Mgogoro wa wanafunzi UDOM na ule wa wahadhiri wao unabeba sura ya kisiasa tena siasa za kuangamiza taifa letu, Nasema haya nikisikitika kwa kinachoendelea katika uwanja wa siasa leo,
Hawa wanafunzi waliofukuzwa UDOM walichaguliwa baada ya kufaulu vizuri(alama A na B) masomo ya sayansi kidato cha nne kutokana agizo la serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete la kuitaka wizara ifanye njia za makusudi kupunguza tatizo la walimu wa sayansi katika shule za sekondari kidato cha 1-4.
Ilianzishwa mpango maalumu (Diploma Special Program) iliyozinduliwa na Rais kwa pesa zilizoombwa bungeni kisheria (bunge liliridhia) kuwasomesha vijana hao kwa gharama za serikali ili wakafundishe O-level katika shule za serikali kisha baadaye wakasome degree. Kazi ya kuwadahili vijana hawa ilifanywa na serikali yenyewe kupitia TCU.
Leo serikali ya chama kilekile na bunge lake lilelile wamekuja na waziri wa chama kilekile wanashindwa kuwalipa malipo wakufunzi wa wanafunzi hao na kupelekea mgomo wa wahariri, hawaishi hapo wanakwenda chuoni na kuwafukuza wanafunzi hao wasio na hatia, wanataka dunia iamini kuwa serikali iliyopita ni nyingine kabisa na haina mazuri iliyoyafanya na ilikua inaongozwa wajinga! Katika bunge lilelile na spika wa chama kilekile wanazuia hoja binafsi ya Mbunge wa upinzani anayetaka bunge lijadili mgogoro huu na kunusuru hatari inayowakumba watoto wetu hapo UDOM, na zaidi mbunge huyo ananyanyuliwa mzobemzobe na polisi na kutupwa nje ya lango la Bunge
Leo ni vijana hao hao kama wangeamua kwenda kidato cha tano wangemaliza form six mwaka jana lakini walijitolea na pamoja na kufaulu kwa division one na two zao kusaidia taifa. Leo wanafukuzwa kwa mabomu na mbwa wa polisi.
Unapowaondoa wanafunzi 7,802 ndani ya saa 24 sijui hii serikali ya CCM inawaza nini....
Ili waondoke wote hapo yanahitajika mabasi zaidi ya 150 ambayo ni karibu nusu ya mabasi yote yanayoondoka Ubungo kwa siku 1 kwenda nchi nzima, Haujafikiria watalala wapi...watakula wapi...
Na: Yericko Nyerere