Waongoza utalii kulipa kiingilio maeneo yao ya kazi sio uungwana

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
352
547
WAONGOZA UTALII KULIPA KIINGILIO MAENEO YAO YA KAZI SIO UUNGWANA

Hawa Vijana walio na mapenzi mema na maliasili nanutalii 2akasomea na kuwa professional katika swala hili, kama kazi yao, wanaumizwa na kitendo cha kulipia Kiingilio kwenye maneo ya Hifadhi.

Ijapokuwa wana License ya utambuzi kuwa wao ni Waongoza utalii, na bado kulipa Kiingilio katika maeneo yao ya kazi haijakaa sawa.

Walimu na madaktari na wafanyakazi wengine Hawalipiswi pesa Kuingia kwenye maeneo yao ya kazi hivyo kwanini kwa hawa vijana wetu wa Utalii walipishwe ikiwa lile ni eneo lao la kazi..

Ifike pahala tuweke mazingira rafiki kwa wafanya kazi wetu ili kudumisha kujituma na watu kupenda fani zao.

Tanapa na Waziri wa Maliasili na Utalii Tunaomba muwaangalie Vijana Wetu hawa.
 
Hiyo si pesa ndogo tu hata laki na nusu haifiki
Je!
Daktari analipia leseni kufanya kazi yake?
Mwalimu analipia leseni kufanya kazi yake?
Mameneja wa hoteli wanalipia leseni kufanya kazi zao?

Guide's wanalipia leseni ya udereva,wanalipia leseni ya u-guide,wanatakiwa sasa kulipia Latra ilhali hawamiliki gari,wanalipishwa viingilio hifadhini ilhali ndio maeneo yao ya kazi, na bafo sasa wanatakiwa kulipia malazi kws $40@night!

Je! Umeliekewa hilo?
 
Hao wote uliowataja wanalipia leseni pia jaribu kuuliza vizuri
 
Back
Top Bottom