Wapeni haki yao...!

Wa mmoja

Member
Aug 4, 2009
99
0
Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema endapo klabu za simba na yanga zitasusia kucheza ligi kuu Tanzania Bara zitashuka daraja.
Timu hizo zimetishia kugoma baada ya kupewa kipato kidogo baada ya mchezo wa ngao ya jamii uliochezwa Agosti 18 katika uwanja wa Taifa DSM.
Zilipatikana milioni 222 lakini wao wanapewa milioni 33...
Hivi jamani hii ni haki kweli?!Wao ndio waliosababisha pesa hizo zipatikane halafu mnataka kuwabania!Pesa nyingine zinakwenda wapi?!
 
inawezekana kuna kiongozi anataka kugombea kupitia thithiem, anafanya maandalizi ya awali ya kulimbikiza pesa ili ahonge wapigakura wakati ukifika.
 
bora wagome, ufisadi hadi kwenye mapato ya mechi! na wakigoma tu ligi inapoteza mvuto kabisa
 
TFF ikizishusha daraja Yanga na Simba itabaki na soka gani? Haiwezi kuthubutu - kwani nayo itakuwa imeshuka daraja. Hilo sio jawabu la mgawo ulio dhahiri mbaya.
 
Kwa mgawanyo wa mapato ya aina hiyo unatakiwa uwaje? kama mgao haukufuata taratibu zilizopo (kama zipo) then kuna tatizo hapo, vinginevyo vilabu vinaweza kuwa vina chemka......!
 
Back
Top Bottom