Zanzibar: Naibu Waziri wa Vijana, Hassan Khamis: Wanaofanya kazi kwenye Mahotel Zanzibar siyo wazawa inabidi tufanye Mapinduzi

Zanzibar: Naibu Waziri wa Vijana, Hassan Khamis: Wanaofanya kazi kwenye Mahotel Zanzibar siyo wazawa inabidi tufanye Mapinduzi

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
896
Reaction score
3,060
Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji, Zanzibar Hassan Khamis Hafidh, akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Vijana katika Baraza la Wawakilishi Juni 6, 2026, alisema licha ya kuwepo kwa hoteli 1,184 zilizosajiliwa Zanzibar, idadi kubwa ya wafanyakazi katika baadhi ya hoteli hizo si wazawa inabidi tufanye Mapinduzi.

"Kuna registered hotel 1,184. Hoteli zilizokuwa registered zipo. Na ukienda kweli, mheshimiwa Spika, wanaofanya kazi wengi katika mahoteli yale si wazawa kweli. Ipo kweli na hakuna ubishi.

Sasa jukumu letu sisi, wizara ya vijana na nini, ni kufanya mapinduzi ya kwamba sasa, kwamba wanaokuwemo miongoni mwa wale wasio wazawa, sasa wawe wazawa. Niachie mimi hiyo kazi, na iwezekane, hata ukwaju wako tu mchanganyiko tutautumia, watakuwemo tu.

Jukumu la wizara ya vijana ni kuhakikisha wazawa wanapata kazi katika miradi yetu. Nitakupa mfano, mheshimiwa Spika, sitataja hoteli kwa sababu ya... something. Kuna hoteli moja juzi niliitembelea, ina wafanyakazi 156. To be honest with you, vijana wetu wa Kizanzibari walikuwa 27.

Yes! Sasa hapo kuna mapinduzi? Hiyo ndio kazi nimepewa mimi na Rais, kuhakikisha sasa... watoto 27 ndio wawe wageni, na waliobakia wote wawe wenyeji! Taswira hiyo. Kwa hiyo nakushukuru, namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Mimi najua kazi yangu, Osha anajua kazi yake, Mussa Lema anajua kazi yake. Tuaminini, tupitisheni pesa mrembo leo, muone kazi hii tunavyokwenda kuifanya. Hilo ndilo jukumu letu tulilopewa na Rais, na kiapo hapa tumekula: kuwatafutia vijana

Pia soma: Kupitia maono ya Rais Samia kuwabeba Wakandarasi wazawa nayaona Mapinduzi ya Uchumi ya Tanzania kupitia sekta ya ujenzi

 
Kuna registered hotel 1,184. Hoteli zilizokuwa registered zipo. Na ukienda kweli, mheshimiwa Spika, wanaofanya kazi wengi katika mahoteli yale si wazawa kweli. Ipo kweli na hakuna ubishi.


Moja la Kwanza ni kukosa ujuzi kwenye kazi za uongozi utakuta ni wakenya na wageni wengine, na pia zile za Kati nazo wazanzibar wengi Hawana ujuzi nazo, hivyo utakuta ni wabara na kwa kazi za ngazi ya chini wazanzibar ni wavivu, na hivyo utakuta hizo KAZI zinachukuliwa na watu wa bara
 
Back
Top Bottom