Waraka wa Mchungaji Mtikila kwa Edward Lowassa

Waraka wa Mchungaji Mtikila kwa Edward Lowassa

1. Tunao ushahidi mzito unaothibitisha
kwamba Edward Lowasa na
wenzake walianza kampeni ya urais
ndani ya chama chao kabla ya
wakati, na kwamba chama chao kiliwapa
adhabu ya kutofanya siasa
kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowasa
ameanza kampeni ya urais
Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa
hadhara wa kampeni haramu
na kumwaga rushwa ya kutisha!
2. Kama ni wadhamini alipaswa
kuwapata katika ofisi za chama chake,
katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na
mikoa miwili tu Unguja na Pemba,
wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini
Edward Lowasa amefanya mikutano nchi
nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi
katika kila mkutano wa hadhara, mambo
atakayofanya kama wakimpa kura zao
awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi,
ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria
za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na
Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue
mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.
3. Edward Lowasa amevunja Katiba ya
Nchi na Sheria ya kiwango cha
fedha kinachoruhusiwa kutumika katika
shughuli halali za Uchaguzi,
kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za
uchunguzi wa kifedha nchini,
upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni
mlazima wanayo kazi muhimu sana ya
kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya
fedha yanayomwagwa nchini na fisadi
Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa
namna gani, kumehusika ‘’Money
laundering’ au la, kama mapato ya
mapesa hayo yote ni halali, na kama
mapato hayo yote yalilipiwa kodi
inayopasa kwa ajili ya Taifa.
Ni marufuku kabisa tena ni makufuru
Edward Lowasa kuruhusiwa
kugombea urais, kwa sababu amevunja
Katiba ya Nchi na Sheria na
Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya
kustahili kugombea uongozi wa nchi
yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa
Sheria, Kanuni na
taratibu za Utawala wa Sheria
4. Edward Lowasa, kwa kujimilikisha
maeneo nchi nzima kwa kutumia kifisadi
Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa
katika hatari kubwa ya mmwagiko wa
damu baina ya wakulima na wafugaji,
baada ya kueneza nchi nzima makundi ya
ng’ombe wake, na kusababisha mapigano
makali ya mara kwa mara kila mahali
nchini kati ya wafugaji wake na
wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata
katika kampeni yake haramu Lowasa
ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo,
ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi
wa nchi yetu na ndiyo shughuli
inayotunza uhai wa asilimia 95 ya
wananchi!
Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi
yao, kuwaua ovyo, kuwaonea
kiasi cha kufisha matumaini yao katika
kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya “Kilimo
kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!
5. Edward Lowasa ni mwiko kabisa
kupewa kugombea urais, kwa
sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri
wa Ardhi akajitajirisha na
kujipatia maeneo makubwa ya ardhi
nchini kote, bali alitumia kifisadi
zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya
Waziri Mkuu, katika uagizaji wa
mashangingi ya Wabunge, mawaziri,
wakuu wa Mikoa na Wilaya.
6. Edward Lowasa alikemewa mnamo
mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere
anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao,
alipotaka kugombea urais, kwa sababu
alikuwa fisadi papa, wala hakuweza
kujitetea kwavile utapeli wote
aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada
ya mabiashara haramu mengi na kulipora
sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli
wa “kununua mvua Thailand” na kuliibia
Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia
kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni
fisadi-nyangumi. Ni mlemavu wa rushwa
tu wa kununuliwa na mapesa machafu
anayomwaga Lowasa, anayeweza
kumruhusu fisadi Edward Lowasa
agombee urais.
Sifa za mtu wa kukugombea Urais
zimeelezwa bayana na Mwenyezi
Mungu katika Kumbukumbu la Torati
17:15-20, ambazo Edward
Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa
awali alikemewa na Mwalimu
Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama
“Baba” yao, kuwa hafai kabisa kuwania
urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa,
kama alivyomtangaza hata Reginald
Mengi pale alipolazimika kujiuzulu
Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa
kampuni hewa ya Richmond, lakini leo
akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa
eti anataka urais!
Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora
vibaya sana Nchi hii kama Sigh Setti na
hata Nazir Karamagi wote wamo katika
genge la Edward
Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald
Mengi leo kuungana na fisadi
Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye
mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na
mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na
mpango wa Chadema
wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka
feki wa kujaribu kuupotosha
ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.
Katika uwaziri wake katika ofisi ya
Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wakewa
Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya
ufisadi ambao katika nchi kama China
zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao
angekuwa wa kupigwa risasi hadharani,
lakini katika nchi yetu anatafuta urais!
7. Edward Lowasa AFYA yake imempiga
marufuku kugombea Urais!
Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja
ya mashart makuu ni lazima mwombaji
awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni
lazima ajira ya kila mwombaji itegemee
taarifa ya kitaalamu ya madaktari,
inayothibitisha kwamba hana dosari
kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa
sababu:
a. Majukumu yote atakayopewa
mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu
kwa kutumia viungo vya mwili wake,
kwahiyo viungo vyake vyote
ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa
ajili ya kazi.
b. Hata kama kwa uthibitisho wa
kitaalamu wa madaktari mwajiriwa
anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa
na hitilafu katika viungo
vingine vya mwili wake huathiri afya ya
akili zake na uwezo wa
utendaji wa akili zake.
c. Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa
sababu ni pamoja na kusimamia
shughuli zote za maendeleo ya nchi
nzima, na matatizo yote
yanayowatokea wananchi wote kila
walipo, na kusimamia
utekelezaji wa majukumu yote ya
watendaji wote katika Taifa,
hivyo kwamba maamuzi sahihi
yanatokana na afya bora yenye
kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili
wakati wote
d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo
wa kifikira na kusababisha
maamuzi mabovu, ambayo huleta athari
mbaya sana kwa Taifa. Na
udhaifu huo huathiri mpaka maadili na
hata uzalendo wa huyo
kiongozi mdhaifu. Kwa mfano
akipatikana Rais anayeishi kwa
matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai
kabla hajaweka sawa
mambo yake na ya familia na jamii yake
atatumikia maslahi yake
zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya
likawa limelikosesha Taifa
kipaumbele, na kuliangamiza
kimaendeleo!
e. Wanaowania kugombea urais ni lazima
wachunguzwe kwa makini
sana afya zao, kwa sababu kukifanyika
makosa akatawazwa
mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda
kuwa mzigo mzito sana kwa
Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji
wa uhai wake ndani na nje
ya nchi, kukosekana na umakini
anaopasa kuwa nao kwa ajili ya
dhamana kubwa aliyopewa n.k.
Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu
sana hata kwa kumwona kwa
macho tu, kabla ya uchunguzi wa
kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa
hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani
amekosa sifa muhimu sana ya afya bora,
ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote
anayestahili kupewa dhamana kubwa
sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata
kugombea urais kwenyewe anatafuta
kutokana na hitilafu ya kiafya,
iliyosababisha udhaifu katika kufanya
maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati
mbaya anagombea asichokiweza kabisa.
Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa
Ubunge na hata wa Udiwani
wachunguzwe kwa makini afya zao kabla
ya kupewa kugombea, na hata
kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa
utumishi wao, kama kweli tunalithamini
na kuliheshimu Taifa.
Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili
ya Nchi ambao ni zaidi ya
maadili ya kizalendo, maono, vipawa na
AFYA BORA. Ni dhana potofu
sana kwamba sifa ya urais ni
kushabikiwa na umati wa watu! Kwa
sababu wengi hufuata mapesa na
husombwa hata na magari ili umati
wa kishabiki tu upatikane. Lakini
kumpenda mtu huwa lazima kuwe na
sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu
au ‘psychological deficiency’.

@END; PINGAMIZI HALIEPUKIKI
 
Bora nimchague ninaeaminishwa Ni fisadi kuliko wale wasafi ambao Ni majizi papa, kama mmachinga na mkerewe! Kura 15 za familia yangu Ni kwa Lowasa, CCM chama cha kufunga majizi hapana maana wewe ndiye unaendeleza umaskini kwa kuiba Mali ya umma
 
hahahaha kura yako tunaiomba mwambie na magufuli pia
 
Umma wa Watanzania utawaukumu Ccm kwa kuwatengeneza Mafisadi wanaopata upako chadema
 
Hatubabaiki NG'OOOO. Jiwe na CCM tunachagua Jiwe,
 
MKUU mbn we ndo unahangaika uzi unachangia pekeako

Tuliza povu ndugu...mafisadi wote wako ccm...sisi tumeridhika na fisadi lowasa..katika kashfa zako hamna ata moja mpya porojo zile zile...

Poleni sana
 
Watanzania bado wamelala. Wakishaamka watakuta nchi nyang'anyang'a haitamaniki

Magufuli hoyeeeeee
 
Ni ratiba ya kuchukua form tu imewafanya ccm wamepata kiwewe like headless chicken.
 
MKUU mbn we ndo unahangaika uzi unachangia pekeako

Ungejadili walau kwa kubalance yaani

1. Ungedadavua uzuri na uovu wa magufuli with evidence beyond doubt

2. Ungedadavua uzuri na uovu wa Lowasa with evidence beyond doubt

Kwakufanya hivyo sisi wachangia ungetutendea haki kuujadili uzi wako kwa kina.
 
1. Tunao ushahidi mzito unaothibitisha
kwamba Edward Lowasa na
wenzake walianza kampeni ya urais
ndani ya chama chao kabla ya
wakati, na kwamba chama chao kiliwapa
adhabu ya kutofanya siasa
kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowasa
ameanza kampeni ya urais
Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa
hadhara wa kampeni haramu
na kumwaga rushwa ya kutisha!
2. Kama ni wadhamini alipaswa
kuwapata katika ofisi za chama chake,
katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na
mikoa miwili tu Unguja na Pemba,
wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini
Edward Lowasa amefanya mikutano nchi
nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi
katika kila mkutano wa hadhara, mambo
atakayofanya kama wakimpa kura zao
awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi,
ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria
za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na
Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue
mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.
3. Edward Lowasa amevunja Katiba ya
Nchi na Sheria ya kiwango cha
fedha kinachoruhusiwa kutumika katika
shughuli halali za Uchaguzi,
kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za
uchunguzi wa kifedha nchini,
upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni
mlazima wanayo kazi muhimu sana ya
kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya
fedha yanayomwagwa nchini na fisadi
Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa
namna gani, kumehusika ‘’Money
laundering’ au la, kama mapato ya
mapesa hayo yote ni halali, na kama
mapato hayo yote yalilipiwa kodi
inayopasa kwa ajili ya Taifa.
Ni marufuku kabisa tena ni makufuru
Edward Lowasa kuruhusiwa
kugombea urais, kwa sababu amevunja
Katiba ya Nchi na Sheria na
Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya
kustahili kugombea uongozi wa nchi
yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa
Sheria, Kanuni na
taratibu za Utawala wa Sheria
4. Edward Lowasa, kwa kujimilikisha
maeneo nchi nzima kwa kutumia kifisadi
Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa
katika hatari kubwa ya mmwagiko wa
damu baina ya wakulima na wafugaji,
baada ya kueneza nchi nzima makundi ya
ng’ombe wake, na kusababisha mapigano
makali ya mara kwa mara kila mahali
nchini kati ya wafugaji wake na
wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata
katika kampeni yake haramu Lowasa
ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo,
ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi
wa nchi yetu na ndiyo shughuli
inayotunza uhai wa asilimia 95 ya
wananchi!
Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi
yao, kuwaua ovyo, kuwaonea
kiasi cha kufisha matumaini yao katika
kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya “Kilimo
kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!
5. Edward Lowasa ni mwiko kabisa
kupewa kugombea urais, kwa
sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri
wa Ardhi akajitajirisha na
kujipatia maeneo makubwa ya ardhi
nchini kote, bali alitumia kifisadi
zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya
Waziri Mkuu, katika uagizaji wa
mashangingi ya Wabunge, mawaziri,
wakuu wa Mikoa na Wilaya.
6. Edward Lowasa alikemewa mnamo
mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere
anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao,
alipotaka kugombea urais, kwa sababu
alikuwa fisadi papa, wala hakuweza
kujitetea kwavile utapeli wote
aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada
ya mabiashara haramu mengi na kulipora
sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli
wa “kununua mvua Thailand” na kuliibia
Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia
kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni
fisadi-nyangumi. Ni mlemavu wa rushwa
tu wa kununuliwa na mapesa machafu
anayomwaga Lowasa, anayeweza
kumruhusu fisadi Edward Lowasa
agombee urais.
Sifa za mtu wa kukugombea Urais
zimeelezwa bayana na Mwenyezi
Mungu katika Kumbukumbu la Torati
17:15-20, ambazo Edward
Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa
awali alikemewa na Mwalimu
Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama
“Baba” yao, kuwa hafai kabisa kuwania
urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa,
kama alivyomtangaza hata Reginald
Mengi pale alipolazimika kujiuzulu
Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa
kampuni hewa ya Richmond, lakini leo
akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa
eti anataka urais!
Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora
vibaya sana Nchi hii kama Sigh Setti na
hata Nazir Karamagi wote wamo katika
genge la Edward
Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald
Mengi leo kuungana na fisadi
Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye
mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na
mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na
mpango wa Chadema
wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka
feki wa kujaribu kuupotosha
ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.
Katika uwaziri wake katika ofisi ya
Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wakewa
Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya
ufisadi ambao katika nchi kama China
zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao
angekuwa wa kupigwa risasi hadharani,
lakini katika nchi yetu anatafuta urais!
7. Edward Lowasa AFYA yake imempiga
marufuku kugombea Urais!
Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja
ya mashart makuu ni lazima mwombaji
awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni
lazima ajira ya kila mwombaji itegemee
taarifa ya kitaalamu ya madaktari,
inayothibitisha kwamba hana dosari
kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa
sababu:
a. Majukumu yote atakayopewa
mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu
kwa kutumia viungo vya mwili wake,
kwahiyo viungo vyake vyote
ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa
ajili ya kazi.
b. Hata kama kwa uthibitisho wa
kitaalamu wa madaktari mwajiriwa
anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa
na hitilafu katika viungo
vingine vya mwili wake huathiri afya ya
akili zake na uwezo wa
utendaji wa akili zake.
c. Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa
sababu ni pamoja na kusimamia
shughuli zote za maendeleo ya nchi
nzima, na matatizo yote
yanayowatokea wananchi wote kila
walipo, na kusimamia
utekelezaji wa majukumu yote ya
watendaji wote katika Taifa,
hivyo kwamba maamuzi sahihi
yanatokana na afya bora yenye
kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili
wakati wote
d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo
wa kifikira na kusababisha
maamuzi mabovu, ambayo huleta athari
mbaya sana kwa Taifa. Na
udhaifu huo huathiri mpaka maadili na
hata uzalendo wa huyo
kiongozi mdhaifu. Kwa mfano
akipatikana Rais anayeishi kwa
matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai
kabla hajaweka sawa
mambo yake na ya familia na jamii yake
atatumikia maslahi yake
zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya
likawa limelikosesha Taifa
kipaumbele, na kuliangamiza
kimaendeleo!
e. Wanaowania kugombea urais ni lazima
wachunguzwe kwa makini
sana afya zao, kwa sababu kukifanyika
makosa akatawazwa
mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda
kuwa mzigo mzito sana kwa
Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji
wa uhai wake ndani na nje
ya nchi, kukosekana na umakini
anaopasa kuwa nao kwa ajili ya
dhamana kubwa aliyopewa n.k.
Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu
sana hata kwa kumwona kwa
macho tu, kabla ya uchunguzi wa
kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa
hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani
amekosa sifa muhimu sana ya afya bora,
ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote
anayestahili kupewa dhamana kubwa
sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata
kugombea urais kwenyewe anatafuta
kutokana na hitilafu ya kiafya,
iliyosababisha udhaifu katika kufanya
maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati
mbaya anagombea asichokiweza kabisa.
Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa
Ubunge na hata wa Udiwani
wachunguzwe kwa makini afya zao kabla
ya kupewa kugombea, na hata
kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa
utumishi wao, kama kweli tunalithamini
na kuliheshimu Taifa.
Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili
ya Nchi ambao ni zaidi ya
maadili ya kizalendo, maono, vipawa na
AFYA BORA. Ni dhana potofu
sana kwamba sifa ya urais ni
kushabikiwa na umati wa watu! Kwa
sababu wengi hufuata mapesa na
husombwa hata na magari ili umati
wa kishabiki tu upatikane. Lakini
kumpenda mtu huwa lazima kuwe na
sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu
au ‘psychological deficiency’.

@END; PINGAMIZI HALIEPUKIKI
Dongo limesharushwa kwa mkwere kuhusuana na Richmond ,msafisheni mkwere sasa ila sisi tunasema Lowassa sio fisadi
 
Back
Top Bottom