Wapi nitapata mabasi yanayoenda Mtwara kutokea Dsm?

Wapi nitapata mabasi yanayoenda Mtwara kutokea Dsm?

Donkere91

Senior Member
Joined
May 28, 2016
Posts
185
Reaction score
162
Wadau wa Jf naomba msaada tutani,ni wapi napata mabus yanayoenda mtwara kutokea dsm,ofisi au namba za mawasiliano... msaada wa haraka plz
 
Wadau wa Jf naomba msaada tutani,ni wapi napata mabus yanayoenda mtwara kutokea dsm,ofisi au namba za mawasiliano... msaada wa haraka plz
Hapo ulipo, panda gari zinazoenda Temeke.
Waambie wakushushe Temeke Sudani.
Hapo Sudani ndipo kuna ofisi za magari yooote yanayokwenda Mtwara, Lindi, Masasi, Newala, Tandahimba, Mangaka na kusini yooooote!!!
Utaona ofisi zimejipanga kama mia hivi.

Note:
Kuna Temeke Sudani na Temeke mwisho.
Wakikupeleka Temeke mwisho ndio mabasi yanapoondokea asubuhi, we waambie wakupeleke Sudani ukakate tiketi.
Asante
 
Ulichomwambia Mleta Mada Akikifanyia Kazi Tu
Anasafiri Haraka
Mtwara Usafiri Tele
Kweli kabisa.
Mtwara mabasi mpaka ya saa 8 mchana.

Afande Sele anakwambia, wengine watabaki na roho za korosho na wengine watabaki na pesa za korosho.
Mtwara kucheleeee.

Mwambie mtoa mada akifika Mtwara kota za Bandari gereji, amsalimie Hamisi Waya
 
Hapo ulipo, panda gari zinazoenda Temeke.
Waambie wakushushe Temeke Sudani.
Hapo Sudani ndipo kuna ofisi za magari yooote yanayokwenda Mtwara, Lindi, Masasi, Newala, Tandahimba, Mangaka na kusini yooooote!!!
Utaona ofisi zimejipanga kama mia hivi.

Note:
Kuna Temeke Sudani na Temeke mwisho.
Wakikupeleka Temeke mwisho ndio mabasi yanapoondokea asubuhi, we waambie wakupeleke Sudani ukakate tiketi.
Asante
Mkuu umetisha sana! Sasa kwa kukusumbua kdg unaweza recomend bus gan/company gani hasa inajielewa ktk usafirishaji kwenye route hyo!? Na kama huez toa shout out ya bure hapa...ning'ate hata sikio DM.

Asante
 
Zamani Mtwara ulikuwa mkoa mkubwa sana, vipi ulishagawanywa? Tulisoma wakati kuna mikoa 20. Pwani, Mtwara, Tabora, Kigoma, Dodoma, Singida, Mara, Shinyanga, Mwanza, Ziwa Magharibi, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mbeya, Iringa, Ruvuma ndo unaongeza za visiwani ambazo sizikumbuki. Sasa kuna utitiri wa mikoa hivyo sijui kulikoni? Population imechangia au ulafi wa madaraka? Kuna nchi zina Count zile zile for almost over 200 years na bado zina manage. Mwishowe kila kata itakuwa jimbo mradi kuna kibosire anataka kuchukua hilo eneo.
 
Hapo ulipo, panda gari zinazoenda Temeke.
Waambie wakushushe Temeke Sudani.
Hapo Sudani ndipo kuna ofisi za magari yooote yanayokwenda Mtwara, Lindi, Masasi, Newala, Tandahimba, Mangaka na kusini yooooote!!!
Utaona ofisi zimejipanga kama mia hivi.

Note:
Kuna Temeke Sudani na Temeke mwisho.
Wakikupeleka Temeke mwisho ndio mabasi yanapoondokea asubuhi, we waambie wakupeleke Sudani ukakate tiketi.
Asante
Umemfafanulia vema sana. Ama kwa Mabasi ya Mtwara na Masasi,yapo yanayoanzia Ubungo Bus Terminal hasa Buti la Zungu,Maning Nice na Tashrif. Pia kuna Maning Nice linaanzia Morogoro asubuhi kwenda Mtwara kupitia Ubungo na Temeke Mwisho/ Sudan. Pia yapo Tashrif yanayotokea Tanga moja kwenda Mtwara na lingine Masasi,haya hupita Ubungo Terminal Saa 7 na Temeke Mwisho saa 8 kuelekea Mbagala then Mtwara basi Moja na Masasi basi lingine.
Lakini pia mdau anapaswa kufahamu kama nyongeza:-
1. Magari yote ya Wilaya za Mtwara na Lindi huanzia Temeke mwisho saa 12 asubuhi na Mbagala( Newala,Tandahimba,Mangaka,Tunduru,Rwanga,Nachingwea). Lakini yapo Magari mengi mazuri na makubwa yanaanzia Mbagala karibu kila baada ya saa 1 hadi saa9 kuelekea Wilayani Kilwa ila stendi ni Mbagala. Kwa safari za mjini Mtwara mabasi mengi huanzia saa 12 Ubungo na basi la Machinga huanzia Temeke saa 12 asubuhi.
2. Ukitaka kwenda Mjini Mtwara mabasi mengi huanzia saa 2 hadi saa 9 na mara nyingi huwa ni mabasi yenye hadhi nzuri kwa maana yana full Ac na kuna ustaarab mkubwa kwa route za mchana,na utapanda saa2,3,4,5,6 7 na saa 8 siku nyingine hadi saa9,yaani unajitune muda uutakao,lakini huanzia Temeke Mwisho. Mabasi hayo ni Leo,Buti la Zungu,Ibra Line,Maning Nice,Machinga,King Yasin nk. Kazi kwako
2.
 
Back
Top Bottom