Wapi Ilipokuwa Ofisi ya Market Master Kariakoo Market?

Wapi Ilipokuwa Ofisi ya Market Master Kariakoo Market?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,420
Reaction score
33,982
Ilipokuwa inapita Barabara ya Swahili makutano na Mtaa wa Tandamti nimekuta pamejengwa na ni sehemu ya Soko la Kariakoo.

Mtaa wa Swahili unakatika hapo na unakuja kuendelea kuanzia Mkunguni kwenda mbele.

Hapo niliposimama kwenye picha nimesimama ilipokuwa zamani Barabara ya Swahili na nikiangalia nje naiona barabara yenyewe.

Miaka mingi imepita lakini akili yangu inaniambia hapo niliposimama kushoto kwangu ndipo ilipokuwa Ofisi ya Market Master, Abdul Sykes katika miaka ya 1950 na yote ninayoeleza yalifanyika sehemu hiyo.

Nikiipa mgongo makutano ya Mtaa wa Swahili na Tandamiti nikiangalia Mtaa wa Mkunguni kushoto kwangu ndiko ilipokuwa ofisi yenyewe.

Abdul Sykes, Julius Nyerere, Shariff Abdallah Attas, Mshume na wazalendo wengine waliopita ofisi ile wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika hata kwa mbali hawakupata kufikiria kuwa uhuru utakuja kuleta nema kama hii - Soko zuri la kisasa na la kupendeza.

Itoshe kuwa Soko hili lilijengwa wakati Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Tanzania.

Angalia Mtaa wa Swahili picha nimeipiga nikiwa ndani ya Soko nimesimama ilipokuwa zamani inapita barabara.

1770896153460.png

1770896282774.png
1770896303157.png

1770896318004.png
1770896333946.png

Shariff Abdallah Omar Attas katika ujana wake akifanya kazi Kariakoo Market.
 
Back
Top Bottom