Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 46,892
- 32,308
Waraka wangu nimeuelekeza Kamati kuu ya CDM.Wewe mwana CCM hauhusiki.Samahani sana.
Kwa nini usingeufunga kwenye bahasha ukaupeleka makao makuu ya Chadema pale Kinondoni Manyanya mtaa wa Ufipa.

how old are you???
Huyo Mufti anaendesha taasisi ipi na ilianzishwa na nani? huyo lazima umuone msema kweli taasisi yake ikiishiwa inasaidiwa bajeti na kanisa katoliki au hulijui hilo?
Analysis ya Molemo ni nzuri na ya haki lakini binafsi naamini kunyamaza na kuwaacha wanachama hawa waamuliwe na nguvu ya umma ndiyo njia bora kwa sasa ku-pre empty hii move iliyopangwa na CCM kupitia washauri wao Usalama wa Taifa (TISS). Molemo, unapomsikia mtu mwenye wadhifa mkubwa kama Wassira akisimama hadharani na kubwabwaja juu ya "kusambaratika" kwa CDM kabla ya uchaguzi mkuu usidhani ni jambo jepesi au la kupuuzwa. Ujue kuna jambo lililopangwa kisawa sawa na wanategemea litaenda kadiri ya mipango yao. Kwa muda mrefu sasa CCM imekuwa ikizitumia asasi zinazogharimiwa na kodi kwa manufaa ya chama chao na baadhi ya asasi zinazotumika ni Polisi, Usalama wa Taifa na hata Mahakama. Hali hii ambayo inaeleweka vema na viongozi karibu wa ngazi zote ndiyo inayokifanya chama kutenda kwa tahadhari kubwa katika kuyashughulikia matatizo ya ndani ya chama ambayo kwa hakika mengi ni ya kupandikizwa na maadui wa chama kwa kutumia watu walio ndani ya chama wanaotumika wakiwa wanajua au bila kujua.
CHDEMA chama kilichokomazwa na mikasa na majaribu ya miaka mingi na sasa ni mali ya wananchi bila kujali jiografia, imani au hali na mwitikio wa wananchi kwa harakati za chama hiki ndiyo unaosababisha kiwewe toka CCM na vibaraka wao. Naamini kwa kufanya hivi CCM wataaibika.
Kwa nini usingeufunga kwenye bahasha ukaupeleka makao makuu ya Chadema pale Kinondoni Manyanya mtaa wa Ufipa.
Nani kakuambia malemo yuko umbali wa kuweza kuupeleka kinondoni
Sio kila jambo kama huna hoja unachangia unaweza hata kwenda kuosha viombo vikawa visafi
"Jambo usilolijua ni kama usiku wakiza"Nakushukuru mkuu kwa majibu mazuri kwa huyu kilaza.
Thanks MANI
Lengo hapa ni kujenga na si kubomoa.
Ikumbukwe kwamba mpaka sasa wanachama WATATU wa CHADEMA wameshatangaza Rasmi nia zao za kugombea URAIS wa Tanzania kupitia CHADEMA mwaka 2015.Wanachama ambao wameshatangaza nia zao ni Mhe. John Magale Shibuda (Mbunge wa Maswa), Deogratius Kisandu(Katibu wa BAVICHA-Tanga) na Mhe. Zitto Zubeir Kabwe(Naibu Katibu Mkuu Bara- CHADEMA)
Wajumbe Kamati Kuu,
Kwa heshima kubwa nawaandikia waraka huu mfupi kuhusu jambo moja ambalo ni la msingi kabisa na ambalo wanachama wa kawaida kabisa wangependa ufafanuzi mapema iwezekanavyo. Nimeona nitumie njia hii ya kupitia mtandao wa Kijamii wa JF nikiamini ndiyo njia bora zaidi kwa sasa na wajumbe wote wa kamati kuu kwa namna moja au nyingine ni watumiaji wa mtandao huu maarufu wa JF.
Kwanza niwapongeze wajumbe wote wa Kamati Kuu na wanachama wote kwa ujumla kwa juhudi kubwa mnazofanya kwa pamoja kupitia Vuguvugu la Mabadiliko-M4C ambalo kwa kiasi kikubwa limewekiweka chama chetu katika nafasi nzuri sana hasa katika maeneo ambako vuguvugu hili limepita.
Ni takribani miezi mitatu sasa tangu kuanza kwa mjadala mpana hasa kupitia vyombo vya habari,mitandao ya kijamii na mijadala ya kawaida mitaani kuhusu UGOMBEA WA URAIS NDANI YA CHADEMA.

Ni ukweli ulio dhahiri kuwa wanachama hawa watatu waliotangaza rasmi nia zao hawajavunja Katiba wala kanuni yoyote ya chama lakini pia ni wazi kutangaza kwao kumesababisha sintofahamu kubwa ndani ya chama.
Athari kubwa zinazoonekana za wazi mpaka sasa ni:
* Kabla ya wanachama hawa kutangaza nia zao mijadala mbalimbali katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ilitawaliwa zaidi na Harakati za chama katika kujiimarisha kupitia Vuguvugu la M4C lakini sasa mijadala hiyo imehamia kujadili URAIS ndani ya CHADEMA kitu ambacho ni furaha kuu kwa maadui wa CHADEMA.
* Makundi ndani ya Chama - Ifahamike kwamba CHADEMA inapaswa kuepuka kwa kila hali makundi ya aina yoyote ili kujitofautisha na vyama vingine vyenye makundi na yanayohatarisha uhai wa vyama hivyo. Tutakuwa tunajidanganya sana tukidhani kwamba hakuna watu wanaowaunga mkono wanachama hawa watatu ambao kwa lugha rahisi watakuwa tayari wanaunda mtandao wa watu watakaowapigania ndani ya chama ili majina yao yapitishwe na vikao wakati ukifika. Tufahamu kwamba hata kama watakuwa wanaungwa mkono na watu watano watano kila mmoja wao basi tayari hayo ni makundi na tayari hiyo ni mitandao. Tufahamu kwamba takriban bado miaka mitatu kufikia uchaguzi mkuu ujao!!
* Nilikuwa katika safari zangu za kibiashara huko Kishapu na nilishangaa kukuta wanachama wa kawaida kabisa wanaokaa vijiweni wakilalamikia hatari inayonyemelea chama chao kwa kile walichodai ni malumbano ya kusaka madaraka.Wakawa na hofu kwamba chama chao kitaishia kama NCCR ya wakati huo.Nilishtuka na sikuamini kusikia hayo kutoka kwa wanachama wadogo kabisa wa kule Kishapu.
Nimalizie waraka wangu huu kuiomba Kamati Kuu ya CHADEMA pindi itakapokutana ijadiliane hili swala kwa uhuru kabisa na kujaribu kutizama athari zilizoko mbele ya chama endapo kama hali hii itaachwa iendelee ingawa hakuna kanuni wala katiba iliyovunjwa.
Kamati Kuu ijiulize swali:
Je, Viongozi kama kumi kila mmoja akitangaza nia hiyo miaka 3 kabla ya uchaguzi mkuu umoja wa chama kweli utalindwa? Je, kunaweza kuwa na watangaza nia kumi kwa mfano halafu wasiunde mitandao ya kuwaunga mkono ili wapitishwe na vikao vya juu?
Si kazi yangu kutoa majibu ya maswali haya bali kwa niaba ya wanachama wengi na wapenzi wa CHADEMA tunaomba Kamati Kuu ije na majibu ya maswali haya na mwongozo kwa ujumla kuelekea 2015.
Naomba kuwasilisha.
Molemo.
"Jambo usilolijua ni kama usiku wakiza"
Kwa mbali naona mpango wa EL ukikamilika.Kwani mwaka 2015, Zitto ataleta utengano ndani ya CDM kisha kura zipungue na EL alambe urais.
Kamati kuu inabidi iwe makini sana na huyu kijana anayetumiwa.aliwahi kutumiwa pia kutushawishi watz tununue ile mitambo ya Richmond iliyotokana na Deals feki.
Hili jambo si la kulichukulia kirahisi,kuna uwezekano mkubwa sana Umri wa kugombea uraisi ukapunguzwa,kwani Hainiingii akilini mtu ambaye sidhani kama atakua 40's by then ,aanze kutangaza nia sasa.Huu mpango umeratibiwa muda mrefu sana.Kwani Zitto alitangaza kugombea Uraisi kule kigoma akiwa kwenye Kampeni za Ubunge.Tangu enzi hizo niliisha ona matatizo aliyokuwa akiyatengeneza.
Lkini Mwisho wa Ubaya ni Aibu,na sikuzote uongo na unafiki haviwezi kuushinda Ukweli