Wapelekeni wake zenu 'vacation' kuboresha penzi

Wapelekeni wake zenu 'vacation' kuboresha penzi

Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada inayosema, wapelekeni wake zenu vacation kuboresha penzi.

Mazingira ya aina moja huchosha hasa kwa wanandoa kwakuwa wanakuwa na mazoea na kuzoeana.

Hata chumba nacho cha wanandoa kinachosha pia maana kila mara mpo pale pale mnaingia na kutoka.

Mazoea katika mapenzi hasa kwa wanandoa yamekuwa ni moja ya kikwazo kikubwa sana kinachopelekea mapenzi kupungua kwa wenza.

Vacation inafaa sana hasa katika kuboresha na kuamsha mapenzi mpya.

Hivyo ni vyema wanaume wakatumia muda wao kwenda mbali na wenza wao kwa kwenda kufurahi na kubadili mazingira.

Hapa wanaume wafanye kulingana na mifuko yao, maana Kila mmoja anajua namna uwezo wake ulivyo.

Ni msimu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya ni wakati mzuri wa kujipa likizo na kujitoa mbali kidogo.
Ahsante kwa muongozo.

Ni wapi naweza kupata sehemu nzuri hapa Don ya kutulia na familia na kufurahia hii pumzi ya bure?
 
Asante [mention]Donatila [/mention]

Tuna vibukta (hotpants), lingerie na shanga ila hatupati uhuru wa kuvaa nyumbani maana kidogo mtoto kaingia ndani, mara kaota monster mara hivi mara vile.

Tupelekwe vacation kwakweli
 
Asante [mention]Donatila [/mention]

Tuna vibukta (hotpants), lingerie na shanga ila hatupati uhuru wa kuvaa nyumbani maana kidogo mtoto kaingia ndani, mara kaota monster mara hivi mara vile.

Tupelekwe vacation kwakweli
Ngoja tuanze kubebisha sasa [emoji1787][emoji1787]

Muda unaenda sana, kama hawaoni vile...
 
Me kuwa mtumwa wa mwanamke ndo siwezi kabisa, Yaani kila kitu wafanyiwe tu wao kufanyia wenzao hawawezi..... Kwendra Takataka🚮
 
Back
Top Bottom