Wapi ilipo ndege ya Malaysia MH 370?

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,320
11,327
Mimi binafsi nililitilia shaka suala zima la ndege ya Malaysia kutoweka angani na isipatikane kokote kwenye uso wa dunia mpaka hivi leo, bado nalitia mashaka suala hilo kwamba halina ukweli wowote ndani yake, bali ni moja kati ya filamu zao nyingi wanazo ziigiza ilikuendelea kuulaghai umma, lakini zaidi mimi naona ni hayo ni

MAANDALIZI YA KUMTAFUTA ADUI MPYA ATAKAYE CHUKUA NAFASI YA ‘VITA DHIDI YA UGAIDI’.

Kwa kuanzia tu, tuitazame moja ya nambari kuu zinazo pendelewa kutumiwa kishetani na Illuminati, nambari 11.

Wakati ndege hiyo ya Malaysia ikipotea ndani yake kuliwa na abiria 227, nambari hiyo ni sawa na 2+2+7=11, ndege yenyewe ni Boeing 777 nambari inayogawika kwa 11.

Ndege hiyo ya Malaysia ilipatwa na ‘ugonjwa’ kama ule uliozipata ndege za 9/11 ambayo tunajua kuwa tukio lile lilifanywa na utawala wa Bush mwenyewe.

1. Ndege hiyo ya Malaysia ilipoteza mawasiliano kama zilivyokuwa ndege za 9/11. Masaa mawili baada ya ndege hiyo kuondoka ilipoteza mawasiliano kabisa na kitengo cha anga ambacho ndicho kilicho kuwa na dhamana ya kuiongoza ndege hiyo.

2. Ndege hiyo iliacha njia yake ya safari kama ilivyokuwa kwenye 9/11. Ndege hiyo ya Malaysia ikaendelea kusafiri maelfu ya maili nje ya njia yake iliyopaswa kupita bila hata ya kutuma taarifa za tahadhari na msaada kwenye kituo chochote cha kuongezea ndege na kisha ‘ikatoweka’ kama mazingaombwe vile.

3. Ndege hiyo ikapotea kabisa na isionekane kama zilivyo potea ndege iliyo gonga Pentagon na ile ya Pennsylvania kwenye tukio hilo la 9/11.

4. Kama ilivyokuwa kwenye 9/11, kwenye ndege ya Malaysia nako abiria simu zao zilikuwa hewani!!!!!

Kila mtu anajiuliza ni nini hicho? Ndugu na jamaa wa abiria kwenye ndege iliyo potea wamethibitisha kusikia milio ya simu walipojaribu kuwapigia wapendwa wao. Na pia baadhi ya kurasa za fecebook za abiria hao zimeonesha kuwa wapo ‘online'.

Shirika hilo la ndege la Malaysia limethibitisha pia simu ya mhudumu aliyekuwepo kwenye ndege hiyo nayo iliita tu bila kupokelewa na mtu yeyote mpaka ikakata kama zilivyo fanya simu 19 za abiria walio kuwepo kwenye ndege hiyo baada ya kupigia na ndugu na jamaa. Hayo yalisemwa na msemaji wa shirika hilo bwana Hugh Dunleavy.

Lakini pia hadithi ya simu za abiria na ile ya muhudumu kuita inatupatia mwanga wa jambo moja, kwamba ndege hiyo haipo ndani wala chini ya bahari! Simu haiwezi kuita kama ipo ndani ya maji, lakini zaidi simu hiyo lazima iwepo karibu na mnara wa simu, ambao tunajua hauwezi ukawepo chini ya bahari isipokuwa aridhini.

5. Kama ilivyokuwa kwenye 9/11 hapa napo kwenye ndege ya Malaysia mapema kabisa Illuminanti walianza kutoa dondoo za tukio zima takribani miaka minne kabla. Tizama picha hii inayofuata na linganisha na tukio lenyewe kisha kuna kichwa na kujiuliza ikiwa tangazo kwenye picha hiyo limetokea kwa bahati mbaya?

Tunapoendelea kulitolea macho suala hili, tunayo maswali ya msingi ya kujiuliza, kumbukua hapa tunazungumzia ndege kubwa aina ya Boeng, ndege ya kisasa kabisa, ndege hii haijalipuka, haijaanguka mahala kokote, si nchi kavu si baharini, imetoweka ghafla, narudia tena IMETOWEKA GHAFLA ikiwa angani, na haijapatikana mpaka hivi leo.

Vipi kama vile MUVI linajirudia ...?

Vipi wanataka kututengenezea Septemba 11 nyingine au?

Swali # 1

Ndege zote aina ya Boeing 777 zimetengenezwa pamoja na ‘Black Box’ ambayo inaweza kuhimili mlipuko wa aina yeyote ule utakaoipata ndege hizo. Kisanduku hicho kinabeba taarifa zote muhimu yakiwemo mawasiliano ya hatua kwa hatua tangi ndege inapotokea mpaka inapo elekea.

Swali linakuja NI VIPI KIBOKSI HICHO KIMESHINDWA KUTUELEKEZA WAPI NDEGE ILIPO?

Swali # 2

Black Box zote zinayo uwezo wa kuendelea kusafirisha mawasiliano na kutambua wapo kilipo hata kwa muda wa siku 30 hata kama ndege ikiwa imezama baharini.

Swali linakuja ni kitu gani hicho kilicho zima ‘signal’ ya kisanduku hicho kiasi kwamba shughuli za kuipata ndege hiyo zimekuwa ni ndoto. Tunajua ndege hiyo haijawaka moto wala kuzama baharini, sababu simu za abiria na wafanyakazi wa ndege zilikuwa zikiita kila zinapo pigwa. Sasa inakuwaje simu zinaweza kuendelea kuleta mawasiliano lakini kisanduku cheusi kipoteze mawasiliano kabisa?

Swali # 3

Ndege inapokuwa imepotelea baharini, mara zote kuna sehemu na mapande ya ndege hizo yataonekana yakielea baharini.

Kama ndege ya Malaysia ingekuwa imetungulia na kushushwa chini basi vipande lazima vingeonekana vikielea baharini, lakini viko wapi vipande hivyo? Ndege ya Boeing 777, imetoweka ghafla kwenye uso wa dunia, IMETOWEKA, ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.

Swali # 4

Mahala ambapo ndege hiyo ‘imepotelea’ panafahamika. Waongozaji wa ndege wanakuwa taarifa zote za ndege husika, kumbuka wao ndiyo waongozaji, hivyo nukta ambayo ndege inakata mawasiliano na wao wanakuwa wanafahamu ilikuwa eneo gani, ilikuwa kwenye mwendo kasi wa aina gani, vyote hivyo vinaweza kutumika kuelekeza ni wapi mapande ya ndege hiyo yanaweza kuwa yameangukia. Lakini ni vipi ndege hii ya Malaysia imeshindwa kupatikana chochote pamoja na kwamba inafahamika ni wapi nukta ya mwisho ilionekana kwenye rada?

Swali #5

Tuseme Ndege 370 ya Malaysia imetekwa, lakini ndege haipotei kwenye rada hata kama ikitekwa. Sasa inakuwaje ipotee hata kwenye rada isionekane?

Ndege nambari 370 ya Malaysia aina ya Boing 777 HAIJALIPUKA, HAIJANGUKA KOKOTE, ILA IMETOWEKA? KIVIPI??

Itaendelea....

Malaysia-missing-plane.jpg
 
Mtoa post usiwe mjinga

Wabongo tumezidi kuamini uchawi na mambo ya freemason ndio maana hatuendelei

Hiyo ndege ni kuwa inawezekana ilivyopoteza mawasisiano iliendelea kuwa hewani hadi pale marubani walipoona mafuta yameisha wakaamua kutua kama ile ndege ya american airline

ilivyotua kwenye maji na watu wote wakapona

So Inawezekana marubani akili yao ilikuwa ni kutua ikiwezekana ielee kwenye maji hadi hapo msaada utakapopatikana

Hivyo inawezekana walifanikiwa kutua juu ya maji bila ndege kulipuka au kugawanyika hivyo ikaanza kuzama mdogo mgogo hadi chini ya bahari

Alafu usijidanganye kuwa kila mawasiliano yanategemea minara, Hapana, kuna baadhi ya makampuni yanatumia satellite kama signal yao kuu ya mawasiliano hivyo kama ndege ilikuwa ishazama na bado maji yalikuwa hajaingia ndani si kitu cha kushangaza kama sim bado zilikuwa zinaita

Kama curiosity iliyopo sayari ya marz ipo umbali wa mabilioni ya km kutoka duniani na bado inadetect mawasiliano pamoja na satelite iliyopo duniani basi sio kitu cha kushangaza sim iliyo chini ya bahari kudetect mawasiliano

Na ukitaka kujua hii ndege kweli ipo chini ya bahari ni yale baadhi ya masalia ya mbawa zake yaliopatikana kandokando ya bahari mwaka uliopita. Kampuni ya Boeing ilithibitisha kuwa yale mabaki ambayo ni vipande vidogo vilivyochomoka kwenye mbawa ni mabaki ya MH 370
 
Umemjibu vizuri sana; na kama ni mtu wa kuelewa amekuelewa. Watu wa conspiracy theory hawa wana matatizo. Kila kitu ni illuminati na mijongeo ya namba hata kama haina uhusiano. Ona sasa mpaka anadanganya eti (Boeing) 777 inagawanyika na 11? Asante Richaabra!
 
Ile ndege ya America si ilitua on a river jamani,juu ya mto na sio bahari..labda sijui ila ndege kutua juu ya bahari inakuja na speed kubwa halafu urefu wa bahari kuelekea chini na the entire volume,dragforce pamoja na mawimbi sio rahisi kwa ndege kutua salama juu ya bahari ikae mda wa kutosha kiasi cha simu zote kuweza kupatikana,Kama hii ndege ilizama inamaana ilitua juu ya bahari katika impact kubwa na wakati inaendelea kupungua speed kuna sehemu Lazima ziliharibika na maji yakaingia ndani hivyo ndege ikazama mpaka chini ya bahari lakini hii case sio rahisi Sana mara nyingi ndege zikitua juu ya bahari zinaishia kuvunjikavunjika na kuungua na moto kwasababu ya mafuta yanayoelea...nadhani hii case Ni sahihi ika challengiwa katika angles zote(theories tofauti)ila sio kuipa majibu marahisi...na wabongo sio watu pekee wanao question Illuminati na Freemason..hawa Ni watu wenye nguvu Sana duniani na wanafanya mipango yao kwa intelligence kubwa.Kwa hiyo aliyeleta Uzi huu sio mtu wa kwanza kuuliza hayo maswali.Majibu ya vitu vingine yako out of normal logic.
 
We unaongelea ndege nyingine. Unaongelea ile iliyogongana na ndege warukao wakaharibu injini zote ikatua mto wa Hudson Marekani kapteni Sully akiwa rubani? Imetengenezewa mpaka na muvi na Tom Hanks ndiyo ameact kama Captain Sully? Hiyo ni nyingine....

Kama Captain Sully aliweza kutua mtoni aki-glide akaokoa abiria wote, kwa nini isiwezekane ku-glide baharini? Ni lazima ndege ikitua baharini isambaratike? Hii ni kanuni ya jumla ya kifizikia?

Nimewahi kukaa Marekani kwa miaka saba na haya mambo ya Illuminati na Freemason siyo dili sana kama ilivyo huku kwetu kwa waamini uchawi na maluweluwe. Kila siku kwenye magazeti ya Shigongo Freemason hivi, Illuminati wamefanya hivi mpaka mwishowe watu wanaamini. Again inawezekana hata dunia ni flat na ni conspiracy ya hawa Illuminati kutudanganya kuwa ni duara!!!
 
richaabra ingekuwa darasani kila mwalimu anapoona mtu hafahamu kitu, akamuita mjinga ingekuwaje? Utaitaje mtu mjinga na bila aibu na jibu refu juu, hapo unafikiri imevutia? sijakusoma.
 
HII NI MARA YA PILI SASA UNAKOPI POSTI KUTOKA KWENYE BLOGI YANGU, "salim msangi" na kuviweka huku kwenye JAMII FORUM KAMA VILE WEWE NDIYE ORIGINATOR WA THEMES/TOPIC/POST.
TAFADHALIA ZINGATIA SHERIA YA MITANDAO NA SHERIA YA HABARI. TAFADHALI KABLA YA KUFANYA TENA HIVYO AU KUEDNELEA KUKOPI NA KUPOSTI KUTOKA KWENYE BLOGI NILIYOITAJA HAPO JUU, WASILIANA NA MIMI KWA NJIA YEYOTE ILE INAYOWEZEKANA, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE.
KENGO LA KUFANYA HIVI NI KUILINDA KAZI YANGU. WADAU WAMEULIZA MASWALI NA WAMECRITISIZE ULICHOKIPOSTI HAPA LAKINI SI DHANI KAMA UTAWEZA KUYAJIBU AU KUWAELEWESHA, SABABU WEWE SIYO ORIGINATOR WA MADA HUSIKA, TAFADHALI, WASILIANA NA MIMI KABLA YA KUENDELEA NA UTARATIBU HUU.
 
Mtoa post usiwe mjinga

Wabongo tumezidi kuamini uchawi na mambo ya freemason ndio maana hatuendelei

Hiyo ndege ni kuwa inawezekana ilivyopoteza mawasisiano iliendelea kuwa hewani hadi pale marubani walipoona mafuta yameisha wakaamua kutua kama ile ndege ya american airline

ilivyotua kwenye maji na watu wote wakapona

So Inawezekana marubani akili yao ilikuwa ni kutua ikiwezekana ielee kwenye maji hadi hapo msaada utakapopatikana

Hivyo inawezekana walifanikiwa kutua juu ya maji bila ndege kulipuka au kugawanyika hivyo ikaanza kuzama mdogo mgogo hadi chini ya bahari

Alafu usijidanganye kuwa kila mawasiliano yanategemea minara, Hapana, kuna baadhi ya makampuni yanatumia satellite kama signal yao kuu ya mawasiliano hivyo kama ndege ilikuwa ishazama na bado maji yalikuwa hajaingia ndani si kitu cha kushangaza kama sim bado zilikuwa zinaita

Kama curiosity iliyopo sayari ya marz ipo umbali wa mabilioni ya km kutoka duniani na bado inadetect mawasiliano pamoja na satelite iliyopo duniani basi sio kitu cha kushangaza sim iliyo chini ya bahari kudetect mawasiliano

Na ukitaka kujua hii ndege kweli ipo chini ya bahari ni yale baadhi ya masalia ya mbawa zake yaliopatikana kandokando ya bahari mwaka uliopita. Kampuni ya Boeing ilithibitisha kuwa yale mabaki ambayo ni vipande vidogo vilivyochomoka kwenye mbawa ni mabaki ya MH 370

Na mie Wacha nikuchallenge,

Ikiwa imetua baharini kwa nini ishindikane kuokoa abiria? Pili kama ndege haiku vunjika na kutua baharini haiwezi kuzama moja kwa moja lazima abiria wangeokoa maisha yao.

Suala la mwanzo la usalama wa abiria ni kuokoa maisha yao, vipi ishindikane hilo? Fuatilia hio picha ya ndege ya usa iliyo tua baharini ilichukua muda gani hadi kuzama?
 
HII NI MARA YA PILI SASA UNAKOPI POSTI KUTOKA KWENYE BLOGI YANGU, "salim msangi" na kuviweka huku kwenye JAMII FORUM KAMA VILE WEWE NDIYE ORIGINATOR WA THEMES/TOPIC/POST.
TAFADHALIA ZINGATIA SHERIA YA MITANDAO NA SHERIA YA HABARI. TAFADHALI KABLA YA KUFANYA TENA HIVYO AU KUEDNELEA KUKOPI NA KUPOSTI KUTOKA KWENYE BLOGI NILIYOITAJA HAPO JUU, WASILIANA NA MIMI KWA NJIA YEYOTE ILE INAYOWEZEKANA, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE.
KENGO LA KUFANYA HIVI NI KUILINDA KAZI YANGU. WADAU WAMEULIZA MASWALI NA WAMECRITISIZE ULICHOKIPOSTI HAPA LAKINI SI DHANI KAMA UTAWEZA KUYAJIBU AU KUWAELEWESHA, SABABU WEWE SIYO ORIGINATOR WA MADA HUSIKA, TAFADHALI, WASILIANA NA MIMI KABLA YA KUENDELEA NA UTARATIBU HUU.
Wacha zako, hii media inaweka habari zote kutoka media tofauti na kujadiliwa hapa
 
Academic integrity ipo kiwango cha chini Sana, hata Kama copy and paste, mleta mada haushughulishi akili hata kidogo?

Mpemba Kama sikosei alilipwa 2M kwa kuokota bawa la hiyo ndege na alipewa huo mpunga baada ya Boeing. Kuthinitisha ni masalia ya hiyo ndege.

Unapopost jambo lipitie kidogo mkuu
 
HII NI MARA YA PILI SASA UNAKOPI POSTI KUTOKA KWENYE BLOGI YANGU, "salim msangi" na kuviweka huku kwenye JAMII FORUM KAMA VILE WEWE NDIYE ORIGINATOR WA THEMES/TOPIC/POST.
TAFADHALIA ZINGATIA SHERIA YA MITANDAO NA SHERIA YA HABARI. TAFADHALI KABLA YA KUFANYA TENA HIVYO AU KUEDNELEA KUKOPI NA KUPOSTI KUTOKA KWENYE BLOGI NILIYOITAJA HAPO JUU, WASILIANA NA MIMI KWA NJIA YEYOTE ILE INAYOWEZEKANA, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE.
KENGO LA KUFANYA HIVI NI KUILINDA KAZI YANGU. WADAU WAMEULIZA MASWALI NA WAMECRITISIZE ULICHOKIPOSTI HAPA LAKINI SI DHANI KAMA UTAWEZA KUYAJIBU AU KUWAELEWESHA, SABABU WEWE SIYO ORIGINATOR WA MADA HUSIKA, TAFADHALI, WASILIANA NA MIMI KABLA YA KUENDELEA NA UTARATIBU HUU.
Kumbe amecopy na ku-paste tu. Basi bila shaka tumeingia kwenye mjadala bubu...

Plagiarism ni tatizo kubwa kwetu na wengi wamefaulu kwa kudesa vipeperushi vya Nyambari Nyangwine. Hakuna critical thinking yo yote. Ndiyo maana elimu yetu hii haitusaidii cho chote. Kwa wenzetu huko nje aisee ni wakali sana kuhusu Plagiarism na kama unataka uaibike kitaaluma we copy kazi ya mtu kama ilivyo hata kama ni aya moja halafu usitoe credit sawasawa. Moto utakaokuwakia aisee hutakaa uamini.
 
Wacha zako, hii media inaweka habari zote kutoka media tofauti na kujadiliwa hapa
Anaye weka habari hapa anabeba dhamana ya habari hiyo, endapo habari hiyo itasababisha lolote baya au zuri kwa mtu, taasisi, au kikundi cha watu au nchi kwa ujumla wake, aliweka habari hapa anakuwa ndiyo wa kwanza kuwajibika na habari hiyo. Hivyo unaposema inaweka habari zote, hii siyo mtu mwenye utashi bali ni chombo, muwekaji wa habari ni wewe na mimi, ndiyo maana kuna sheria ya habari, sheria ya hati miliki ya habari, ambazo zina lengo la kumlinda na kuuongaza mtoa habari kulingana na taratibu za jambo hilo. Unavyo weka habari ambayo si yako lazima utanabaishe wazi kuanzia mwanzo kuwa habari hii ni kwa mujibu wa "-----" ili likitokea la kutokea inajulikana chanzo cha habari hiyo ni ipi, lakini si kujifanya ni yakwako halafu ukibanwa ndiyo unaanza oooh! mimi niliikuta tu, sijui mimi .... acha hizo. kama umeikubali kazi yangu just simple niandikie kwenye email kuwa naomba niwe na post kazi zako mahala fulani, na mimi nitakupa utaratibu wa kufanya hivyo.
 
Kumbe amecopy na ku-paste tu. Basi bila shaka tumeingia kwenye mjadala bubu...

Plagiarism ni tatizo kubwa kwetu na wengi wamefaulu kwa kudesa vipeperushi vya Nyambari Nyangwine. Hakuna critical thinking yo yote. Ndiyo maana elimu yetu hii haitusaidii cho chote. Kwa wenzetu huko nje aisee ni wakali sana kuhusu Plagiarism na kama unataka uaibike kitaaluma we copy kazi ya mtu kama ilivyo hata kama ni aya moja halafu usitoe credit sawasawa. Moto utakaokuwakia aisee hutakaa uamini.
nashukuru mkuu kwa kunielewa.
 
Hiyo Ndege ilipotelea nje ya Dunia.

Mi huwa siamini kwamba, Dunia ni duara ila naamini dunia ni flat.

Na hii ndege, nadhani haina kifaa chochote kilichoonekana popote, bali wale waliotangaza hivo nao walikuwa wanawatumainisha ndugu wa abiria waliokuwemo kwenye ndege husika tu. kwa sababu haiwezekani kiokotwe kifaa mahala eti ndege isionekane kabisa kwa teknolojia zilipofikia!

Mimi naamini Dunia ni flat, na ina ukingo, (Mwisho wa dunia)
kwa hiyo ndege ile ilipopotea iliupita ukingo na hivo kwenda mwisho wa Dunia.
Kama hamuamini shuri zenu!!
 
HII NI MARA YA PILI SASA UNAKOPI POSTI KUTOKA KWENYE BLOGI YANGU, "salim msangi" na kuviweka huku kwenye JAMII FORUM KAMA VILE WEWE NDIYE ORIGINATOR WA THEMES/TOPIC/POST.
TAFADHALIA ZINGATIA SHERIA YA MITANDAO NA SHERIA YA HABARI. TAFADHALI KABLA YA KUFANYA TENA HIVYO AU KUEDNELEA KUKOPI NA KUPOSTI KUTOKA KWENYE BLOGI NILIYOITAJA HAPO JUU, WASILIANA NA MIMI KWA NJIA YEYOTE ILE INAYOWEZEKANA, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE.
KENGO LA KUFANYA HIVI NI KUILINDA KAZI YANGU. WADAU WAMEULIZA MASWALI NA WAMECRITISIZE ULICHOKIPOSTI HAPA LAKINI SI DHANI KAMA UTAWEZA KUYAJIBU AU KUWAELEWESHA, SABABU WEWE SIYO ORIGINATOR WA MADA HUSIKA, TAFADHALI, WASILIANA NA MIMI KABLA YA KUENDELEA NA UTARATIBU HUU.
Ila sio mbaya maana nisingeijua blog yako kama sio wewe kucomment katika hiyo post ya Hugo jamaa,samehe bure hiyo mutu
 
Back
Top Bottom