Wapiga punyeto wanajinadi, wanajilaumu, wamechoka kujichua. Ukweli kuhusu punyeto ni upi?

Lighton

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
881
1,636
kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Ni utafiti ambao, umefanywa na unaendelea kufanywa na watu, ambao ni wahanga wa hiki kitendo(hili janga) ambao either ni wapenzi wa huu mchezo, ambao wamechoshwa na hiki kitendo au wale ambao wanatamani kuacha lakini wameshindwa kabisa kuacha.

Makala hii itaeleza visa mbalimbali, ambavyo ni matukio ya kweli ya wahusika waliokumbwa na changamoto hii au tuiite starehe hii kwa wale wanoiabudu.

Mrejesho wa utafiti unaanza na mimi mwenyewe ambae nimeshawahi kuandika makala mabalimbali zinahusu kujichua (punyeto), nilieleza changamoto nilizokutana nazo kipindi napambana kuachana na hiki kitendo, na changamoto hizo zilinipa nafasi ya kujua mambo kadhaa kuhusiana na punyeto.

1. Ugumu kwenye kujiepusha na matamanio ya kimwili
Kwa wapiga punyeto na wote ambao wamefikia ule umri wa kubalehe wanaelewa hii kitu, kuna muda unashindwa kujizuia kabisa tena kama upo stagnant hivi hufanyi kazi yoyote, yaani vile akili na mwili vinakuwa free, unakula na kushiba (hapa wengi wao ni wanafunzi) na wale ambao hawafanyi kazi ngumu, hawana wapenzi au wanao ila ni madomo zege, hapa hawawezi kutoboa.

Simply ni kwasababu satisfaction ya masturbation hahiitaji mambo mengi, its just your time, your will na sexual desire inafinalize. Hii changamoto unahitaji maombi kama kweli unataka kutoka, na sio maombi tu yaani wewe mwenyewe uwe willing kuacha.

2. Maandiko kuhusu punyeto
Ukifutilia wahanga wengi wa kujichua, wanajificha kwenye kivuli cha maandiko, sisemi kwamba hawapo sahihi, ila kama utashindana hoja za kiimani na mpenda punyeto atakueleza na kuchambua maandiko na utabaki huna hoja.

Ila ukimuuliza Mungu anaweza kubariki upigaji punyeto? Hawezi kukupa majibu. Ukirejea mada zangu ambazo nimewahi kuandika kuhusu punyeto, ukiangalia kwenye comment section utaona namna wapenda punyeto wanavyojitetea.

3. Scientific facts
Hapa kuna mkanganyiko kidogo. Kuna baadhi ya wataalam wa afya wanapinga ama kukilaani kitendo hiki kwasababu wanasema tafiti za kisayansi zimeonyesha upigaji punyeto unachangia kwa asilimia kubwa kwenye kupunguza nguvu za kiume kama kulegeza misuli ya uume, kuaffect sperm motility nk.

But at the same time, tafiti za kisayansi zinashauri upigaji punyeto kama njia sahihi ya kujiepusha na ugonjwa wa saratani ya tezi dume na ukwepaji wa magonjwa ya zinaa (unaona hapo kuna mkanganyiko).

4. Jamii
Hapa kuna mgawanyiko wa watu, kwasababu jamii ni watu, wapo ambao wanaona kitendo cha kujichua kinaathiri vijana kimaadili na kupelekea kusababisha mmomonyoko wa maadili kwasababu vijana, watu wazima au wazee wanajikita zaidi kwenye kutazama picha au video za ngono kitendo kinachopelekea uvunjifu wa maadili. Wakati huohuo kuna baadhi watu wanaona upingaji punyeto ni njia sahihi ya kujiepusha na magonjwa hatari kama UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.

Conclusion
kipi ni kipi? Miongoni mwetu wapo wapiga punyeto na ambao hawapigi punyeto kama Mapadri, wanandoa, wanafunzi, Wachungaji, Masheikh na binadamu wote wenye elimu kuhusiana na hii makala. Tupeane elimu ili hii makala pia iwe sehemu ya utafiti, ili tujiokoe na hili janga, ama tuendelee kufanya, kwa njia gani, ama wanaoacha waache kwa njia gani, au tusiwalaumu wapiga punyeto ama tuwalaumu, wale waliochoka waache kwa njia zipi?

Binafsi mimi ni mpinga punyeto, narudia tena siyo typing error mimi ni mpinga punyeto kwahiyio mimi nashauri vijana, na wazee tuache punyeto.

karibuni tupeane mawazo.
 
zimeonyesha upigaji punyeto unachangia kwa % kubwa kwenye kupunguza nguvu za kiume kama kulegeza misuli ya uume, kuaffect sperm motility nk.
UONGO UONGO UONGO

mwaka wa tatu huu nanyetuka

Bajet yangu ni 5000/- kwa kopo la mafuta ambalo linaisha kila baada ya miezi 7

Gono, UTI, Ngoma, Kaswende, HPV, Herpes na warts hua nazisikia kwenye radio na TV

Sijilaumu Kuwa Chamani
 
UONGO UONGO UONGO

mwaka wa tatu huu nanyetuka

Bajet yangu ni 5000/- kwa kopo la mafuta ambalo linaisha kila baada ya miezi 7

Gono, UTI, Ngoma, Kaswende, HPV, Herpes na warts hua nazisikia kwenye radio na TV

Sijilaumu Kuwa Chamani

"""Gono, UTI, Ngoma, Kaswende, HPV, Herpes na warts hua nazisikia kwenye radio na TV"""🤓🤓🤓🤓🤓🙌🙌🙌🙌
Hizi comment zako zinafanya nisiache huu mchezo..
Vijana hovyo sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom