Namna ya kupika sotojo la mchemsho wa ndizi nyama

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Naendeleza somo langu la mbinu za mapishi na masotojo ya kijanja. Nimegundua jamii ya watanzania wapo nyuma sana kwenye mapishi.

Last time nilikuja na kigongo cho rosti la kitimoto Mbinu za kupika sotojo / rosti la kitimoto, unaweza kula mpaka ujiume ulimi... Enjoy

Leo nakuja na sotojo la mchemsho wa ndizi mshare na nyama ya kidari cha ng'ombe.

Nimesisitiza kidari kwasababu nimegundua pia watu wengi hawajui hii sanaa ya kuchagua nyama. Sio kila nyama ya ng'ombe inafaa kupika mchemsho wa ndizi mshare. Na hapa ndipo watu wengi hufeli.

Unakuta mtu anaenda buchani kwa kutokujua unakuta anakatiwa li mnofu la nyama ya paja la ng'ombe anafurahia amependelewa na muuza bucha wakati amepewa linyama la hovyo lisilokuwa na ladha.

Sasa sikia unyama hapa chini

1. Nenda buchani mwambie akukatie 'kidari cha ng'ombe' au mbavu pia sio mbaya sana au mkono wa mbele sehemu ya juu huku. Hizo nyama ni tamu sana

2. Kama kawaida, katakata nyama tia kwenye sufuria. Osha mara moja, weka maji kidogo sana, tia na chumvi halafu anza kuichemsha.

3. Utaendelea kuongeza maji walau dakika 45 zipite. Kwa nature ya hizi nyama baada ya dakika 45 zinakuwaga zimeiva kabisa na zimelainika vizuri.

4. Menya ndizi zako za mshare na uzioshe mara moja kisha uweke kwenye nyama ambayo inachemka, ila unaweza kupunguza jiko kidogo.

5. Ukishaweka ndizi, anza kukatia katia hoho, karoti, nyanya, kitunguu, na pili pili kulingana na ukali unaoupenda.

6. Baada ya hapo unafunikia mchemsho wako na kuacha uendelee kuchemka. (Kama maji ni mengi kwenye sufuria unaweza ukapunguza kidogo ili uje kuyarudishia baadae)

7. Ndizi mshare haihitaji maji mengi wakati wa kuchemka kwahiyo unaweza kuchemsha maji pembeni ili yawe yamoto kwa ajili ya kuongezea baadae kwenye mchemsho ili upate mchuzi.

8. Baada ya kama dakika 10 mpaka 12 ndizi mshare itakuwa imeanza kulainika, unaweza kuongeza maji ya moto ili sasa ichemke vizuri.

** Usiweke mafuta kabisa maana zile nyama zina mafuta ya kutosha

9. Baada ya dakika zingine 10 unaweza kuepua mchemsho wako utakuwa tayari.

Huu mchemsho unaenda vizuri na kipande cha parachichi.

Karibuni....
20231101_224103.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom