Tunutu kiwavi
JF-Expert Member
- Jul 2, 2016
- 528
- 215
USHAIDI WA UFISADI WA LOWASA ANAO MNYIKA AU NA YEYE ALITUDANGANYA ?Hoja za kichovu hizi! Eti watanzania kwa ujumla wanahitaji maendeleo, basi! Hizi ndizo blah blah mlizolishwa na Sizonje za kutaka kupumbaza wajinga. Kuna uhusiano mkubwa wa maendeleo ya nchi na sera za chama kinachoongoza nchi kwa wakati husika. Ni mtu mjinga pekee atakayeendelea kung'ang'ana na Lowasa kwa hoja ya ufisadi ilihali mambo yote yaliishawekwa wazi kwamba hiyo ilikuwa ni vita ya madaraka ndani ya CCM. Kwanini usijiulize swali dogo tu. Hivi Lowasa ana kinga gani kiasi kwamba kama alihusika na huo ufisadi asifikishwe kortni tangu mwaka 2008? Tena kwa siasa hizi za chuki, leo Lowasa angekuwa uraiani? Na kama hoja ni ufisadi, hawa akina Chenge, Ngeleja, Karamagi; na the like ambao wamejazana CCM mnawazungumziaje? Hakuna mtu mwenye mawaa atakayeondoka CCM kwenda upinzani, hifadhi ya mafisadi iko CCM, kama una akili lakini!
Kwa nini ni Pointless?Andika maneno machache lakini yenye point. Hapo umeandika maneno mengi lakini pointless
KWELI KABISA HIKI KIZAZI CHA KINALOWASA KITAISHA TUKizazi chenu kilichounda TANU kitaisha tu. Na ndio utakua mwisho wa HUU UTAWALA WA KISHETANI
Kwani enzi Dr. Slaa akiwa CHADEMA nyie CCM mlikuwa mnaiunga mkono CHADEMA?Bila CHADEMA kumfukuza Lowassa na Sumaye na kisha kumuomba Msamaha Dr. Slaa Ikulu wataiona kwenye TV tuu.
Imezuka hoja hapa JF kwamba CCM kuendelea kwake kuwa madarakani ni kwa sababu Tanzania tuna vyama vya upinzani dhaifu. inawezekana hoja hiyo ina ukweli fulani ndani yake lakini lazima wanaouona upinzani ni dhaifu watoe maoni yao ni nini kifanyike ili CCM ing'oke madarakani Tanzania ikibaki salama.
Wengine hatuuoni uimara wa CCM bali tunaona mabavu ya CCM kutumia dola dhidi ya vyama vingine vya siasa. Leo hoja kubwa kwamba upinzani ni dhaifu ni madai kwamba wameiacha hoja "yao" ya ufisadi.
Lakini ni kweli kuwa Upinzani wameacha hoja yao ya kupiga vita ufisadi? Hivi kuna tofauti gani ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Lugumi kama ilivyokuwa kwa EPA ama Tegeta Escrow? Wakati ajenda ya wapinzani ilipokuwa kupiga vita ufisadi, CCM walifanya nini tofauti na sasa?
Lowassa aliitwa fisadi Pale Mwembe Yanga kwa kuvunja mkataba kati ya City waters na Dawasa, leo wapinzani wakizungumizia kuhusu Bombadier, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, matumizi nje ya bajeti,kukopa fedha kinyemela inaonekana hawazungumzii ufisadi, ni kwa nini?
Dah....kumbe nawe in mpinzani? Sikujua..... Unapinga nini hasa?[emoji13] [emoji87] [emoji41]Hatuwezi kuweka wazi mbinu zote za upinzani, kuna komba humu wanasubiri kunywa kosha
Mwambieni aruhusu mikutano ya kisiasa kama katiba na sheria inavyosema gogoro nnImezuka hoja hapa JF kwamba CCM kuendelea kwake kuwa madarakani ni kwa sababu Tanzania tuna vyama vya upinzani dhaifu. inawezekana hoja hiyo ina ukweli fulani ndani yake lakini lazima wanaouona upinzani ni dhaifu watoe maoni yao ni nini kifanyike ili CCM ing'oke madarakani Tanzania ikibaki salama.
Wengine hatuuoni uimara wa CCM bali tunaona mabavu ya CCM kutumia dola dhidi ya vyama vingine vya siasa. Leo hoja kubwa kwamba upinzani ni dhaifu ni madai kwamba wameiacha hoja "yao" ya ufisadi.
Lakini ni kweli kuwa Upinzani wameacha hoja yao ya kupiga vita ufisadi? Hivi kuna tofauti gani ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Lugumi kama ilivyokuwa kwa EPA ama Tegeta Escrow? Wakati ajenda ya wapinzani ilipokuwa kupiga vita ufisadi, CCM walifanya nini tofauti na sasa?
Lowassa aliitwa fisadi Pale Mwembe Yanga kwa kuvunja mkataba kati ya City waters na Dawasa, leo wapinzani wakizungumizia kuhusu Bombadier, ujenzi wa uwanja wa ndege Chato, matumizi nje ya bajeti,kukopa fedha kinyemela inaonekana hawazungumzii ufisadi, ni kwa nini?
Waberoya nashukuru kwa kutoa ushauri mzuri sana. Badala ya kurusha vijembe ni kheri kutoa mawazo hata kama tutatofautiana na mawazo hayo.
Nianze na la Lowassa. Mimi kwa mtazamo wangu kila siku ni kwamba Lowassa si tatizo bali tatizo ni CHADEMA. Kuna hoja aliitoa Dr. Slaa kwamba kabla ya kujiunga na CHADEMA ni lazima kwanza Lowassa atangaze hadharani kwamba yeye si mhusika na kashifa ya Richmond. CHADEMA wakapuuzia.
Haiwezekani mtu ambaye kila siku mlikuwa mnamwita majina mabaya ya kila aina ghafla tu bila ya maelezo mnapokea na kumfanya mgombea wenu bila hata ya kutoa maelezo ni nini kimewafanya kubadilika kwa kiasi hicho.
Ndiyo maana "marafiki" wa Dr. Slaa kina Mzee Mwanakijiji na idawa wanawananga kila siku CHADEMA kwa upuuzi huo walioufanya. Hawajajibu hoja kama walipokuwa wanasema wana "ushahidi" walikuwa wanamaanisha nini ama walikuwa wanatumia uongo kujipatia ufuasi tu?
Leo mtu anajiuliza ni kwa nini Msigwa, Lema, Mnyika na hata Mbowe ambao walikuwa wanawaaminisha watanzania kuwa Lowassa ni mtu "Mbaya sana", wanatakaje watanzania wamchague mtu mbaya kuwa Rais wao?
Sasa mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba Lowassa alihusika na ufisadi wowote ule kwenye Richmond, lakini itakuwa ngumu sana kuwaamini viongozi wa CHADEMA wanaposema kwamba Lowassa anafaa kuwa Rais. Viongozi wa CHADEMA hawana nguvu ya kimaadili (Moral Authority) kumnadi Lowassa bila ya kwanza kuwaeleza watanzania ni kwa nini walikuwa wanamsema ni mtu mbaya kiasi kile?
Kuhusu Sera na ujenzi wa chama nadhani kuna matatizo mawili makubwa. Kwanza ni wana CHADEMA kutaka kumlinganisha Vincent Mashinji na Slaa. Mungu kampa kila mtu kipawa chake kwa ivo haiwezekani tukafanana. Mashinji anapata wakati mgumu sana kuiunganisha hii CHADEMA "mpya".
Jambo la pili ni CHADEMA kushughulika na Lowassa wakiwa wamemakinika. Lowassa alijitengeneza kama taasisi na alipokwenda CHADEMA alikwenda kama taasisi. CHADEMA wanatakiwa kumlazimisha Lowassa asiwe taasisi ndani ya taasisi.
Kuingia kwa Lowassa kulileta taharuki na fadhaa kwa baadhi watendaji ndani ya CHADEMA ambao walikuwa wanaamini waliipigania chama kwa muda mrefu wakati huo Lowassa "anakula raha" CCM. Kuna watu CHADEMA wamepotezwa kabisa kwa ujio wa Lowassa.
Jambo moja la kufurahisha ni kwamba hata CCM wanaposema vyama vya upinzani humaanisha CHADEMA. je CHADEMA wenyewe wanaijua na kuikuza thamani yao?
Tanzania kuna chama kimoja tu cha siasa, siku tukipata chama kingine tutaona namna ya kubadilisha, mengine haya ni magenge ya wanaharakati yenye wafuasiSasa kwa nini hivi vyama vipo?
Acha uzwazwa, yaani ushahidi wa ufisadi wa Lowasa awe nao Mnyika lakini sio vyombo vya dola? Mwambieni Mnyika awape huo ushahidi mtimize nia yenu ya hovyo, chuki na kutenda kishamba!USHAIDI WA UFISADI WA LOWASA ANAO MNYIKA AU NA YEYE ALITUDANGANYA ?
Pengine unachosema ni kweli mkuu.Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ndiyo suluhisho la kudumu.