mkuu, ili elimu iwe bora ni lazima mfumo mzima wa elimu uhusike.
aidha, ubora wa elimu haupimwi kwa ufaulu wa mitihan tu (kama ambavyo wanasiasa vilaza hujitapa wanapoona ufaulu umeongezeka) bali huangalia uwezo wa mhitimu kutumia elimu yake ktk mazingira yake
mwanafunzi hawezi kufanya vizuri kwenye mitihani ktk mazingira ambamo:
1. mwalimu hana uhakika wa kupata mahitaji yake muhimu mfano chakula na malazi
2. mwalimu hana vitendea kazi
3. mwalimu hana amani moyoni kwani haoni kuthaminiwa na mwajiri wake. anafanyafanya tu bora siku ipite.
4. shule haina walimu wa kutosha kiasi cha kufanya mwalimu mmoja afundishe masomo hata yale asiyosomea
5. mwanafunzi nyumbani hapati chakula cha kutosha/uhakika kiasi cha kulala/kusinda njaa. hali hii hupunguza umakini wa kufikiri
6. mwanafunzi anaishi mazingira hasimu kwa elimu mfano, nyumbani wanafanya biashara na akirudi anatakiwa kuwapokea, au wazazi/walezi hugombana kila siku.
7. mwanafunzi hana vitabu vya kujifunzia, hakuna maabara
8.
9.
10.
mambo ni mengi sana.
waliofaulu kwa kiwango cha chini kabisa tuwafariji waone kwamba wanayo nafasi ya kusonga mbele na maisha.
kuna jamaa anaitwa Stanley nilisoma nae std 1.
darasani ilikuwa shughuli
MWALIMU: "Stanley sema 'AAA' "
STANLEY: (Kwa kibezi)"Stanley sema 'AAA' "
MWALIMU: Nimesema useme 'AAA' "
STANLEY: (kwa kibezi)Nimesema useme 'AAA' "
MWALIMU: "AAA"
STANLEY: "AAA"
shule akaachishwa std 2. sasa hivi ana maisha mazuri huwezi kuamini.
watoto wengine akili zao hazipeki elimu ya darasani lkn zinacharge kwenye mambo mengine.
tujitahidi kuwasoma na kuwasikiliza wanachodhani wanaweza kufanya then tuwashauri. tuache kuwaamulia kila kitu na wanaposhindwa tunaanza kuwatukana kuwasimbua na kuwasimanga.