Wapi nitapata mabasi yanayoenda Mtwara kutokea Dsm?

Wapi nitapata mabasi yanayoenda Mtwara kutokea Dsm?

Ubungo hakuna basi ya Mtwara, labda uvizie zikienda pakia mzigo, na ni bahati kuikuta.
Afu sio Ubungu ni Ubungo
Zipo dadangu tena zipo kabisa.. ni zile zinazoanzia safari zake saa 12 asubuhi.. Machinga, Maning nice nk.. nishawahi pandia UBUNGO zaidi ya mara 3
 
Zamani Mtwara ulikuwa mkoa mkubwa sana, vipi ulishagawanywa? Tulisoma wakati kuna mikoa 20. Pwani, Mtwara, Tabora, Kigoma, Dodoma, Singida, Mara, Shinyanga, Mwanza, Ziwa Magharibi, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mbeya, Iringa, Ruvuma ndo unaongeza za visiwani ambazo sizikumbuki. Sasa kuna utitiri wa mikoa hivyo sijui kulikoni? Population imechangia au ulafi wa madaraka? Kuna nchi zina Count zile zile for almost over 200 years na bado zina manage. Mwishowe kila kata itakuwa jimbo mradi kuna kibosire anataka kuchukua hilo eneo.
Mtwara haujawahi kuwa mkoa mkubwa.. Ulikuwa namba tatu kwa udogo.. ukitoa Dar na Kilimanjaro
 
Mtwara haujawahi kuwa mkoa mkubwa.. Ulikuwa namba tatu kwa udogo.. ukitoa Dar na Kilimanjaro
Kwa orodha aliyotoa yuko sahihi,hapo mwanzo mkoa wa Mtwara na Lindi ulikuwa mmoja..Huyo mtoa hoja atakuwa ni mhenga usimmbishie Mkuu.
 
Mtwara haujawahi kuwa mkoa mkubwa.. Ulikuwa namba tatu kwa udogo.. ukitoa Dar na Kilimanjaro
Dar imekuja kuwa mkoa hivi karibuni. Enzi zetu ilikuwa chini ya mkoa wa Pwani na hata Pwani isingeingia kwa Mtwara. Mkoa uliokuwa mkubwa ulikuwa Tabora ukifuatiwa na mkoa wa Arusha. Nenda kwenye ramani za Sixties mpaka wanaanza kugawana mikoa hivi karibuni. Mkoa wa Kilimanjaro kwanza ni mdogo kuliko Dodoma. Dar yenyewe inazidiwa na Bariadi kwa ukubwa.
 
Zipo dadangu tena zipo kabisa.. ni zile zinazoanzia safari zake saa 12 asubuhi.. Machinga, Maning nice nk.. nishawahi pandia UBUNGO zaidi ya mara 3
Yeah, nilishajibiwa pale juu kaka.
Asante sana
 
Hapo ulipo, panda gari zinazoenda Temeke.
Waambie wakushushe Temeke Sudani.
Hapo Sudani ndipo kuna ofisi za magari yooote yanayokwenda Mtwara, Lindi, Masasi, Newala, Tandahimba, Mangaka na kusini yooooote!!!
Utaona ofisi zimejipanga kama mia hivi.

Note:
Kuna Temeke Sudani na Temeke mwisho.
Wakikupeleka Temeke mwisho ndio mabasi yanapoondokea asubuhi, we waambie wakupeleke Sudani ukakate tiketi.
Asante

Mabasi yanaanzia ubungo
 
Dar imekuja kuwa mkoa hivi karibuni. Enzi zetu ilikuwa chini ya mkoa wa Pwani na hata Pwani isingeingia kwa Mtwara. Mkoa uliokuwa mkubwa ulikuwa Tabora ukifuatiwa na mkoa wa Arusha. Nenda kwenye ramani za Sixties mpaka wanaanza kugawana mikoa hivi karibuni. Mkoa wa Kilimanjaro kwanza ni mdogo kuliko Dodoma. Dar yenyewe inazidiwa na Bariadi kwa ukubwa.
Lindi ndiyo kubwa
 
Kuna private Vanguard nikusubiri wapi utavaaje na saa ngapi niko alone Madame B
 
Mtwara haujawahi kuwa mkoa mkubwa.. Ulikuwa namba tatu kwa udogo.. ukitoa Dar na Kilimanjaro
Ni kweli tupu. Nafikiri mkoa huo unaingia mara 3 kwa Lindi,Morogoro,Tabora. Ila kwa udogo wake,na idadi ya watu,unaweza kusema ukiondoa Dar na Kilimanjaro,nao una population density kubwa.
 
Atakuwa alienda na amerudi na wasafi nadhani sasa hivi atakuwa anatafuta bus la moro ama iringa
Hajarudi alipitiliza hadi Nachunyu hala za korosho zilitoka huko.
 
Back
Top Bottom