Wapinzani mnavuna mlichokipanda

Omuchimati

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
427
202
Assalam aleykhum wana JF,

Nimekaa na kutafakari nimetamani kunyamaza lakini nimeshindwa kujizuia kwa yale yanayotokea na kuendelea kwa jamii yangu pendwa ya Tanzania , nikiwa mtanzania halisi nilielelewa katika maandili ya kitanzania na kuitanguliza nchi yangu mbele kama mtanzania halisi mwenye dhamira safi ya kuilinda nchi yangu mpaka mauti yanikute

Nawapa pole sana familia ya Akwilina kwa msiba mkubwa uliowakuta kwa kuondokea na binti yao mpendwa. Akwiline kufuatia kifo chake kilichosababishwa na maandamano haramu ya chama kimojawapo cha Siasa kinachojinasibu kuwa ni chama cha harakati na chenye kuleta ukombozi nchini Tanzania, nawalaani kwa Nguvu zote walioleta haya maandamano, na ninawaalani tena nikiomba hatima yao iwe ni mwaka 2020, wakati wa uchaguzi.

Narejea kwenye ujumbe wangu mahsusi, wapinzani mlichokipanda ndicho mnachokivuna, wakati wa MHE Rais wetu mpendwa Jakaya Mrisho kikwete, mlimbeza , mkamtukana, ilifikia wakati hata Mhe John John Mnyika akatamka kuwa hajawahi kuona Rais dhaifu kama yeye, je mnajua madhila mliokuwa mnayasababisha kwake yeye na familia yake?

Hewala aliwavumilia hata ilifikia wakati aliwaita ikulu mkanywa , juice, pamoja na vitafunwa, achilia mbali pocket money mlizokuwa mnapewa baada ya kikao na Mhe Rais.

Mlipokuwa mnatukana, mnakebehi, mnaandamana hovyo, kuna watu walikuwa nje ya game wanwacheki tu wanasema wallah siku nikikamata hili rungu hawa jamaa watanitambua, rungu limepata mwenyewe leo mnanyooshwa mnalialia, mnatiwa ndani mnalialia, kumbukeni mbinu mlizotumia wakati ule ni hizi hizi mnazozitumia leo msitegemee kuitwa ikulu, mnywe juice,chai na baadae mpewe pocket money.

Ushauri wangu, hii nchi ni yetu sisi sote, kaeni chini mjiulize mmekosea wapi na mnapaswa kujirekebisha vip, social networks zilileta athari kwa nchi mbalimbali msitegemee kuwa hiyo mbinu mnayotumia italeta athari mnazozitegemea kama zilizotokea katika nchi hizo, tafuteni ushauri nje kabisa ya chama chenu, na isiwe kwa wale wafadhili wenu wanaowapeni pesa ili kuleta tafrani na kuzua commotion bila sababu za msingi, mtaendelea kupoteza na mtateketea kabisa.

APANDACHO MTU NDICHO AVUNACHO, MAPIGO MNAYOPATA NI MBEGU MBOVU MLIOIPANDA.
 
Kuna hasara gani kwani tukiwa na monarchy government..!!
Kila siku upupu hadi unashindwa kuamua :(
 
You have a poor brain ndio maana umeandika huu uharo hapa dammit!
Once again nonsense if not crap n your high stupidity level Next......
Wapinzani wanavuna walichopanda walipanda nini?
Tukutane 04/26/2018
Mnazidi kupanda na mtaendelea kuvuna................
 
soma vizuri, binti amefariki kutokana na maandamano haramu, wish Risasi ile ingemramba mmoja wa viongozi wenu.
Acha kutupia lawama wandamaji......
Mbona huwalaumu askari kutumia risasi za moto kwenye kadamnasi

Ova
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Assalam aleykhum wana JF,nimekaa na kutafakari nimetamani kunyamaza lakini nimeshindwa kujizuia kwa yale yanayotokea na kuendelea kwa jamii yangu pendwa ya Tanzania , nikiwa mtanzania halisi nilielelewa katika maandili ya kitanzania na kuitanguliza nchi yangu mbele kama mtanzania halisi mwenye dhamira safi ya kuilinda nchi yangu mpaka mauti yanikute

Nawapa pole sana familia ya Akwiline kwa msiba Mkubwa uliwakuta kwa kuondokea na binti yao mpendwa kwa Akwiline kufuatia kifo chake kilichosababishwa na maandamano haramu ya chama kimojawapo cha Siasa kinachojinasibu kuwa ni chama cha harakati na chenye kuleta ukombozi nchini Tanzania, nawalaani kwa Nguvu zote walioleta haya maandamano, na ninawaalani tena nikiomba hatima yao iwe ni mwaka 2020, wakati wa uchaguzi.

Narejea kwenye ujumbe wangu mahsusi, wapinzani mlichokipanda ndicho mnachokivuna, wakati wa MHE Rais wetu mpendwa Jakaya Mrisho kikwete, mlimbeza , mkamtukana, ilifikia wakati hata Mhe John John Mnyika akatamka kuwa hajawahi kuona Rais dhaifu kama yeye, je mnajua madhila mliokuwa mnayasababisha kwake yeye na familia yake?
, hewala aliwavumilia hata ilifikia wakati aliwaita ikulu mkanywa , juice, pamoja na vitafunwa, achilia mbali pocket money mlizokuwa mnapewa baada ya kikao na Mhe Rais.

Mlipokuwa mnatukana, mnakebehi, mnaandamana hovyo, kuna watu walikuwa nje ya game wanwacheki tu wanasema wallah siku nikikamata hili rungu hawa jamaa watanitambua, rungu limepata mwenyewe leo mnanyooshwa mnalialia, ******* ndani mnalialia, kumbukeni mbinu mlizotumia wakati ule ni hizi hizi mnazozitumia leo msitegemee kuitwa ikulu, mnywe juice,chai na baadae mpewe pocket money.

Ushauri wangu, hii nchi ni yetu sisi sote, kaeni chini mjiulize mmekosea wapi na mnapaswa kujirekebisha vip, social networks zilileta athari kwa nchi mbalimbali msitegemee kuwa hiyo mbinu mnayotumia italeta athari mnazozitegemea kama zilizotokea katika nchi hizo, tafuteni ushauri nje kabisa ya chama chenu, na isiwe kwa wale wafadhili wenu wanaowapeni pesa ili kuleta tafrani na kuzua commotion bila sababu za msingi, mtaendelea kupoteza na mtateketea kabisa.

APANDACHO MTU NDICHO AVUNACHO, MAPIGO MNAYOPATA NI MBEGU MBOVU MLIOIPANDA.
Tufafanulie walichokipanda na kile wanachokivuna.
 
Omuchimati, hujanikera nakuunga mkono, cdm hawajielewi walosema jana wakikumbushwa wanajitia pambani yaani wanajifanya kusahau: KIKWETE HAFAI DHAIFU lakini mkwere alicheka tu, kaja waliyemtaka DIKTETA, waliyemtaka sasa anawaonesha UKAKAMAVU, watulie waliyemtaka kaja!
 
Walichopanda cdm ni mbegu madhubuti isiyodhaifu baada ya kuidharau mbegu dhaifu, sasa cdm wanavuna walichopanda, raisi madhubuti!!!
 
Uzi ni ule ule. Haata kama hupendi, ni lazima uheshimu MAMLAKA iliyowekwa. Lets go Pr President
lakini mkumbuke hawa wapinzani sio mbuzi au ng'ombe kwamba ukiswaga, piga ua wao aah twende tu, nao wanabuni njia mbadala, hivyo hili suala mie naiomba serikali ni kwenda nalo makini sana, wasije wakaibuka akina m23 hapa, kwa sababu wao unaowasemea kinachowapa kichwa ni risasi, msije tupeleka likawa taifa la watu kujitoa mhanga, chonde chonde
 
Kwa akili yako unadhani magufuli ndio yupo sahihi? Jk ndio mtu aliyekubali mfumo wa vyama vingi, na vijana wa ccm mnafurahi maonevu haya ambayo hayapo kisheria, ipo siku naye atajuta!
 
Back
Top Bottom