Wapi naweza kupata simcard za Uwakala M-pesa/Tigopesa

princess ariana

JF-Expert Member
Aug 19, 2016
8,697
17,320
Habari wapendwa;
Kwa yeyote anaefahamu namna gani naweza kupata Line za uwakala za Tigopesa/Mpesa(process)
-Namna ya kufatilia
-Garama za kununua
-zinapatikana wapi

Naomba anifahamishe
(sio za watu wanaoziuza mitaani lakini, nataka OG kusajili kwa Majina ya muhusika)

Ahsanteni
 
unatakiwa uwe na TIN number,Leseni ya Biashara na Kitambulisho. Cha kuongezea hela ya mtaji basi, kwa voda nenda kwny voda shop au wana mameneja wao wa maeneo na kwa tigo nenda kwa mawakala wakuu
 
Tin namba? ndio nini mkuu
Leseni ya biashara
Mawakala ws kuu ndio wapi hao
 
Habari wapendwa;
Kwa yeyote anaefahamu namna gani naweza kupata Line za uwakala za Tigopesa/Mpesa(process)
-Namna ya kufatilia
-Garama za kununua
-zinapatikana wapi

Naomba anifahamishe
(sio za watu wanaoziuza mitaani lakini, nataka OG kusajili kwa Majina ya muhusika)

Ahsanteni
1. Leseni ya biashara.
2. TIN number.
3. Kitambulisho (cha kura au chochote).

Ukishakuwa na vitu hivyo peleka vodashop / tigo shop. Kama upo dar kwa voda nenda m.city makao makuu ya voda ulizia block tu then uliza kitengo cha mawakala.
Mambo murua kabisa
 
Upo mkoa gani?
Fika ofisini kwao watakusaidia, mtaani watakupiga hela bure.
 
Tin namba? ndio nini mkuu
Leseni ya biashara
Mawakala ws kuu ndio wapi hao
Tin namba unapata tra ya mapato yao kwa hiyo watakadiria ni kiasi gani unaingiza kwenye Duka lako na leseni kibali cha kufanya biashara.Wakala Mkuu ni Wakala ambaye atakua karibu yako .atakupa huduma kama za float.mabango. vitabu.huduma zote za Tigo pesa unakua unapata kwake
 
ooh kwahiyo TrA nako naanzaje jamani... niende na Tsh ngapi

hii kazi ya kufatilia sio mchezo
 
Sio mchezo ndo maana watu wengi wanaona bora Kuchukua za mtaani.watakudiria kulingana na Duka lako lilipo na biashara utakayoweka.apo uwe makini usije lipishwa tofauti na mapato unavyoingiza.ukishakamilisha ukipeleka ofisin Voda itachukua mwenzi mzima ndo upate laini
 
Duuh, kwahiyo niende TrA nikiwa nmeshajua frem naiweka wapi
 
Back
Top Bottom