Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,618
- 20,556
Matapeli wa kidini, wanajimu na waganga wanajua kucheza na matukio.
Mbasi
Kwa muda fulani alikuwepo Mbasi aliyedai kuwa sawa na Kyala (kwa ukuu). Alijifunua kupitia kwa kaimu wake hasa sehemu za Lufilyo chini ya milima ya Ukinga.
Hata kabla ya Wamisionari wa Berlin kufika kule, yule kaimu kwa jina la Mwamafungubo alikuwepo. Yeye alikuwa mtu mnyonge, lakini aliyeogopwa sana. Mmisionari Schumann (wa Berlin Mission) alieleza hivi juu ya Mbasi na kaimu wake (katika: Warneck, Allgemeine Missionszeitschrift 1916): “Usiku Mbasi aliweza kusema kwa sauti kuu na nyembamba, ‘Mimi ni Mbasi, nina shida. Msaidizi wake mmoja aliuliza, “Je, wewe ni Mbasi? Unataka nini kutoka kwetu?” Ndipo sauti nyembamba ilipojibu, “Nipeni binti wa N.N. (fulani) kuwa mke wangu. Akabidhiwe mtumishi wangu Mwamafungubo. Chifu N.N. (fulani) anitolee ng’ombe watatu. Mtumishi wangu Mwamafungubo atanichungia ng’ombe hao.” n.k.
Mbasi alitolewa vitu hivyo vyote. Mtumishi wake Mwamafungubo alichunga ng’ombe, alikunywa maziwa, alimwoa msichana na hivi aliishi maisha ya anasa kabisa.
Wamisionari walipoingia walidai kuwa wao ni watumishi wa Mungu, yaani Kyala. Mwamafungubo naye alileta ng’ombe mdogo kama salamu, walivyofanya machifu wote, lakini ilibidi zawadi yake ikataliwe. Kwa njia hiyo Wamisionari walieleza kuwa Mbasi siyo Mungu. Ndipo Chifu Mwakatungila (ambaye Wamisionari walikaa katika eneo lake) alimtwaa tena mwanamke fulani kwa jina la Kinyolobi (ambaye alikuwa amemtolea Mbasi) na vilevile aliwachukua ng’ombe aliokuwa amewatoa. Machifu wengine nao walifanya vivyo hivyo. Basi mchunga ng’ombe wake Mbasi, Mwamafungubo, alikimbia kuishi upande mwingine wa mto Lufilyo.
Tauni ilitokea. Mwamafungubo - Mbasi alieleza kwamba yeye ndiye aliyetengeneza tauni kwa sababu walikuwa wamemchukua mke wake Kinyolobi. Alidai kwamba atawafufua ng’ombe, mwanamke akirudishwa kwake.
Machifu walitaka kujaribu kuwa Kinyolobi arudi kwa Mwamafungubo kwa muda wa siku tano; ndivyo alivyofanya. Baada ya muda alikuja na kusema kwamba Mbasi alidai hata ng’ombe wakuja naye. Basi chifu Mwakatungila alitoa ng’ombe mmoja mwenye tauni akisema kwamba Mbasi aonyeshe uwezo wake wa kuwaponya ng’ombe katika huyo ng’ombe. Mwanamke alikuja tena akadai vibuyu vilivyojaa mafuta. Kwa sababu ng’ombe waliokufa hawakufufuka, basi Mwakatungila hakuruhusu mwanamke arudi tena kwa Mbasi. Ndipo Mwamafungubo alienda magharibi kwenye eneo la chifu Mwainyekule akamwonya kwamba ataleta simba. Wakati ulenzige walikuja baada ya tauni. Mara moja sauti ya Mbasi ilisikika ikisema, “Nzige hao ni simba ambao nimewatuma kama adhabu kwa sababu mmemchukua mke wangu Kinyolobi.”
Basi kundi la wanajeshi wa kutoka Ziwa Nyasa walikuja kudai kwamba mwanamke arudishwe kwa Mwamafungubo. Kwanza ombi hilo lilikataliwa, lakini baadaye mwanamke alirudi. Kinyolobi mwenyewe ambaye bila shaka alikuwa amechoka na matatizo hayo, usiku mmoja, sauti nyembamba iliposikika, alimkamata mwenye sauti. Kumbe ni Mwamafungubo mwenyewe. Kinyolobi aliwaita watu wengine waone na hivi Mwamafungubo alidhihirishwa kuwa mdanganyifu kwa watu. Kinyolobi mwenyewe kwa hiari yake alirudi kwa Mwakatungila. Mwamafungubo alipoendelea na shughuli zake vijana wawili walitangaza kuwa wanajiandaa kumshika. Ndipo Mwamafungubo alipotea, wala hakuonekana tena.” Maelezo ya Mmisionari Schumann yanaishia hapa. Niliambiwa kwamba kabla ya kufika kwetu huko Rungwe 1891 Mbasi alikuwa anafanya fujo yake hata huko, kwa mfano katika kijiji cha Ilolo. Mbasi alijiita,“Kyala, Mwatonoka, Lwembe, Njoka ja misi”. Mara nyingi alidai apewe ng’ombe akapewa. Ng’ombe hao walikaa kwa chifu Mwainyekule mpaka Mwamafungubo alipofukuzwa.
Baadaye nilisikia kwamba alionekana tena katika sehemu za Bwanji. Pale alitangaza kuwa yeye atawafukuza Wazungu katika nchi. Alidai kuwa tayari alikuwa ameipiga teke nyumba ya Kyamba (Misionari Nauhaus). Fahamu: Radi ilikuwa imeipiga ile nyumba.
Baadaye Wamisionari wa Berlin walifahamu kwamba mwana wa Ngulubi (aliye Mungu mkuu wa Wabena) anaitwa Mbasi. Hivi inaonekana kwamba Mbasi aliabudiwa kama mzimu mkuu wa Wabena na kwa jina hilo Mwamafungubo amewadanganya wenyeji huko Lufilyo.
Kisa hiki kipo kwenye kitabu Wa-Konde. Unaweza kisoma ndani ya app ya Maktaba Sauti. Ipo playstore.