Wapenda ugali mpo?

Wapenda ugali mpo?

Habari za J3 wapendwa

Mimi ninapenda sana kula ugali, ninaweza kula chakula hiki siku saba za juma mradi tu nibadilishe kitweo. Kuna wanaume nikiwaeleza mapenzi yangu kwa ugali wananiona mlugaluga.

Imebidi nipunguze ulaji wa ugali kutokana na issue za uzito wa mwili. Siku hizi ninakula ugali Jumamosi tu. Kuna wanawake wanaopenda kula ugali kama mimi?

Wanaume pia mnakaribishwa
Ugali dona la moto (dona la home made-unanunua unga wa dona unachanganya na dagaa waliosagwa na unga wa muhogo) alafu na rosti ya dagaa na rosti ya matembele, aiseeee!
 
Ugali dona saiz ya ngumi yangu,pembeni nyama ya kukausha,mchicha/tembele,kachumberi iliokolea ndimu,mango chatne ama pilipili ya kupikwa,kipande cha tikiti na maji yenye ubaridi kwa mbaaali
Ugali na mchuzi wa samaki uliotiwa nazi, bamia, nyanya chungu nyanya kitunguu na ndimu
 
Habari za J3 wapendwa

Mimi ninapenda sana kula ugali, ninaweza kula chakula hiki siku saba za juma mradi tu nibadilishe kitweo. Kuna wanaume nikiwaeleza mapenzi yangu kwa ugali wananiona mlugaluga.

Imebidi nipunguze ulaji wa ugali kutokana na issue za uzito wa mwili. Siku hizi ninakula ugali Jumamosi tu. Kuna wanawake wanaopenda kula ugali kama mimi?

Wanaume pia mnakaribishwa

uko vizuri
 
Ugali dona la moto (dona la home made-unanunua unga wa dona unachanganya na dagaa waliosagwa na unga wa ulezi) alafu na rosti ya dagaa na rosti ya matembele, aiseeee!
Mkuu nitajaribu hii
 
Ugali na mchuzi wa samaki uliotiwa nazi, bamia, nyanya chungu nyanya kitunguu na ndimu
Ebanaee mate yashantoka,mchuzi wa samaki raha yake uliwe na ugali wa muhogo(udaga).afu chuzi liwe zitoo la sato au samaki asiye na mamifupa mengi
 
Ebanaee mate yashantoka,mchuzi wa samaki raha yake uliwe na ugali wa muhogo(udaga).afu chuzi liwe zitoo la sato au samaki asiye na mamifupa mengi
Yaani mku hili la ugali wa mhogo afadhali umelileta. Jaribu kutembea Dar uoe ni hoteli ngapi wanapika ugali wa mhogo. Watoto wa sikuhizi hata hawaufahamu. Tunapoteza asili yetu
 
Mkuu ninaishi Kwamtogole nimepanga chumba kimoja na kisebule. Ugali ninapenda unga wa Azam.
kwanini usisage mwenyewe?,
niliona mmoja anachanganya mahindi,mtama kiasi,mahindi ya bisi na ngano kisha ndo anaenda saga,ugali wake very rich in nutrition kwa vimbao mbao unafaa sana kunenepesha ila kwakuwa we tayari mnene kiasi labda huo plain unakufaa.
 
Mimi pia napenda ugali hasa dona.... Mara nyingi mchana mida ya lunch apa offisini unakuta wanawake wanaagiza chips miiii naagiza ugali tena dona maybe nasamaki basi wanaishangaa wanaume walioko hapa ofsini huwa wanasema wewe ndo mwanamke kweli hujivungi cjui wali chipsi...... Ila kwakweli napenda ugali lkn siwezi kuula usiku maana naamka bado nimeshiba so ucku napenda vyakula laini lakini mchana ni nguna tuu
 
Mkuu nilipenda kufahamu kama kuna wengine wanaoonekana walugaluga kama mimi. My. Weekend was fantastic and now I'm back to normality.

hahahahaha mie na ugali kama mgonjwa na dawa naweza kula ugali mwaka mzima bila shida kabisa nabadili mboga.....naweza kula ugali kwa kachumbari kama nakula samaki vile......kuna mahindi ya njano hivi ugali wake balaa

Sky Eclat karibu ugali tembele na dagaa kidogo
 
Kuna ambao waliathiriwa na maisha ya boarding enzi za awamu ya kwanza. Ilikuwa dona maharage kwa kwenda mbele
 
Mimi naweza kula ugali mwaka mzima, wali, ndizi huwa naona kama sio chakula..

Naonaga kama ni vitafunwa kwenye breakfast na sio mlo kamili.

Bila kula ugali naona kama sijala chakula kabisa.
 
Back
Top Bottom