Tumezoea kusikia tu mawaziri mizigo, msemo ulioasisiwa na kada maaarufu na katibu mkuu wa ccm mzee Kinana, baada ya kuona utendaji wa mawaziri hao hauna tija na ni mzigo kwa Taifa, hii ni siasa,
Sasa unajua kuna wapenzi mizigo, waume mizigo, wake mizigo, marafiki mizigo ?
Awe yeyote kati ya hao hapo juu bila kujali jinsia, yeye kazi yake ni kupokea na kutumia tu, kutafuta aah ah sio kazi yake almradi ameoa au ameolewa basi mambo mengine yoote kasoro kutumia hayamhusu.
Kama ni mwanaume pesa yake ni yake, lakini ya mkewe ndio ya kufanyia kila kitu kuanzia ada za watoto, kodi chakula nk,
Kama ni mwanamke pesa yake ni ya vipodozi, mavazi na mapambo yake. lakini matumizi ya hm na mengine yooote ni jukumu la baba
Kama ni rafiki anakutafuta anapokuwa mhitaji, kama hana shida chake ni chake,
Wengine hawataki maendeleo, wanataka kila kinachopatikana kiliwe kiishe, na kutumia kwenye starehe,
wengine hawapendi wapenzi wao wavae wapendeze kisa watapendwa au watatongozwa.
Hawa wote ni mizigo,。。。
Tunapoijadili mizigo ya ccm nasi tujipime tusijekuwa nasi ni mizigo kwenye kampani na familia zetu.