Da mpiga penalti anapanuliwa goli na bado anashindwa kufunga (BRN) ,ntampa moyo yule aliyekuwa shule za kata vijijini.
Jibu ni rahisi tu mkuu kwa maswali yako hayo...
Mfumo mzima wa elimu haujakaa sawa si wakati huu au wakati uliopita.
Hata kina sisi tuliomaliza miaka ya nyuma sio kwamba hakukuwa na vikwazo au tulifaulu kwa sababu mfumo mzima ulikuwa mzuri.
Ili mwanafunzi afaulu kunahitajika mambo kadhaa:
1. Mfumo mzuri wa kielimu.
2. Juhudi na maarifa binafsi
3. External support
umenena vyema, yapo meng yanayochangia, serikali ina sehemu yake, wazaz nao na pia mtoto mwenywe, cha muhimu wajue tu kufeli mtihani siyo kufeli maisha wanahitaji kugeukia upande mwngne zaid pia tuwasaidie kuwapa elimu ya kijikomboa itakayomsaidia atakapomaliza siyo anaanza kusaka ajira bali anatakiwa ajiari mwenyewe ili na yy siku moja awaajir na wengine. Ila jana uliniudhi kidogo kuna uzi mmoja ulichangia halafu ukaonesha matokeo yalikuwa ni ya wanawake halafu ukasema eti ndo unaniambia nioe hapa, ulikosea sana kwani ufaulu wa mtu hauusian na mambo ya ndoa,mtu anaweza kuwa alipata div one lkn kny ndoa akawa ni bogas kabisa, please rekebisha kauli yako ya jana na uwatake radhi wanawake wote kwa niaba yao.
kufeli shule sio kufeli maisha, mmesikia wadogo zangu? kuteleza pia sio kuanguka. ni hayo tu kwa leo.
Kuna mmoja nimeona kajichoma kisu. Waambieni watoto/wadogo/ndugu zenu hiyo ni pancha tu, safari bado inaendelea.
Ila kwenye swala la lawama nadhani zinategemea mtoto na mtoto. Wapo waliofeli kwa kutozingatia masomo, waliofeli kwa kukosa waalimu wazuri/wakutosha, kwa kukosa vifaa, kwakukosa muda wa kusoma kwasababu ya majukumu ya nyumbani n.k
Kwahiyo wapo wazazi, watoto, waalimu na viongozi wa kulaumiwa kila mmoja kwa nafasi yake.
Tusiilaumu sana serikali hata mtoto yenyewe ni ngumbalu hamna kitu kichwan. Nina mdogo wangu nilimpeleka shule nzuri sana ya private ambayo matokeo yake ni mazur kwasababu kuna div 1 mpaka 3 na four ni kumi na hakuna zero. Lakin limekuwa miongon mwa waliopata div4 tena mbaya pamoja na kumpa mazingira mazur ya usomaji. Sina hata hamu ya kumpeleka popote zaidi ya kuwa mnyampala shamban
48 ni zero eti Excel??
mkuu, ni kweli kwamba kufeli mtihani si kufeli maisha, lakini hii kauli nayo ina walakini.. kumbuka nmithali 4.13 iasema mshikeni sana elimu, usimwache aende zake, maana huyo ndiye mkombozi wako.
that means, bila elimu, mambo mengine hayatoenda vizuri. pia, hali ya ufeli inazidi kuwa mbaya kila kukicha, kila mwaka mambo ni mpwito mpwito katika taifa hili la TANZANIA. kwanin sisi lakini? wana-east africa wenzetu wanafanya nini?
Mtoto akinyea mkono utaukata? Jitahidi tu umpe elimu itakuja kumsaidia uko mbeleni hata kama ana kichwa kigumu sukumaneni hvyohvyo mpaka afike anapostahili....vinginevyo atakuwa mzigo wako wa kudumu....Tusiilaumu sana serikali hata mtoto yenyewe ni ngumbalu hamna kitu kichwan. Nina mdogo wangu nilimpeleka shule nzuri sana ya private ambayo matokeo yake ni mazur kwasababu kuna div 1 mpaka 3 na four ni kumi na hakuna zero. Lakin limekuwa miongon mwa waliopata div4 tena mbaya pamoja na kumpa mazingira mazur ya usomaji. Sina hata hamu ya kumpeleka popote zaidi ya kuwa mnyampala shamban
huyo ni mmoja kati ya ndugu zangu wa pekee niliyempa tumaini langu kwa asilimia 100 kwamba atafaulu.
mwisho wa siku yamemfika.. sina namna, siwezi kupindua matokeo.
i've just decided to let it go as it wasnt meant to be hers.
Simu na mitandao ya kijamii imeharibu sana watoto....yani utamkuta mtoto yuko kwenye mitandao ya kijamii karibia 10.......unategemea shule atamudu vizuri...?wazazi kujifanya wako busy na kutojali maendeleo ya mtoto shuleni...wazazi wengine wanajua wajibu wao ni kulipa ada tu ila kufwatilia maendeleo ya mtoto ni jukumu la mwalimu.....huyu mwalimu atafwatilia watoto wangapi na ukizingatia yey mwenyewe ana familia na watoto wa kuwafwatilia....Serikali nayo iko hovyo sana na mfumo wao wa elimu...ndo mana Dr. Ndalichako kajiondoa mana huu uozo uliopo hawezi kuuvumilia...
huwezi.... she is too serious to be with you...
mkuu, ni kweli kwamba kufeli mtihani si kufeli maisha, lakini hii kauli nayo ina walakini.. kumbuka mithali 4.13 inasema mshikeni sana elimu, usimwache aende zake, maana huyo ndiye mkombozi wako.
that means, bila elimu, mambo mengine hayatoenda vizuri. pia, hali ya ufeli inazidi kuwa mbaya kila kukicha, kila mwaka mambo ni mpwito mpwito katika taifa hili la TANZANIA. kwanin sisi lakini? wana-east africa wenzetu wanafanya nini?
Naweza bhana!
Angekua too serious angepata matokeo hayo?
Nami nisingekuwa serious ningekuepo hapa nilipo?
Kuna mda wa utani na kuna mda wa kufanya kweli!!!!
...
Embu rudia andiko hapo chini (underline):
Umeona hapo?
Nipe nimuendeleze bhana!
mwekundu Pita huku Excel hataki mdogo wake apasishwe ati!!!!