Wapi nitapata brown rice kwa bei nzuri?

Zasasule

JF-Expert Member
Aug 12, 2009
1,001
103
Hello jf!!
Naomba msaada wenu... Je ni wapi nitapata brown rice kwa bei nzuri? Namaanisha usiyokuwa ghali saana.. Natanguliza shukran...
 
Kama wa kula nenda kwenye supermaret upo unatoka Magugu Arusha na wameweka lebo ya wanaotengeneza kuanzia hapo waweze endelea ,upo Shoprite TSN supermarkets
 
Mchele wa kutoka magugu ni brown? mbona mweupe ingawa si kwa sana.

Upo Shoprite kuna kiwanda huko Arusha ndio huuza na watoka Magugu,pia upo mweupo wa kutoka Magugu,sijui teknolojia wanayotumia kuukoboa hadi kubakia brown.najua ninachokisema kwa vile ni mdau wa brown rice na ninaposema brown rice si maanishi rangi tu ya brown bali ni kuwa kiini chake hakijasagwa/kobolewa
 
oooh kwani huu brown rice unasaidia nini..

Brown rice ni kama vile unga wa dona nafikiri waelewa tofauti ya unga wa dona na unga wa sembe.brown rice kama ilivyo dona hutumiwa sana na watu wenye kisukari,pia kiafya ni lishe yenye virutubisho vyote ,mchele mweupe kama ilivyo sembe umekosa viini na virutubisho wenyewe huita kama vile unakula makapi,vivyo hivyo ni sawa na brown bread ukilinganisha na white bread
 
Umenena vyema.
 
Kama wa kula nenda kwenye supermaret upo unatoka Magugu Arusha na wameweka lebo ya wanaotengeneza kuanzia hapo waweze endelea ,upo Shoprite TSN supermarkets

thanx man.. nimeenda shoprite nimekuta wanauza 3800 kwa kg1 na huo uko tayari kwenye package yake. je kuna sehemu ambayo nitapata bei ahuen zaidi ya hii
 
Brown rice kwa bei ya 3000 kwa kilo inapatikana. Wasiliana nami-PM nikupe maelekezo.

Toa oder yako mapema tukuandalie.

Hello jf!!
Naomba msaada wenu... Je ni wapi nitapata brown rice kwa bei nzuri? Namaanisha usiyokuwa ghali saana.. Natanguliza shukran...
 
Ninatafuta mchele wa brown kwa bei ya jumla. Tafadhari mwenye taarifa yoyote ya mahali ninapoweza kuupata anisaidie
 
arsenic levels? kuna data yoyote kutoka TFDA inayoonesha kiwango cha arsenic katika michele kutoa sehem mbalimbali Tanzania? hasa hii brown rice.

au kiwango cha walaji hakijafikia kiwango cha kuchochea utafiti huo?
 
Back
Top Bottom