Mende0,
Hilo halina ubishi wala halihitaji maelezo.
Wajua kwa upande wa Alizeti na Mafuta, Tanzania tunazalisha 40% tu ya mahitaji yetu ambayo ni sawa na 35,000MT. Hii haitoshi hata mahitaji yetu ya miezi miwili! Kwa mwezi Tanzania tunatumia 18,000MT na ili kufidia mahitaji tunaagiza zaidi ya 200,000MT kwa mwaka!
Mafuta ya kula kwa miongo mingi yamechukua nafasi ya pili katika vitu vinavyoongeza nakisi ya fedha za kigeni Tanzania. Kama tukijidhatiti kwenye hili zao si kama tutaweza kuzalisha ajira, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja tu, bali tutapunguza nakisi (Deficit) ya mizania ya malipo (BoP-Balance of Payments) na kuongeza fedha za kigeni kwani hata sasa huwezi amini; kwenye hizo 40% tunazozalisha, double refined oil yote inakwenda Holland. Hii ni kuonyesha uzuri wa mafuta yetu na mahitaji katika ulimwengu.
Kama kweli una nia kwenye hii sekta tuzidi kuwasiliana