Wapinzani wajitathimini kwa chaguzi zijazo kama wana nia ya kushika dola

Monasha

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
561
422
Mwaka wa 2020 unaenda tena kuwa mwaka mwingine wa kihistoria kwa nchi yetu. Ni mwaka ambao tunasubiri maamuzi ya Watanzania ambapo kilele chake itakuwa tar 28 October 2020.

Tunaona chama tawala na vyama vya upinzani vikijinadi kwa mengi majukwaani mbele ya waamuzi wao ambao ni wananchi. Kila chama ikijitahidi kushawishi kwa hili na lile. Ni kipindi ambapo sasa vyama vingi vinajulikana vikiwemo ambavyo siyo maarufu masikioni mwa watu wengi.

Ni vizuri kuwa na upinzani, kwani huimairisha demokrasia lakini pia ni chachu kubwa sana ya maendeleo katika nchi. Lakini kwa nchi yetu hii kwa kweli suala la upinzani bado sana. Miongoni mwa wapinzani bado kuna watu ambao wana maslahi binafsi. Hili ni gumu sana kwa wapinzani kutoboa. Kama kweli Vyama vya upinzani vina nia ya kuiangusha CCM na kuchukua dola kwa maslahi ya Watanzania, basi ni lazima wajiangalie sana kwa kufanya yafuatayo;

1. Watumie muda wao mwingi kukijenga chama. Hili limekuwa na ukakasi sana miongoni mwa vyama vya upinzani. Ni ukweli kwamba vyama vingine vya upinzani vinakuja kuonekana hata kwenye vyombo vya habari nyakati za uchaguzi tu. Baada ya uchaguzi vinaingia mtini. Hakuna kutafuta wanachama wapya, hakuna uongozi unaoeleweka kutoka ngazi za chini hadi za juu. Kama hawatachukua muda wao kuvijenga vyama basi hivi vyama vitajikuta kila nyakati za uchaguzi vikilalamika tu kuibiwa kura na uchaguzi kutokuwa huru na wa haki. Kufanya hivi watakuwa wanawekeza kwa wapiga kura kwa faida ya miaka ijayo.

2. Wakubali kuungana. Kama kweli siyo maslahi binafsi na kupata ruzuku tu, kuna vyama vinajua kabisa kwamba hawataambulia chochote hata nafasi za ubunge. Lakini kila ikifika uchaguzi mkuu utaviona majukwaani navyo vikijaribu kuokoteza na kueneza sera huku wakijua fika kabisa kwamba hawatabadilisha chochote. Laiti kama kweli wangekuwa wana nia ya kuleta upinzani dhabiti nchini basi wangeungana na kuwa chama kimoja chenye nguvu ili waweze kupambana na chama tawala.

3. Viongozi wa vyama wakubali kushindwa na kuachia uongozi. Madhalan pale kiongozi wa chama anapojikuta amegombea kwa miaka mingi bila hata kuleta mabadiliko ndani ya chama kwa kuongeza hata wanachama, ifike mahali wakubali kuachia ngazi na kutengeneza mtiririko mzuri wa kuachiana uongozi kama chama. Wakiendelea na huu mfumo wa kila mwaka fulani kugombea tena bila mafanikio, dhana ya vyama hivyo kuwa vya watu binafsi na vyenye lengo la kujifunufaisha haitaisha.

Chama hujengwa kuanzia chini mpaka juu. Vyama hivi vijiangalie kama kweli wana nia na watanzania wote, basi viache kulala mara tu uchaguzi unapoisha. Viamke vitembee huko vijijini kujiimarisha kwa kupata wanachama wapya mradi tu hawavunji taratibu za nchi. Bila kufanya hivi kila uchaguzi ukifika vitaishi tu kupokea ruzuku na baadae kurudi kujificha.

Ni ajabu sasahivi unaona mgombea wa chama anajinadi jukwaani ukiuliza ofisi katika mkoa wako haipo kabisa na hawajawahi hata kupatembelea eneo pengine unalokaa. Ni ngumu sana wao kupata ushindi kama hawatakubali kutumia muda wao mwingi kujenga hivi vyama.
 
Wewe rudisha wagombea wa upinzani mliowakata kwa hujuma - kama nyie ni chama dume kweli mbona mnaogopa sanduku la kura? acheni wananchi wenyewe waamue, mambo ya kuweka mpira kwapani ni mambo ya kilongi sana.
 
Uonevu kama huo wa kuwazua wapinzani sawa ni changamoto sana. Lakini bado nashauri wapinzani kujijenga sana. Haya ya kuonewa mara mara mtu anazuiliwa kugombea naamini yataisha tu. Kwa sasa nguvu ya wananchi ndo ngao kubwa na isipokusanywa itazidi kuwa rahisi kuonewa tuu.
 
Wagombea wanarudishwa vipi wakati hawana vigezo?
 
Uonevu kama huo wa kuwazua wapinzani sawa ni changamoto sana. Lakini bado nashauri wapinzani kujijenga sana. Haya ya kuonewa mara mara mtu anazuiliwa kugombea naamini yataisha tu. Kwa sasa nguvu ya wananchi ndo ngao kubwa na isipokusanywa itazidi kuwa rahisi kuonewa tuu.
Wewe ni mpenzi wa ccm kwa sababu ccm ipo madarakani siku ikiondoka na upenzi wako unakoma.
 
Mwaka wa 2020 unaenda tena kuwa mwaka mwingine wa kihistoria kwa nchi yetu. Ni mwaka ambao tunasubiri maamuzi ya Watanzania ambapo kilele chake itakuwa tar 28 October 2020.

Tunaona chama tawala na vyama vya upinzani vikijinadi kwa mengi majukwaani mbele ya waamuzi wao ambao ni wananchi. Kila chama ikijitahidi kushawishi kwa hili na lile. Ni kipindi ambapo sasa vyama vingi vinajulikana vikiwemo ambavyo siyo maarufu masikioni mwa watu wengi.

Ni vizuri kuwa na upinzani, kwani huimairisha demokrasia lakini pia ni chachu kubwa sana ya maendeleo katika nchi. Lakini kwa nchi yetu hii kwa kweli suala la upinzani bado sana. Miongoni mwa wapinzani bado kuna watu ambao wana maslahi binafsi. Hili ni gumu sana kwa wapinzani kutoboa. Kama kweli Vyama vya upinzani vina nia ya kuiangusha CCM na kuchukua dola kwa maslahi ya Watanzania, basi ni lazima wajiangalie sana kwa kufanya yafuatayo;

1. Watumie muda wao mwingi kukijenga chama. Hili limekuwa na ukakasi sana miongoni mwa vyama vya upinzani. Ni ukweli kwamba vyama vingine vya upinzani vinakuja kuonekana hata kwenye vyombo vya habari nyakati za uchaguzi tu. Baada ya uchaguzi vinaingia mtini. Hakuna kutafuta wanachama wapya, hakuna uongozi unaoeleweka kutoka ngazi za chini hadi za juu. Kama hawatachukua muda wao kuvijenga vyama basi hivi vyama vitajikuta kila nyakati za uchaguzi vikilalamika tu kuibiwa kura na uchaguzi kutokuwa huru na wa haki. Kufanya hivi watakuwa wanawekeza kwa wapiga kura kwa faida ya miaka ijayo.

2. Wakubali kuungana. Kama kweli siyo maslahi binafsi na kupata ruzuku tu, kuna vyama vinajua kabisa kwamba hawataambulia chochote hata nafasi za ubunge. Lakini kila ikifika uchaguzi mkuu utaviona majukwaani navyo vikijaribu kuokoteza na kueneza sera huku wakijua fika kabisa kwamba hawatabadilisha chochote. Laiti kama kweli wangekuwa wana nia ya kuleta upinzani dhabiti nchini basi wangeungana na kuwa chama kimoja chenye nguvu ili waweze kupambana na chama tawala.

3. Viongozi wa vyama wakubali kushindwa na kuachia uongozi. Madhalan pale kiongozi wa chama anapojikuta amegombea kwa miaka mingi bila hata kuleta mabadiliko ndani ya chama kwa kuongeza hata wanachama, ifike mahali wakubali kuachia ngazi na kutengeneza mtiririko mzuri wa kuachiana uongozi kama chama. Wakiendelea na huu mfumo wa kila mwaka fulani kugombea tena bila mafanikio, dhana ya vyama hivyo kuwa vya watu binafsi na vyenye lengo la kujifunufaisha haitaisha.

Chama hujengwa kuanzia chini mpaka juu. Vyama hivi vijiangalie kama kweli wana nia na watanzania wote, basi viache kulala mara tu uchaguzi unapoisha. Viamke vitembee huko vijijini kujiimarisha kwa kupata wanachama wapya mradi tu hawavunji taratibu za nchi. Bila kufanya hivi kila uchaguzi ukifika vitaishi tu kupokea ruzuku na baadae kurudi kujificha.

Ni ajabu sasahivi unaona mgombea wa chama anajinadi jukwaani ukiuliza ofisi katika mkoa wako haipo kabisa na hawajawahi hata kupatembelea eneo pengine unalokaa. Ni ngumu sana wao kupata ushindi kama hawatakubali kutumia muda wao mwingi kujenga hivi vyama.
Mkuu Monasha , asante sana kwa bandiko hili, japo sisi JF tuko members wengi humu, na miongoni mwetu kuna wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa vyama, lakini ni wachache sana wako objective kuvisaidia vyama vyao, bandiko lako hili ni very objective, lenye lengo la kuvisaidia vyama.

Baadhi ya haya uliozungumzia humu, nami niliwahi kuyazungumza.
Asante
Pp
 
Mwaka wa 2020 unaenda tena kuwa mwaka mwingine wa kihistoria kwa nchi yetu. Ni mwaka ambao tunasubiri maamuzi ya Watanzania ambapo kilele chake itakuwa tar 28 October 2020.

Tunaona chama tawala na vyama vya upinzani vikijinadi kwa mengi majukwaani mbele ya waamuzi wao ambao ni wananchi. Kila chama ikijitahidi kushawishi kwa hili na lile. Ni kipindi ambapo sasa vyama vingi vinajulikana vikiwemo ambavyo siyo maarufu masikioni mwa watu wengi.

Ni vizuri kuwa na upinzani, kwani huimairisha demokrasia lakini pia ni chachu kubwa sana ya maendeleo katika nchi. Lakini kwa nchi yetu hii kwa kweli suala la upinzani bado sana. Miongoni mwa wapinzani bado kuna watu ambao wana maslahi binafsi. Hili ni gumu sana kwa wapinzani kutoboa. Kama kweli Vyama vya upinzani vina nia ya kuiangusha CCM na kuchukua dola kwa maslahi ya Watanzania, basi ni lazima wajiangalie sana kwa kufanya yafuatayo;

1. Watumie muda wao mwingi kukijenga chama. Hili limekuwa na ukakasi sana miongoni mwa vyama vya upinzani. Ni ukweli kwamba vyama vingine vya upinzani vinakuja kuonekana hata kwenye vyombo vya habari nyakati za uchaguzi tu. Baada ya uchaguzi vinaingia mtini. Hakuna kutafuta wanachama wapya, hakuna uongozi unaoeleweka kutoka ngazi za chini hadi za juu. Kama hawatachukua muda wao kuvijenga vyama basi hivi vyama vitajikuta kila nyakati za uchaguzi vikilalamika tu kuibiwa kura na uchaguzi kutokuwa huru na wa haki. Kufanya hivi watakuwa wanawekeza kwa wapiga kura kwa faida ya miaka ijayo.

2. Wakubali kuungana. Kama kweli siyo maslahi binafsi na kupata ruzuku tu, kuna vyama vinajua kabisa kwamba hawataambulia chochote hata nafasi za ubunge. Lakini kila ikifika uchaguzi mkuu utaviona majukwaani navyo vikijaribu kuokoteza na kueneza sera huku wakijua fika kabisa kwamba hawatabadilisha chochote. Laiti kama kweli wangekuwa wana nia ya kuleta upinzani dhabiti nchini basi wangeungana na kuwa chama kimoja chenye nguvu ili waweze kupambana na chama tawala.

3. Viongozi wa vyama wakubali kushindwa na kuachia uongozi. Madhalan pale kiongozi wa chama anapojikuta amegombea kwa miaka mingi bila hata kuleta mabadiliko ndani ya chama kwa kuongeza hata wanachama, ifike mahali wakubali kuachia ngazi na kutengeneza mtiririko mzuri wa kuachiana uongozi kama chama. Wakiendelea na huu mfumo wa kila mwaka fulani kugombea tena bila mafanikio, dhana ya vyama hivyo kuwa vya watu binafsi na vyenye lengo la kujifunufaisha haitaisha.

Chama hujengwa kuanzia chini mpaka juu. Vyama hivi vijiangalie kama kweli wana nia na watanzania wote, basi viache kulala mara tu uchaguzi unapoisha. Viamke vitembee huko vijijini kujiimarisha kwa kupata wanachama wapya mradi tu hawavunji taratibu za nchi. Bila kufanya hivi kila uchaguzi ukifika vitaishi tu kupokea ruzuku na baadae kurudi kujificha.

Ni ajabu sasahivi unaona mgombea wa chama anajinadi jukwaani ukiuliza ofisi katika mkoa wako haipo kabisa na hawajawahi hata kupatembelea eneo pengine unalokaa. Ni ngumu sana wao kupata ushindi kama hawatakubali kutumia muda wao mwingi kujenga hivi vyama.
Tuko Iringa ,magufuli haionekani kakimbia kampeni?
 
Back
Top Bottom