Waraka maalum kwenda kwa waziri wa mambo ya ndani kuelezea ukabila uliokithiri idara ya uhamiaji

Wadau hivi ni kwanini wachaga kila mahali wawe wanalalamikiwa, yani mpaka uhamiaji naona huu ni uzushi sababu hawa watu uwepo wao ni kutokana na elimu walizonazo.

Mkuu una uhakika unayozungumza!! Kwani makabila mengine hawana elimu?
 
Huu ni uzushi tu...hi mijamaa ya kichaga bwana inasoma we nenda vyuoni tu humo alafu angalia wachaga jinsi walivyowengi wanapiga shule balaa tofauti na makabila mengine nenda mashuleni humo na vyuoni tafuta mluguru,mdigo,mnyamwezi,mzaramo,------ na mengineyo kama utapata hata kumi ila wachaga tu ni wengi..pia kwenye kutafuta jamaa wanajua bwana we nenda kijiji huko mkoa mwingine kabisa kama hutakuta mangi anauza duka au anachoma mbuzi....tuache ulalamishi sa nyingine tupige kazi bwana na tuhamasishe na sisi ndugu zetu wasome waje wapambane..
 
Bado na TRA nayo imejaza wachagga

Waende Chuo Kikuu chochote! Wachukue orodha ya Majaji kabla ya utawala wa JK wa kuteua majaji! Wakishamaliza huko waende tena mitaani, waangalie mafundi saa, simu, wapiga rangi viatu, fudni cherehani, halafu mafundi waashi, halafu waende ofisi za uchoraji nyumba.....halafu wakaangalie mapadre wangapi wachagga Dar halafu Zanzibar, halafu Mtwara....wakishatoka huko waende shule za vijijini kule Nachingwea waone walimu wachagga ni wangapi....mbona mwajitesa! Mchagga ni nani? Aliyesomea Uchagani? Aliyezaliwa Uzaramoni? Aliyeolewa Usukumani? aliyekulia Dar? Uchaga ni nini? Acha ukabila utakutafuna!

Oh nilisahau na masheik kule Arusha, hapa Dar na kule Dodoma!
 
Uongozi dhaifu, mambo huenda mrama. Rai imetolewa wahusika wachukue hatua. Waite agency iwachape usaili watakaoonekana bomu waondolewe mara moja. Wachaga chapeni kazi survival for the fittest hata kama ni kwa mlango wa nyuma tuliifungua hiyo milango wenyewe! Ifungeni lakini hawa jamaa watapitia ya mbele bila wasiwasi. Big up Wachaga.
 
alioandika ho waraka ana chuki tu...angalia idadi ya wanaomaliza vyuo ,shule kama ungeweka ukabila na maksi zao ungejua angalia wanaosoma shule nzuri zenye viwango utajua.....angalia watu waliopo kwenye idara hizo wengi ni wapi.............sasa kama uhamiaji wengi ni wachaga unategemea viongozi watoke wapi ?waliosoma zaidi shule wachaga unafikiri hizo kazi wamuajiri nani,,,,,acheeni ujinga someni...wachaga wan bidii katika kila jambo wafanyalo wanaojaribu kuiga nao pia hufanikiwa......hata biashara za bar nyingi hoteli nyingi ni wachaga...teh teh.....mmekalia ushirikina tu.....
 
wadauuu...
KWA MTAZAMO WANGU...
Ngoja tuweke sawa kitu, mnadhan ni UCHAGA TUU...
Labda mngesema ni UNDUGU WA KICHAGA, kwa sababu wachaga kibao walishaomba kazi hapo wakakosa, ila kama kuna mtu mnafahamiana na ni ndugu yako ndio unanafas ya kuajiriwa pale...
Na ili linawezwa fanywa na kabila lolote tz.
Sio vizuri ukaweka wachaga wote kama waraka ulivyo.
Pili ni vyema wa Tz tukawa na umoja na kujaliana bila kuangalia makabila yetu, leo ile kasumba ya kuoana kimakabila inapotea na inaweza fika kipindi tukuwa tunajua lugha nyingi kw sababu ya muunganiko huu.
Pia ni vyema watu waka wanajitaidi kuwapa watoto wao elimu hasa wa KIKE, leo hii tunasema wachaga,wahaya,wanyakyusa,wasukuma,wabena,wakinga wanajitaidi saaana kwenye elimu,ni ngumu kidogo kwa msomi kunyenga mahusiano/kuona na mtu asiye na elimu.Kw hiyo kama kutakuwa na muinuko na ushindan wa elimu ni vyema itapelekea kunyenga usawa ktkt maisha.
SHUKRANI.
 

Mkuu huo ndo ukweli tuache kuwalaumu wachaga hawa jamaa wanajituma sana na wanajua sana kupambana na maisha!
 
someni na fanyeni kazi kwa bidii, hata wakiondolewa wote leo watarudishwa tena tu kwani ni wachapa kazi. Ingia mtaa wowote wa nchi hii hautakosa duka la mangi, je? na huko ni nani aliwapendelea?

MImi ni Mchaga na sijipendelei
hata kama Mchaga hajasoma lakini anajituma na kupambana na kwa taarifa tu ni kwamba tunathubutu kufanya mambo ambayo wengi hawawezi
kuna wachaga wanasafiri kwenda china na taiwan kuchukuwa mizigo na jamaa hawajui kiingereza wala hawajasoma
nafikiri imefika wakati watanzania wakubali kwamba wachaga wanachangia sana kwenye kubadilisha uchumi wa taifa letu
wote tungekuwa kama wakwere kukaa vibarazani kutwa kucheza bao tungefika??kaa chini tafakari
 

Na tuombe mungu mchagga asipate u rais.Mbona mtatumaliza
 
asilimia kubwa ya wachaga ni wakristo na hapa nchini kuna malalamiko ya kuhusu wakristo kutawala serkali...sasa hapa inabidi mfikirie kwa umakini je huo ni udini au ukabila...kutoka mfumo kristo to chagalism mbona kazi hipo tanzania...
 
jaribu kufanya utafiti, nenda chuo chochote kusanya watu kumi, trust me 6 wanatoka kilimanjato, unategemea nini

si sita tu. Yawezekana nane kabisa. Hawa jamaa wanasoma shule na kuitafuta popote pale. Ukiingia kwenye vyuo vya diploma wamejaa kuanzia kwao mpaka tandala makete huko wakati mhehe wa iringa ukimwambia aende tandala anakataa na kusema kijijini haendi.
 
Ukiona hivyo ujue mwakyembe au magufuli ndo anaweza kuondoa uchafu huo
 
Ndugu yangu, mimi nipo kwenye kampuni moja binafsi. Managers wote Watano including HR sio wachaga...ila wafanyakazi 8 kati ya 23 ni wachaga. Sijui hapo utasemaje..Na kila mmoja amekuja kivyake.

Ukienda kwenye mabenki ndio utashangaa. Darasa nililokuwa nasoma chuoni karibu nusu ya darasa walikuwa wachaga. Nashauri hili swala tuanze kulitazama kwa jicho la tatu. La sivyo tutaendelea kuwa watu wa kulalamika tuuu.
 
Nimeshangaa kumbe yule Kamishna wao HAJAAPISHWA hadi leo! Ni kumtega ili awekwe mchagga? Ila mwandishi alipaswa asimumunye maneno, aseme yupi kawekwa wapi na hasitahili, aliyestahili ni fulani kwa vigezo a, b, c na sio ilivo sasa. Hata kama ni ukweli ni rahisi mno kuamini kuwa kilichoandikwa ni matokeo ya 'wivu wa kike' [ashakum si matusi]
 



aliyeandika huu waraka ni shemeji yangu mmoja wa kanda ya ziwa, ninamfahamu vizuri, kwa bahati mbaya amefanya kazi uhamiaji muda mrefu hata kwao hajawahi kujenga hata nyumba ya kufikia, ndugu na wazazi wake wanateseka yeye anajenga chuki na wachaga!!!! tukimaliza kwa wachaga tutakuta si wachaga tu, kuna wahaya, wanyakyusa na wagogo, tukimaliza hawa tutaanza kuwajengea wabena kama ilivyokuwa tuhuma za Luhanjo, naona tumehama kwenye ukanda kuwa chadema ni chama cha kikanda tunaenda kwenye udini!!! Hamfany kazi ni majungu tu na kukaa vijiweni, tumewajua tutawashughulikia sawasawa, anayetaka kupata cheo ajitahidi awe na elimu na uzoefu mzuri uliotukuka na si kwa propaganda hizi za kipumbavu!!! lkn shemeji tumeshakujua na tutakushughulikia uende zako usukumani ukachunge ngo'ombe
 
Kama waziri husika hatafanyia kazi tuhuma hizi yeye si waziri wa kudumu katika wizara hii atakuja waziri mwingine TYPE ya MAGUFURI atafanyia kazi tuhuma hizi na yeye atabakia kuwa historia ya kushindwa kutatua matatizo ya wananchi.
 
Hili si jambo la kupuuzwa. Kuna kitu muhimu cha kufuatiliwa. haiwezekani kabila moja liwe na watu 70 katika Idara moja-tena makao makuu pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…