Wajumbe Kamati Kuu,
Kwa heshima kubwa nawaandikia waraka huu mfupi kuhusu jambo moja ambalo ni la msingi kabisa na ambalo wanachama wa kawaida kabisa wangependa ufafanuzi mapema iwezekanavyo. Nimeona nitumie njia hii ya kupitia mtandao wa Kijamii wa JF nikiamini ndiyo njia bora zaidi kwa sasa na wajumbe wote wa kamati kuu kwa namna moja au nyingine ni watumiaji wa mtandao huu maarufu wa JF.
Kwanza niwapongeze wajumbe wote wa Kamati Kuu na wanachama wote kwa ujumla kwa juhudi kubwa mnazofanya kwa pamoja kupitia Vuguvugu la Mabadiliko-M4C ambalo kwa kiasi kikubwa limewekiweka chama chetu katika nafasi nzuri sana hasa katika maeneo ambako vuguvugu hili limepita.
Ni takribani miezi mitatu sasa tangu kuanza kwa mjadala mpana hasa kupitia vyombo vya habari,mitandao ya kijamii na mijadala ya kawaida mitaani kuhusu UGOMBEA WA URAIS NDANI YA CHADEMA.
Ikumbukwe kwamba mpaka sasa wanachama WATATU wa CHADEMA wameshatangaza Rasmi nia zao za kugombea URAIS wa Tanzania kupitia CHADEMA mwaka 2015.Wanachama ambao wameshatangaza nia zao ni Mhe. John Magale Shibuda (Mbunge wa Maswa), Deogratius Kisandu(Katibu wa BAVICHA-Tanga) na Mhe. Zitto Zubeir Kabwe(Naibu Katibu Mkuu Bara- CHADEMA)
Ni ukweli ulio dhahiri kuwa wanachama hawa watatu waliotangaza rasmi nia zao hawajavunja Katiba wala kanuni yoyote ya chama lakini pia ni wazi kutangaza kwao kumesababisha sintofahamu kubwa ndani ya chama.
Athari kubwa zinazoonekana za wazi mpaka sasa ni:
* Kabla ya wanachama hawa kutangaza nia zao mijadala mbalimbali katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ilitawaliwa zaidi na Harakati za chama katika kujiimarisha kupitia Vuguvugu la M4C lakini sasa mijadala hiyo imehamia kujadili URAIS ndani ya CHADEMA kitu ambacho ni furaha kuu kwa maadui wa CHADEMA.
* Makundi ndani ya Chama - Ifahamike kwamba CHADEMA inapaswa kuepuka kwa kila hali makundi ya aina yoyote ili kujitofautisha na vyama vingine vyenye makundi na yanayohatarisha uhai wa vyama hivyo. Tutakuwa tunajidanganya sana tukidhani kwamba hakuna watu wanaowaunga mkono wanachama hawa watatu ambao kwa lugha rahisi watakuwa tayari wanaunda mtandao wa watu watakaowapigania ndani ya chama ili majina yao yapitishwe na vikao wakati ukifika. Tufahamu kwamba hata kama watakuwa wanaungwa mkono na watu watano watano kila mmoja wao basi tayari hayo ni makundi na tayari hiyo ni mitandao. Tufahamu kwamba takriban bado miaka mitatu kufikia uchaguzi mkuu ujao!!
* Nilikuwa katika safari zangu za kibiashara huko Kishapu na nilishangaa kukuta wanachama wa kawaida kabisa wanaokaa vijiweni wakilalamikia hatari inayonyemelea chama chao kwa kile walichodai ni malumbano ya kusaka madaraka.Wakawa na hofu kwamba chama chao kitaishia kama NCCR ya wakati huo.Nilishtuka na sikuamini kusikia hayo kutoka kwa wanachama wadogo kabisa wa kule Kishapu.
Nimalizie waraka wangu huu kuiomba Kamati Kuu ya CHADEMA pindi itakapokutana ijadiliane hili swala kwa uhuru kabisa na kujaribu kutizama athari zilizoko mbele ya chama endapo kama hali hii itaachwa iendelee ingawa hakuna kanuni wala katiba iliyovunjwa.
Kamati Kuu ijiulize swali:
Je, Viongozi kama kumi kila mmoja akitangaza nia hiyo miaka 3 kabla ya uchaguzi mkuu umoja wa chama kweli utalindwa? Je, kunaweza kuwa na watangaza nia kumi kwa mfano halafu wasiunde mitandao ya kuwaunga mkono ili wapitishwe na vikao vya juu?
Si kazi yangu kutoa majibu ya maswali haya bali kwa niaba ya wanachama wengi na wapenzi wa CHADEMA tunaomba Kamati Kuu ije na majibu ya maswali haya na mwongozo kwa ujumla kuelekea 2015.
Naomba kuwasilisha.
Molemo.