Wapenzi wengi wa Bob Marley wanavuta bangi?

Sio kweli mkuu, Mimi nazipenda sana nyimbo zake, lakini sijawahi kuona live mmea wa bangi au hata msokoto wa bangi zaidi ya kuona mimea ya bangi iking'olewa na askari kule tarime kwenye tv.
 
Jamani ni udadisi tu wa hapa na napale, nikagundua kwamba ukiona mtu yeyote;
Mkeo, mchumba wako, rafiki yako, baba yako, mama yako, mwanao,mjomba yako rafiki yako n.k anamzimikia sana bob, sana yaani ile mbaya....kila wakati yeye bob bwana, bob......
Ujue huyo anavuta bangi au aliwahi kuvuta bangi.....
Mnasemaje kuhusu hili?

Wewe unazipenda nyimbo za bob? If not why?
 
ndugu yangu mzizi, sikiliza nyimbo za Bob kama "war, real situation, rat race, babylon system, redemption song, survial, Zimbabwe, Judge not, Africa unite na nyingine nyingi itaweza kukusaidia kung'amua why watu makini wa leo still wanapenda kusikilizia reggae music na hasa za Robert Nesta Marley (Bob) na si suala la kuvuta marijuana. There is a message in Bob's music most of which is still applicable/tangible even today though aliimba years ago.
 
What do you know about Marley, what do you know about Reggae, what do you know about Rastafarian you Babylonian!
 
Bob marley alikuwa mvuta bangi kati ya wavuta bangi,,,,,,upenzi wa watu kwa bob ni kutokana na nyimbo zake za mapinduzi na kukomboa watu kutoka katika mifumo ya kitumwa.....kama mtu ana mapenzi na bob na anavuta bangi sawa anafuata life style ambayo bob alikuwa anafanya,,,,,,na ambaye havuti na ni mpenzi wa bob nadhani huyu anaufahamu mkubwa wa nyimbo za bob..............binadamu kama binadamu hawezi kuwa perfect 100%
 
bob marley alikuwa mvuta bangi kati ya wavuta bangi,,,,,,upenzi wa watu kwa bob ni kutokana na nyimbo zake za mapinduzi na kukomboa watu kutoka katika mifumo ya kitumwa.....kama mtu ana mapenzi na bob na anavuta bangi sawa anafuata life style ambayo bob alikuwa anafanya,,,,,,na ambaye havuti na ni mpenzi wa bob nadhani huyu anaufahamu mkubwa wa nyimbo za bob..............binadamu kama binadamu hawezi kuwa perfect 100%

kuacha vipite sio kushindwa wakati mwingine ni ujasiri wa kukubali
 
Kwanza bange ina tatizo gani? Majuzikati nimeangalia documentary moja wanasema hakuna kazi za kitabibu kuthibitisha madhara ya bange. No kiddin. Anyways inaeza ikakudhuru kama ukila mjani kwa spidi ya 120, ukila kwa spidi ya wastani ni pouwa tu tena nchi nyingine wameshastukia uhondo wanaoukosa kwene mjani na kuanza kuruhusu matumizi yake kwa maeneo flaniflani. Watabibu wengine wanatumia mjani kwa wagonjwa wenye maradhi yanayoambatana na maumivu makali. Lakini unaeza kudhuru afya yako kwa vitu ambavo wengi wetu tunavisujudu kama pombe,machipsi, makuku, pizza, samaki, matunda hata mbogamboga. Kwa hiyo bana anayetaka kula mjani aendelee tu kubanjuka cha msingi azingatie dozi isizidi..:pound:
 
jamani nyie mbona mie nampenda Bob Marley lakini sijawahi hata kuwa na wazo la bangi:biggrin1:

Kweli umetuvunjia heshima "Bad Card"
 
ukweli ni kwamba washabiki wengi wa bob marley ambao ni vijana wa mtaani ndio wanaovuta bangi, lakini si mashabiki wote au wengi wa bob marley wanavuta bangi, if u can differentiate bro.
 
Jamani ni udadisi tu wa hapa na napale, nikagundua kwamba ukiona mtu yeyote;
Mkeo, mchumba wako, rafiki yako, baba yako, mama yako, mwanao,mjomba yako rafiki yako n.k anamzimikia sana bob, sana yaani ile mbaya....kila wakati yeye bob bwana, bob......
Ujue huyo anavuta bangi au aliwahi kuvuta bangi.....
Mnasemaje kuhusu hili?

Wadau wengi wengi wamechangia vema,kijana mtoa thread nafikiri amekurupuka tu,anapaswa kueleweshwa tu!

Bw Mzizi wa Mbuyu - unapaswa kufahamu ya kwamba tulio wengi tunaomkubali Robert Nesta Marley "Bob Marley" ni kwa sababu kubwa mbili;ya kwanza ni ujumbe ambao unapatikana kwenye nyimbo zake nyingi kuzitaja chache tu ni kama vile "War" Rat Race" "Real situation" "Africa Unite" n.k...Lakini sababu ya pili ni msimamo wake juu ya mambo mbalimbali ya kisiasa...Alikuwa anavuta bangi,anafata imani ya Rastafarian nk hayo yalikuwa ya kwake kama walivyo binadamu wote wengi hayo hayatuhusu...Kwa hiyo kama waliotangulia walivyosema si kweli kwamba wanaomzimikia Bob walivuta/wanavuta bangi.
 
Nashukuru kwa mlionielewa.
Lakini wengine naona inakuwa vigumu mno kunielewa...sijasema nyimbo za bob siyo nzuri wala sijasema wapenzi wa bob woote wanavuta bange....
Lakini jiulize na jitazame ukiwa huru kwelikweli, wale wanaomfeel mno bob! yaani wao wakisikia mziki wanatamani uwe wa bob, wamebandika mapicha ya bob (tena akivuta bange) sehemu mbalimbali iwe ukutani kwenye magari n.k, wanatoa nukuu mbalimbali za bob kila mara, wanahudhuria matamasha ya Bob kila mara(amabako bangi huvutwa kwa saaana! kama unabisha nenda la mwaka huu!) n.k.....
Hao lazima wamewahi au wanavuta bange...
Na hii ni tabia ambayo inawafanya hata watu wengine wenye heshima zao kuugopa hata kuusiliza muziki wa bob tofauti na wanamziki wengine kwani wataonekana nao wavuta bange!!
 
Quotes_Creator_20190116_192128~2.jpeg
 
Back
Top Bottom