Wanaume mliooa, hudumieni wake zenu msituletee usumbufu mtaani!

Wanaume mliooa, hudumieni wake zenu msituletee usumbufu mtaani!

Namshakende

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
860
Reaction score
2,256
Wanaume mlioamua kuoa, timizeni wajibu wenu. Msiwaache wake zenu wakizunguka huku na kule wakijileta kwa wanaume ambao hawana hata mpango wa kuoa. Sisi hatuna mazoea nao, lakini wao ndiyo wanajisogeza sogeza tu!

Kama uliamua kuoa kwa hiari yako, basi simama kwenye nafasi yako. Mpe mkeo muda, upendo na huduma anazostahili. Usimwache akatafute faraja nje ya ndoa, halafu baadae uanze kulaumu jamii.

Hakuna aliyekulazimisha kuoa. Kama ulikuwa na ujasiri wa kuingia kwenye ndoa, uwe na ujasiri pia wa kubeba majukumu yake.

Mnatuletea usumbufu bure. hatuna mazoea na wake zenu, lakini wao ndiyo wanajileta wenyewe. Timizeni wajibu wenu!
 
Hoja yako inaonekana kama inawapa wanaume ruhusa ya kuingia kwenye mahusiano na wake za watu, kisha kuwahusisha waume zao na lawama zote. Hilo si sahihi na linaweza kuwa hatari.


Ndiyo, mume ana wajibu wa kumpa mke wake upendo, muda, uangalizi na mahitaji mengine ndani ya ndoa. Lakini mke naye ana wajibu wa kuheshimu ndoa yake na kuweka mipaka. Kama kuna changamoto kwenye ndoa, suluhisho ni mazungumzo, ushauri au kuchukua hatua zinazofaa—si kujileta kwa mwanaume mwingine.


Pia, kusema “sisi hatuna mazoea nao, wao ndiyo wanajileta” si kinga. Mtu mzima ana uwezo wa kukataa, kuweka mipaka na kuheshimu ndoa ya mwingine. Kumkaribisha au kuendeleza mahusiano na mke wa mtu kunaweza kuleta migogoro, kuvunja familia na hata kuhatarisha usalama wa wahusika.


Kwa hiyo, tusihalalishe usaliti kwa kumlaumu upande mmoja. Ndoa ni wajibu wa watu wawili, na heshima ya ndoa ni jukumu la kila mtu.

NB; Mke WA mtu NI sumu NI hatari na kwako wewe mwenyewe
 
Ila jeiefu unaweza kuta mleta Uzi ni hanisi/demu, kaamua tu kutuharibia siku tuliooa......
fe39048c6ddaac57b0717bef8ef6fa8d.jpg
 
Hao wanaojileta kwako walianza kuomba omba tangu wanaishi kwa wazazi wao wakihudumiwa kila kitu.
Ni hulka Yao tuu usiwaone wanaume wenzieo ni mabwege. Subiri na wewe ukue unaweza ukapigwa tukio na mkeo na usiamini.

Nyie ndio dizaini ya wanaume unapigwa tukio huna kosa na bado utamuomba msamaa mkeo.
 
Back
Top Bottom