Pole sana mkuu,naelewa sana jinsi unavyo jisikia sababu na mimi nilikuwa kwenye hiyo position miaka kadhaa iliyopita,alikuwa mdogo wangu wa tumbo moja na wa mwisho kuzaliwa.Iliniuma sana.
Hili swala kila pande zina lawama kulingana na mazingira.Mzazi asiye na uwezo anaweza kujitahidi akamfuatilia mtoto lakini mtoto akafeli sababu ya kusoma shule isiyo na walimu.Mwingine anaweza kupelekwa shule nzuri na wazazi wanampa support bado akafeli pia.
This issue is a matrix of various factors.Lakini yote kwa yote wa kulaumiwa ni mzazi kwa kiasi kikubwa hasa kwa wale wanafunzi wa shule za milioni,wazazi wamekuwa busy kulipa ada ila ufuatiliaji hakuna na malezi kwa ujumla ni F.wazazi wangapi wamewawekea ratiba watoto wao toka wakiwa chekechea? Watoto wetu wanaishi bila ratiba na wanaishia kufanya mambo ambayo hayawajengi kiupeo wa kufikiri.Wazazi wangapi wanapata muda wa kujifunza namna ya kumjengea mtoto uwezo wa kujiamini na kutafakari mambo? Haya mambo huanza kujengwa utotoni wakuu.
Tafuteni movie inaitwa THE GIFTED HANDS OF BEN CARSON,hapo ndio mtaelewa umuhimu wa mzazi kumuwekea mtoto ratiba katika kujenga upeo wa mtoto
Angalizo:
Naomba tusiwalizimishe watoto au ndugu zetu waliofanya vibaya wafanye vile ambavyo sisi tunaona.Japo wamefanya vibaya lakini wanajua nini wanataka na wanapenda hvyo waulizeni what do they want to do next.My young sister tulimlazimsha arudie mtihani matokeo yake alifeli tena,but tulipomuuliza anataka nini alituambia and now she is taking a bachelor degree in mass communication baada ya kusoma foundation course then cheti then akaenda diploma baadae bachelor