Ziroseventytwo
Platinum Member
- Mar 27, 2011
- 9,158
- 17,056
Miaka ya 1980 na 1990 kwenda 2000 kulikuwa na watu wanadaiwa kuwa ni wanyonya damu. Magari ya msalaba mwekundu tulikuwa kukikutana nayo lazima tutoke mbio kwa hofu ya kunyonywa damu.
Binafsi mimi kuna watu pale kijijijni kwetu mkoani kilimanjaro walikuwa wakihusishwa na unyonyaji damu. Mmoja nadiriki kumtaja alikuwa akiitwa Michael Ibrahim wa kijiji cha Longuo. Huyu bwana alikuwa akiogopwa na kila mtu.
Watoto wadogo wakimwona walikuwa lazima wakimbie. Pia baadhi ya wakina mama nao pia walikuwa wakimwogopa. Kuna taarifa za wakati huo kukutwa kwa miili ya watu wakiwa wamekufa na huku miili yao ikiwa imegongwa mihuri kuonyesha kuwa yule marehemu kanyonywa damu. Na wengi wa watu ambao walikuwa akisemwa kuwa ni wanyonya damu walikuwa ni watu wenye kipato. Hivyo kipato chao kuhusishwa na unyonyaji wa damu.
Kilichonifanya nilete huu uzi hapa ni kutaka kujua hii kadhia ni kweli ilikuwepo? Na kama ni kweli hiyo damu walikuwa wanapeleka wapi?
Sababu mimi nachojua ni kwamba damu ni kwa ajili ya tiba yaani kwa ajili ya kumwongezea mtu aliyepungukiwa na damu.
Sasa inakuwaje utoe uhai wa mtu kwa ajili ya kuokoa uhai wa mtu?