kesi yake ya uchaguzi aliyofunguliwa na mgombea wa CCM, na zile zilizokipa ushindi chama chake zilizowavua ubunge wana CCM huko Sumbawanga na Igunga.

Naamini ili jeshi la polisi liweze kuendelea kulinda amani ndani ya nchi ni lazima tuliamini na lazima tujue kwamba lipo, likizuia jambo kwa mujibu wa sheria wote tuheshimu vinginevyo litakuwa halina sababu ya kuwepo. Si mara moja au mbili mamlaka za umma na vyombo vya sheria viliamua mambo muhimu katika maendeleo ya taifa, lakini yalipata upinzani hadi pale polisi ilipotumia nguvu kuhakikisha sheria inafuatwa na utekelezaji wake unatimia.

Je, kumfukuza waziri katika hafla ya kulaani mauaji na kumkaribisha mwana-CHADEMA Dk. Lweitama kuhutubia na kuilaani serikali ni sawa? Je, ni sawa kulilaumu jeshi zima la polisi kwa tatizo lililojitokeza sehemu moja ya nchi tena katika kutimiza wajibu wao? Kitendo cha kutowalaani walioanzisha uvunjaji wa sheria uliosababisha ndugu yetu Mwangosi kupoteza maisha katika umri mdogo kinaashiria nini kutoka katika taasisi zetu za habari?

Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?

Wote tumesikitishwa na msiba huu sidhani kama ni vyema kuendelea kushambulia jeshi la polisi bali kuangalia nani ameanzisha sokomoko ili awajibishwe kisheria, kama ikibainika aliyeua ni raia wa kawaida sheria ichukue mkondo wake, pia ikibainika muuaji ni askari akiwa katika kutimiza majukumu yake ni vyema taratibu za kijeshi na mahakama zitumike badala ya kuendeleza chuki zisizo na msingi.

Tusijisahau wote tunawahitaji polisi kama ambavyo tulikuwa tunamhitaji ndugu yetu Mwangosi nikiwemo mimi niliyeshirikiana naye katika shughuli mbalimbali. Tusiwe na hasira maana wahenga walisema hasira hasara. Tutafute suluhisho la yanayotokea yasijirudie.

Kwenye Red, Nafikiri angeuawa Mwanao ungekuwa kwenye position nzuri sana ya kuuliza haya.....Kwa Hivo Kule Bububu Polisi hawakuwepo?au kule Hakuna Wananchi wanaohitaji ulinzi wa Polisi?its Only Iringa they need Police eeeh?Too low Argument to justify such a Crime....
 
Tambweeeee....bado upooooo!!! Baba January kakutosa hivyooo??? Usijali, ukitoa vi-waraka kama hivi vitatu au vinne utakumbukwa tu!! CDM ilitii 'amri' ya kusitisha mikutano ya nje ya M4C ila kwa vile tayari walishakuwa Iringa wakaruhusiwa kuendelea na mikutano ya ndani (key word hapo ni kuruhusiwa). Acha kufikiri kwa 'masaburi' japo kwa dakika mbili then jiulize kama chama cha kisiasa kinakatazwa kufanya hata mikutano ya ndani maana yake nini?? Mtapaka rangi zooote lakini kwa hili limewavundia CCM
 
Bomu la machozi kupigwa tumboni,katika hali ya kawaida hilo linaweza kuwa kosa la kiufupi,any one can make mistake even kwenye kazi aliyoisomea zaidi ya miaka minne,inatutokea wote makazini,haiyumkiniki bomu la machozi akatandikwa nalo mtu tumboni kwa makusudi,ni wazi ilikua ni bahati mbaya,lakini chadema wangetii amri halali ya polisi bahati mbaya za namna hii zingeepukika,kwanini chadema walikua wakaidi hasa slaa maana tunaambiwa siku moja kablaya tukio alituma ujumbe kwa IGP akimuagiza aje na mabomu ya machozi nafikiri ya kutosha ambayo ndio yamegharimu maisha ya ndugu yetu,ni huruma na unyonge labda niseme wa IGP huyu wa sasa otherwise ingekua kipindi cha mahita slaa alitakiwa kuwa ndani anaisadia polisi now kama ilivyowahi kutokea kwa lipumba enzi za igp mahita

As I have said, two wrongs dont make no right, sipendi mtu anayejitetea kwa makosa mengine. Polisi kama wanatuhumiwa wakubali tu tuhuma or else waje na maelezo yanayojitegemea na sio kusema CHADEMA ndio wanahusika. Na kama CHADEMA wamefanya makosa basi washitakiwe kwa mujibu wa sheria.
 
ushindi wa ccm hauujui????kuna mengi yamefanyika hapo,kila mbunge anajua ameingiaje?wapo hata waliovua CHUPI,na wapo waliolalamika huko kwenye semina zao bungen kuwa hata ubunge unahusisha rushwa za NGONO

Lakini mzee mlitegemea mshindane vipi na ccm na muwashinde wakati nyie kuna sehemu nyingin hamkua hata na wagombea,is that possible katika hali ya kawaida tukiweka ushabiki pembeni?mbona hii hamuisemi mko busy kuimba wimbo wa rushwa as if ndio sababu iliyofanya mshindwe vibaya.Na hiyo rushwa hamuisemi moshi mjini ama kigoma,karatu,Hai,lindi mjini,nyamagana au pemba,why?au kwa kuwa upinzani ulishinda sehemu hizo,kwa hiyo mnataka mshindage nyie tu hata kama hamna uwezo ikishinda ccm rushwa,tujenge utamaduni wa kukubali kushindwa ndipo tutaweza kujipanga
 
Mr tambwe Hiza sio kama hana akili ila ametumwa kujaribu kuwa danganya wananchi, kwa kufanya hivyo anapata pesa ya kula. Sithani kama haelewi anacho ongea, nafikiri anaona kama watu wote hawaelwi kitu.

Chama tawala kinafikiri ni watu wote hawana akili za kufikiria.

POLE SANA MR TWAMBE you are just beating around the bush, people know what is going on. POLE MKUU kwa leo huja mdanganya mtu.
 
Anatafuta kibarua kwa Mukama kama ilivyokuwa kwa Makamba. Kashatumika kamba dume sasa kawekwa kando.
Tambwe, sasa huwezi danganya mtu. Hata kabla hujaleta 'majibu' watu wanayo tayari.
 
Kama sharti lake la kurudi ccm ni kumlala mama yake, na tayari amerudi ccm maana yake amesha timiza sharti la kurdi ccm. Tunapo mjadili mr Tambwe lazima LOGIC zitumike.
 
Je kulikuwa na ulazima kwa CHADEMA kukaidi amri ya polisi ya kusubiri sensa ipite? Je, ukaidi wa CHADEMA siyo chanzo cha maafa yaliyotokea na yanayotokea mara kwa mara nchini? Je, ingekuwa sawa kwa jeshi la polisi kuwaachia CHADEMA kufanya shughuli ambayo walikwisha wazuia wasiifanye? Je, polisi ingewaachia kufanya jambo ambalo walikwishawazuia
wangekuwa wanatimiza sheria na wajibu wao?

Hapa ndiyo maswali mengine yasiyo na majibu yanapoanza, kwa nini tamko lililotolewa na CHADEMA na lile la wanahabari yanashabihiana. Kwa nini wanahabari hawakuilaumu CHADEMA hata mara moja kwa kutokutii sheria na kuanzisha ghasia zilizosababisha maafa ya ndugu yetu. Nadhani tunahitaji tafakuri pana zaidi. Je wametumwa? Wana hasira? au nao wameanza kushirikishwa katika ajenda za siri dhidi ya serikali na vyombo vyake?

Bw Hizza, nadhani unahitaji umakini zaidi kabla ya kuzungumza jambo kama hili, nadhani kilichokuwa kimekubalika ni kutoendesha mikutano ya nje mpaka sensa ipite, sasa ule ulikua mkutano wa nje mpaka polisi wakazuie? Mbona CCM walikuwa wakiendelea na vikao vya namna hiyo? Na ushahidi wa vikao vyao uko humu humu, jinsi walivyokua wakikata mauno bila usimamizi wa polisi. Hebu chukua muda wako upitie mada iliyoandikwa na FRANCIS GODWIN kuhusu tukio zima mpaka kifo, kisha ndipo urudi kutoa mada hapa, hili jukwaa la wenye fikra pevu, si rahisi ukaja na blablaa kana kwamba unazungumza na watoto, unless kama umetumwa.
 
Ukiwa ccm unakuwa zezeta,hamuwezi kulaani mauaji yaliyofanywa na polisi kwa sababu si ulikuwa mkakati wa siri kwenye chama chenu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
BADO kumbe wengine wana majina fikra na uchambuzi unadhihirisha uvivu wa kufikiri, Yaani yeye anaona SENSA inafanyika Iringa tu, na je kama CHADEMA ndio walivunja amri kwa nini waue mwandishi wa habari na si viongozi wa CHADEMA mabao hawakutii amri sio hivyo kwa nini mikutano ya CHADEMA Ndio inawekea vipingamizi tu hakujioji haya maswali kipindi anandaa hoja yake.
Kwa tukio hili lililotokea Iringa CCM wanahusika kwa kutoa amri hata wakatae na lengo ni kuonyesha chadema chama cha fujo kama kampeni za mwaka 2010 walivyokuwa wanasema. Nakitendo cha bwana Tambwe kusema Tundu alipewa ushindi na mahakama anakosea mahakama sana kwani uthibitisho wa madai ndio haukutosheleza kwani mahakam uwa haipo sehemu ya tukio bali wanchopelekewa niushidi na asome ushahidi wa LISU ndio aelezee hayo mambo.
 
tambwe alimaliza hata darasa la 7 jamani?mbn maelezo yake ni kama aliishia la6 B?
 
Kwani kukaidi kwa chadema si ndio chanzo cha Mwangosi kwenda kuchukua habari?. Basi kama ni hivyo polisi wangemwacha ili atupashe ukaidi huo. Hii ingesaidia sana wao kutolaumiwa. Sasa wao kwa chuki binafsi wakamhukumu hata yule ambaye labda taarifa yake ingejenga uhalali wa operation yao. Ujinga wa jeshi letu na chuki binafsi ndo chanzo cha kifo, sio kukaidi kwa chadema. Hata kama ni kukaidi, kwa kiasi walivyokua wamemzunguka vile walishindwa kumdhibiti kweli? Baadhi ya wanasiasa wa bongo mmelaanika kweli, yani hata makosa yakitokea mnajitahidi kujenga hoja za kujikosha!!! Watanzania wa leo sio wa jana hatudanganywi na vihotuba vyenu uchwara, tunaweza kuona na kufanya uchambuzi mzee. Labda muende Mars mkadanganye huko sio hapa TZ
 
Tambwe aigombanisha CCM na Waandishi!

----Kuhusu kutafuta suluhisho........:
Suluhisho ni CCM kuacha kulitumia Jeshi la Polisi kwa manufaa yake ya kisiasa na Jeshi la Polisi kufanya kazi yake kwa weredi. Hatuhitaji mtaalamu kutoka ng'ambo kujua suluhisho la mauaji haya yanayofanywa na Polisi. Wala hatuhitaji tume kutafuta suluhisho la mauaji haya.
 
Huo Waraka ulipaswa upelekwe kwenye Kamati ya Nchimbi kwani hapa umepotea njia.Kama sikosei Dk. Lweitama alishasema kwenye Sibuka T.V. kuwa yeye ni mwana C.C.M. sasa kumgeuzia kipande hapa kuwa ni mwana CHADEMA humtendei haki.
 
Nimeamini yale maneno kwamba hili jeshi la polisi ni policcm. Sababu kila kiongozi wa chama na serikali ukimsikia analitetea jeshi la polisi. Kama wanalindana hivi, ila Tambwe Hizza hapa Jf anatumika kutolea mfano wa kilaza, sasa hili shairi limebainisha kabisa ukilaza wake, in short jamaa ni mweupe kichwani.
 
Back
Top Bottom