Waoaji wapo, tatizo wanawake mmezidi tamaa sana

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,203
Habari za wakati huu ndugu zangu..

Bila ya kupepesa pepesa macho naomba ni waambie dada zangu kwamba wanaume waoaji wapo wengi sana na wanajielewa tatizo nyie dada zetu tamaa nyingi sana mpaka unambadilisha mwanaume nia ya kua na wewe , yani unakuta ume mwelewa binti/ dada flani unaanza kumfatilia kimnya kimnya unaridhika nae, na baadae unaamua kumtokea kumwambia ukweli kuwa umemwelewa na unataka umweke ndani, shida inakuja pale tuu yani anaanza kuomba omba hela sana mpaka unajiuliza hivi huyu kabla sijamtokea alikua anaishije, unakutwa mwanamke bila aibu unaanza visingizio vingi mara mama anaumwa, mara baba anaumwa, mara sijui wewe unaumwa yani kila siku matatizo tuu , mara naomba hela ya kusuka, sijui mafuta ,nguo, viatu mara hela ya kula yani hamjielewi mnakatisha tamaa kwa kweli... Yani mpaka mwanaume unabaki unajiuliza huyu dada vipi na kabla ya mimi alikua anaishije..

Wanawake mbadilike kwa kweli,, waoaji tupo wengi sana na wenye nia njema tuu na nyie na tunawapenda sana kama tulivyo Amriwa kuwapenda tatizo mnatukatisha tamaaa mapema sana .

Hatukatai mtuombe hela , tunajua kuwahudumia ni jukumu letu na mwanaume kuoa ni kukubali majukumu tatizo hata bado sijakuweka ndani umeanza kulia shida kibao mara unaomba omba hela ..hebu dada zangu badilikeni acheni kujiaibisha bana na kujifungia wenyewe ridhiki za kuolewa muda mwingine mnapata mwanaume sahihi ila kutokana na ulimbukeni mnapoteza bahati na kubaki kupiga kelele waoaji hamna.
 
Hivi ni kweli wanawake wanaomba pesa kiasi hicho kweli..??
Mbona ni kama mnalikuza hili suala kuliko ukhalisia wenyewe..??

Hivyo hapa JF kila mwanaume anaombwa pesa na wanawake tofauti tofauti kila siku...?

Hebu tuoeni bhana, Acheni visingizio..!
 
Hivi ni kweli wanawake wanaomba pesa kiasi hicho kweli..??
Mbona ni kama mnalikuza hili suala kuliko ukhalisia wenyewe..??

Hivyo hapa JF kila mwanaume anaombwa pesa na wanawake tofauti tofauti kila siku...?

Hebu tuoeni bhana, Acheni visingizio..!
Kuna mwingine nae analalamika wanaume/vijana wanaomba hela..
Basi hii vita nadhani ni humu jf tu..
Mbona mtaani watu wanaoa kila week jamani.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom