Mbinu za kupika sotojo / rosti la kitimoto, unaweza kula mpaka ujiume ulimi... Enjoy

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Habari wakuu, kwa wale wadau wa hii nyama yetu pendwa, ngoja leo nikupe mbinu.

1. Nunua nyama yako, ni vizuri kama atakukatia katia pale.

2. Weka nyama kwenye sufuria, weka na maji, halafu anza kuisuuza ili uondoe vile vimifupa vidogo vidogo.

3. Weka nyama kwenye sufuria safi, kisha kamulia limao, tia na chumvi halafu uichanganye.

4. Washa jiko lako la gesi uibanike ukiwa umeifunikia. (Usiweke maji kwanza)

5. Itachemka kwa kujichuja maji yenyewe. Kama haina mafuta sana yale maji ya kwanza yakikauka hapo unaweza sasa kuweka maji mengine na uiache walau kwa dakika 60..... kama ina mafuta sana, mimi huwa nachofanya siongezi maji bali naacha mpaka zile nyama za mafuta zinajichuja mafuta na kuanza kujikaanga... hapo sasa ni kukoroga ili isishike chini, ikianza kubadili rangi... ondoa kipande kimoja kimoja uweke pembeni...

6. Chukua sufuria mpya kaanga kitunguu, kikiva kidogo weka karoti, hoho kwa pamoja na uweka na pili pili ambayo umeikatia katia vipande vidogo vidogo...

7. Baada ya hapo, weka ile nyama kwenye mchanganyiko wa karoti na hoho halafu uikorogo mpaka ichanganyika vya kutosha.

8. Ikishachanganyikana, weka nyanya ili kutengeneza mchuzi.

9. Endelea kuchanganya, usifunikie kwa sababu haina maji itashika kwenye sufuria, wewe koroga tu vya kutosha.

10. Mchanganyiko ukikolea, sasa weka maji kidogo sana na ukoroge, ukiona mchuzi kidogo unejitengeneza, basi waweza funikia kwa dakika moja au moja na nusu...

11. Kisha funua na endelea kukoroga kwa dakika kama tatu zingine, na chakula chako kitakuwa tayari.

12. Huwa inapendeza kama utakula na ugali, ndizi za kukaanga, au Chipsi yote inaenda vizuri sana. Pembeni ukiwa na parachichi itapendeza zaidi.
20230924_173746.jpg
 
Habari wakuu, kwa wale wadau wa hii nyama yetu pendwa, ngoja leo nikupe mbinu.

1. Nunua nyama yako, ni vizuri kama atakukatia katia pale.

2. Weka nyama kwenye sufuria, weka na maji, halafu anza kuisuuza ili uondoe vile vimifupa vidogo vidogo.

3. Weka nyama kwenye sufuria safi, kisha kamulia limao, tia na chumvi halafu uichanganye.

4. Washa jiko lako la gesi uibanike ukiwa umeifunikia. (Usiweke maji kwanza)

5. Itachemka kwa kujichuja maji yenyewe. Kama haina mafuta sana yale maji ya kwanza yakikauka hapo unaweza sasa kuweka maji mengine na uiache walau kwa dakika 25..... kama ina mafuta sana, mimi huwa nachofanya siongezi maji bali naacha mpaka zile nyama za mafuta zinajichuja mafuta na kuanza kujikaanga... hapo sasa ni kukoroga ili isishike chini, ikianza kubadili rangi... ondoa kipande kimoja kimoja uweke pembeni...

6. Chukua sufuria mpya kaanga kitunguu, kikiva kidogo weka karoti, hoho kwa pamoja na uweka na pili pili ambayo umeikatia katia vipande vidogo vidogo...

7. Baada ya hapo, weka ile nyama kwenye mchanganyiko wa karoti na hoho halafu uikorogo mpaka ichanganyika vya kutosha.

8. Ikishachanganyikana, weka nyanya ili kutengeneza mchuzi.

9. Endelea kuchanganya, usifunikie kwa sababu haina maji itashika kwenye sufuria, wewe koroga tu vya kutosha.

10. Mchanganyiko ukikolea, sasa weka maji kidogo sana na ukoroge, ukiona mchuzi kidogo unejitengeneza, basi waweza funikia kwa dakika moja au moja na nusu...

11. Kisha funua na endelea kukoroga kwa dakika kama tatu zingine, na chakula chako kitakuwa tayari.

12. Huwa inapendeza kama utakula na ugali, ndizi za kukaanza, au Chipsi yote inaenda vizuri sana. Pembeni ukiwa na parachichi itapendeza zaidi.View attachment 2752470
Eeka mushi
 
Back
Top Bottom