Katika Biblia hakuna mahali pamezuiliwa mtu kwenda Hospitali ila ikiwa mtu ana imani yake ya kupona bila kwenda Hospitali ni sawa kwani hakuna jambo lisilowezekana kwake aaminiye. Pia ikumbukwe kuwa kiwango cha imani hutofautiana kutoka mtu hadi mtu kwahiyo mwenye kuamini kutokwenda hospitali asimlazimishe mwenye imani ndogo kufanya hivyo kwani kama mtu ana mashaka moyoni mwake hata maombi yake ni bure. Kuhusu kuhamia porini na kusubiri kunyakuliwa hapa panaleta utata kidogo kwani Biblia inatuambia hakuna ajuaye siku wala saa atakayokuja BWANA YESU kwa mara ya pili kulichukua kanisa lake. Kwahiyo nashawishika kusema kuwa hii dini inaweza ikawa ni dizaini ya akina Kibwetere in the name of Pentekoste kwani Wapentekoste ni watu wenye ufahamu wa hali ya juu katika masuala ya MUNGU kutokana na uongozi wa ROHO Mtakatifu katika maisha yao
umeongea vyema sana. nakuunga mkono kabisa. wapentecost ni watu wanaomjua Mungu kwa ukweli kabisa. mimi ninatoka makanisa ya pentecost...yaani makanisa ya kilokole yanayoamini ujazo wa Roho Mtakatifu kuwa ni wa lazima kwake yeye aaminiye. makanisa haya ni mengi sana, na yote yanajumuishwa kuwa ni ya wapentecost.
cha kufahamu ni kwamba, inawezekana, wakati mwingine, kukawa na mtu anayeleta imani fulani ambayo haina uongozi wowote wa Roho Mtakatifu, akaita mlokole na watu wakamdefine kuwa ni mpentecost...akachafua wapentecost wote. cha kuelewa ni kwamba, KITU CHOCHOTE AMBACHO HAKINA UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU, HAKIKA YAKE NI UHARIBIFU TU. kwenu nyie mnaomjua Mungu, kama kitu haujaongozwa na Roho Mtakatifu,umeongozwa ether na chuki yako, elimu ya kidunia, ufahamu na hekima za kidunia, doctrine ambayo haikuanzia kwa Roho mtakatifu etc, hakika yake, mwisho wake ni aibu tu na huwa haufanikiwi..kwasababu kila jambo linalofanyika kimwili hilo ni la uharibifu. NDIO MAANA NI MUHIMU KUJAZWA NA KUISHI NA ROHO MT. ili akuongoze, na chochote atakachokuambia Roho, hakika yake hata kama unaona kama utapitia hatari fulani, mwisho wake ni mwema. ndio maana mimi nilisema, inawezekana kuwa, hao watu ni wa Mungu na inawezekana kuwa ni hekima ya kibinadamu tu au mchomeko wa shetani tu anayevaa sura ya malaika wa nuru....HIVYO, KAMA NI JAMBO LA KIMUNGU, LITASIMAMA, KAMA SI LA KIMUNGU, LITAISHIA KAMA WALE WASABATO MASALIA. pamoja na kwamba mimi hapo siungi mkono kabisa.
Shetani baada ya kuona watu wanaokoka na kuzijua nguvu za Mungu, anatumia mawakala wake wengi tu siku hizi ili waingie kama malaika wa nuru, kusudi walete picha chafu kwa watu wanaotaka kumpokea Mungu..ili shetani aendelee kuwa na kundi kubwa la watu wanaoelekea motoni....hivyo kila kitu lazima kipimwe kwa Neno la Mungu, na kwa Roho Mtakatifu.