Waraka wa Mchungaji Mtikila kwa Edward Lowassa

Swali:Kama kweli EL ni fisadi mliwezaje kukaa naye ndani ya ccm kwa muda wote huo?ninachoweza kusema ni kwamba ameondoka ccm baada ya kuona ufisadi wenu umezidi kiwango ni hivyo kuhatarisha usalama wa taifa hili.
 
Cc AssadSyria:
hivi unajua kuijadili afya ya mtu na kutoa tathmini ni kosa la jinai? Wajua hata daktari anayemtibia mgonjwa hatakiwi kuizungumzia afya ya mgonjwa bila ridhaa ya mgonjwa au chini ya kiapo?
Wewe umeupata wapi ujasiri wa kuisemea afya ya Lowasa?
Ndiyo maana nimekuambia wanaokutuma watakukana swala hili likifikishwa mahakamani. Acha kutumika na umwombe radhi Lowasa asije anza na wewe. Najua huna ubavu wa kudhibitisha uliyoyaandika humu popote kwani huna ushahidi zaidi ya porojo za kijiweni lumumba. Waambie na wenzako ninaisubiri ile sheria ianze kazi niwafunze adabu mahakamani kwa heshima ya Lowasa na kwa gharama zangu.
 
Cc AssadSyria:
hivi unajua kuijadili afya ya mtu na kutoa tathmini ni kosa la jinai? Wajua hata daktari anayemtibia mgonjwa hatakiwi kuizungumzia afya ya mgonjwa bila ridhaa ya mgonjwa au chini ya kiapo?
Wewe umeupata wapi ujasiri wa kuisemea afya ya Lowasa?
Ndiyo maana nimekuambia wanaokutuma watakukana swala hili likifikishwa mahakamani. Acha kutumika na umwombe radhi Lowasa asije anza na wewe. Najua huna ubavu wa kudhibitisha uliyoyaandika humu popote kwani huna ushahidi zaidi ya porojo za kijiweni lumumba. Waambie na wenzako ninaisubiri ile sheria ianze kazi niwafunze adabu mahakamani kwa heshima ya Lowasa na kwa gharama zangu.

muulize mtikila yeye amepimaaaaa? asitake sifa....hii agenda sio laini anavyohisi
 
Mbona kasema sita lkn lowassa ndo anatajwa sana na kuwekewa makosa kibao??? KWELI ccm wana hali mbaya
 
Eating season kwa Mtikila na wenzie

Lile jiwe la Tarime lilimuathiri sana hata hivyo anaelewa kinachoweza kufanywa na ccm kama asipowatetea. Huyu ni njaa kama za kina Polepole,Mkinga na wenzao. Huo ufisadi wa Lowassa usioonekana hata kwenye hesabu za mkaguzi mkuu wa serikali na hasara aliyolisababishia taifa ni upi.Wote wanaoshupaza shingo zao kwenye suala la richmond mbona hawajawahi kutamka kiasi kama tunavyojua cha escrow na ,meremeta,majengo pacha ya b.o.t,misamaha ya kodi n.k.Lowassa alijiuzulu kisiasa kama alivyotakiwa na tume ya Mwakyembe kuwa apime mwenyewe kubakia na wadhifa wake au kujiuzulu. Baada ya kutafakari aliona kuna kitu zaidi kinachotafutwa na pengine ni nafasi yake. Aliona hivyo baada ya kuona takukuru ilishaagizwa na bunge kuchunguza kashfa ya richmond na ikaleta majibu kule kule bungeni kuwa haipo hasara yoyote serikali iliyopata. Bado Samwel Sitta akaunda tume nyingine ya wabunge ikiongozwa na dr. Mwakyembe. Hii nayo haikuona upotevu wa hela ya serikali ila iliona nia ovu ya kuingiwa mkataba ule na kampuni isiyo na uwezo wala ofisi. Katika uchunguzi wake waliwahoji wengi na walienda hadi nje ya nchi ila hawakumhoji waziri mkuu kabisa ingawa kwa kipindi chote alikuwepo nchini tena ofisini.Sasa hata ungekuwa wewe ungeamua tofauti na alivyoamua Lowassa? Hivi kweli ungekuwepo ufisadi wa hela kwa miaka yote minane asingekuwa amepelekwa mahakamani? Kina Mramba na mwenzie si walishtakiwa mahakamani kwa kuwa ulikuwepo ushahidi? Waliokwapua escrow hawapo waliopelekwa mahakamani? Acheni kulishwa maneno kama kasuku. Watanzania wa leo wameshaerevuka hata kama mtawapelekea siasa za maji taka za kuchafuana watawakatalia.Tunasema mfumo wa uongozi ccm ni m-baya kwa kuwakumbatia wezi na mafisadi hadi kuogopa eti wakiwapeleka mahakamani nchi itatetereka.Mwizi anaambiwa lipa polepole ulicholiibia taifa hatutakupeleka mahakamani. Sawa Lowassa kajiunga chadema na atagombea uraisi kwa tiketi ya chadema.Chadema mwenyekiti na raisi ni watu wawili tofauti na ccm ni mtu mmoja.Raisi wa chadema atapewa miongozo ya kuendesha serikali na chama kikiongozwa na m/kiti.Atafuata sera za chadema na ukawa wasiotaka rushwa,ufisadi wa mali na rasilimali za taifa n.k. Hivyo raisi hawezi kuongoza kwa utashi wake,mkewe au marafiki zake. Kama walivyokuwa wanajinasibu mikataba yote mikubwa baina ya nchi na mataifa mengine, mikataba yenye kuhusisha fedha nyingi za taifa kama ya mabarabara hata kama ni kwa wakandarasi wa ndani lazima mikataba hiyo iletwe bungeni kupitishwa. Na mengine mengi.
 
Mtikila mwenye afya amekufa, Lowassa "mgonjwa" (maneno ya Mtikila) bado anadunda na baada ya tarehe 25/10 ataapishwa kuwa rais wa JMT, sijui Mtikila atakuwa katika hali gani.
 
KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU TUSIRUHUSU MAFISADI WALICHEZEE TAIFA Edward Lowassa ni balaa kwa Taifa! Democratic Party (DP) inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha CCM pamoja na wanachama wake sita, Edward Lowassa na wengine, kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza kampeni ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.

1 Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowassa na wenzake walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya wakati, na kwamba chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowassa ameanza kampeni ya urais Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu na kumwaga rushwa ya kutisha!

2 Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake, katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na Pemba, wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowassa amefanya mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi katika kila mkutano wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa kura zao awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.

3 Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha fedha kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi, kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini, upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu sana ya kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa nchini na fisadi Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani, kumehusika ‘’Money laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo yote ni halali, na kama mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa ajili ya Taifa. Ni marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa kugombea urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa nchi yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Utawala wa Sheria

4
Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia kifisadi Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya mmwagiko wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza nchi nzima makundi ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano makali ya mara kwa mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu Lowasa ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa asilimia 95 ya wananchi! Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea kiasi cha kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya “Kilimo kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!

5
Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na kujipatia maeneo makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa mashangingi ya Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.

6
Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli wote aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu mengi na kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua mvua Thailand” na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi.

Ni mlemavu wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa, anayeweza kumruhusu fisadi Edward Lowassa agombee urais. Sifa za mtu wa kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati 17:15-20, ambazo Edward Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa awali alikemewa na Mwalimu Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama “Baba” yao, kuwa hafai kabisa kuwania urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, kama alivyomtangaza hata Reginald Mengi pale alipolazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond, lakini leo akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!

Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.

Katika uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake wa Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi kama China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa kupigwa risasi hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!

7.
Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais! Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima mwombaji awe na afya iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila mwombaji itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha kwamba hana dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:

a. Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu kwa kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.

b. Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo vingine vya mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa utendaji wa akili zake.

c.
Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia shughuli zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote yanayowatokea wananchi wote kila walipo, na kusimamia utekelezaji wa majukumu yote ya watendaji wote katika Taifa, hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na afya bora yenye kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote

d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na udhaifu huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo kiongozi mdhaifu. Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai kabla hajaweka sawa mambo yake na ya familia na jamii yake atatumikia maslahi yake zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya likawa limelikosesha Taifa kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!

e. Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini sana afya zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje ya nchi, kukosekana na umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya dhamana kubwa aliyopewa n.k. Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa macho tu, kabla ya uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya afya bora, ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewa dhamana kubwa sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais kwenyewe anatafuta kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha udhaifu katika kufanya maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbaya anagombea asichokiweza kabisa.

Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani wachunguzwe kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli tunalithamini na kuliheshimu Taifa. Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya maadili ya kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA.

Ni dhana potofu sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa watu! Kwa sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili umati wa kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’. LOWASA NI MOJAWAPO WA WAGONJWA WA MAGONJWA SUGU WA;IOKUWA WANATIBIWA NA BABU WA LOLIONDO NA TANGIA PALE HAJAPONA NA ZAIDI SANA ANAANZA KUTETEMEKA

Source: Mtikila Mwenyewe :0766 053081 View attachment 266356
Umetuachia ujumbe mzuri sana mzee wetu,RIP.
 
USHAHD ZAID ATAUTOA KWA MWENYE DUNIA YAKE ila asisahau kutubu kuhusu kumhukum mtu kwa afya yake na kwa hlo sijui atamwambia nn mungu, akjua kabxa mungu hadhihakiw kaz kwel kwel sawa rip
 
Kama hali ndiyo hii basi tuache kuwaita mafisadi watu ambao hawajapelekwa mahakamani hata kama ni ccm.
 
Yaani asipodakwa kwa gharama za uchaguzi atadakwa tu kwa kuanza kampeni mapema. Ushahidi ni CCM wenyewe.

Huyu CCM wakimpitisha tu basi UKAWA wanaibuka na ushindi wa mezani kwa kumuwekea pingamizi, anawekwa benchi na NEC kisha uchaguzi unakua kukamilisha formality tu.
ulitabiri vyema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom