GE2025 Wapiga kura Zanzibar kushiriki kura ya mapema leo Jumanne

GE2025 Wapiga kura Zanzibar kushiriki kura ya mapema leo Jumanne

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Wapiga kura visiwani Zanzibar leo Oktoba 28, 2025 wanaanza zoezi la kupiga kura katika kile kinachofahamika kuwa ni "kura ya mapema" ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa kuanzia saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na matokeo ya urais yatatangazwa ndani ya saa 72.

1761632266983.png

Uchaguzi huo unafanyika siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa kesho Oktoba 29, utakaofanyika Tanzania bara na visiwani.

Soma zaidi: INEC yatoa takwimu mpya: Wapiga Kura 37,647,235, vituo vya kupigia Kura 99,895 nchini

Rais wa sasa Hussein Mwinyi, kupitia chama tawala cha mapinduzi, CCM, anakabiliana na makamu wake wa kwanza, Othman Masoud Othman kupitia chama cha upinzani cha ACT Wazalendo. Chama hicho kimekuwa kikipinga kura hiyo ya mapema.

Vituo vya kura ya mapema vitafunguliwa saa moja asubuhi saa za Afrika Mashariki na kufungwa saa 10 jioni na matokeo ya urais yatatangazwa ndani ya saa 72 kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC.
 
Kwa kina Hamijay, hakuna mabalaaa kama huku Tanganyika
 
Vipo baadhi ya vyombo vya habari vilifika zanzibar siku ya leo kwa lengo la smear campaign lakini Tume huru ya Uchaguzi imewanyima fursa ya kudanganya...
 
Back
Top Bottom