Wanunuzi wa mpunga/mchele karibuni

ELIAS MICHAEL MORRIS

JF-Expert Member
Sep 26, 2016
384
500
mimi ni mkulima mdogo mdogo nafanyia shughuri zangu za kilimo mkoan Morogoro wilaya ya Mvomelo maeneo ya manungu tulian (karibu na kiwanda cha Mtibwa suger), nimelima mpunga heka sita (6) na umezaa vizuri mno, nategemea kupata si chini ya gunia 70 mpaka 100 za mpunga, nategemea kuanzia jumamos ijayo nianze kuvuna hivyo nakaribisha wanunuzi wa mpunga na mchele tufanye biashara na nategemea kupeleka jijini dar es salaam kufanyia biashara huko hivyo kama wewe ni mnunuzi huko dar au hata kama huku huku morogoro nakukaribisha pia
contacts.
0621038229.
0784133449.
0679670906.
eliusmoris2@gmail.com
 
usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
11,956
2,000
Heka 6 gunia 70 mpaka 100 kweli? Wewe unacheza sio mkulima, mkulima wa kweli kila heka 1 gunia zaidi ya 45, Hivyo heka 6 ni zaidi ya gunia za mpunga 270.

Bila kuweka sawa hesabu nakuona tapeli mkuu kweli tena.
Aiseee me hata nlikua na,shda na
Mchele lakin kwa hzo hesabu zake
Za hekar 6 gunia 70
Haziingian kabsa

Huyu kuna ambao hata waacha salama
 
TEAM VIBAJAJI

JF-Expert Member
Oct 9, 2016
1,852
2,000
Aiseee me hata nlikua na,shda na
Mchele lakin kwa hzo hesabu zake
Za hekar 6 gunia 70
Haziingian kabsa

Huyu kuna ambao hata waacha salama
Yupo sahihi wakuu kwakilimo chetu cha jembe lakusukuma kwamkomo nabila pembejeo nikimaanisha mbolea na dawa kwa heka moja niwastani wa gunia kumi mpaka kumi na mbili
 
ELIAS MICHAEL MORRIS

JF-Expert Member
Sep 26, 2016
384
500
Heka 6 gunia 70 mpaka 100 kweli? Wewe unacheza sio mkulima, mkulima wa kweli kila heka 1 gunia zaidi ya 45, Hivyo heka 6 ni zaidi ya gunia za mpunga 270.

Bila kuweka sawa hesabu nakuona tapeli mkuu kweli tena.
sijakata ila hayo ni maoni yenu na hesabu zenu ila sisi huku kwa kawaida heka ya mpunga mdogo inaweza kutoa gunia 18 mpaka 20 na mpunga mkubwa hutoa gunia 15 mpaka 18 inategemea na jinsi ulivyobeba maana kuna mengine huwa mapumba tu yasiyo na mchele ndani na kikubwa ni utapeli gani huo mnaozungumzia nyinyi wakati we unauona mzigo, unauchunguza ukishalizika nao ndio tunafanya biashara,

mi sijajua wao wanapiga hesabu hozo kwa kilimo cha wapi ila kwa sisi huku huwa tunapata gunia hizo yani ukikosa zaidi basi ni gunia 70 ila kwa kawaida zinaweza kua 80, 90, 100 au hata kuzidi hapo
 
Kamawewe

JF-Expert Member
Jan 16, 2013
471
500
kwa huku tuliani kwa sasa mpunga mdogo au wenyeji wa huku wanauita saro (sijui jina la kitaalam unaitwaje) unauzwa tsh 65,000 na mpunga mkubwa (super) huuzwa tsh 75,000 mpaka tsh 80,000
Mkuu samahani ukikoboa mpunga Mkubwa gunia moja unapata kilo ngapi na na mpunga mdogo kilo ngapi.Wewe ni mwenyeji huko?
 
MBITIYAZA

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
15,060
2,000
Yupo sahihi wakuu kwakilimo chetu cha jembe lakusukuma kwamkomo nabila pembejeo nikimaanisha mbolea na dawa kwa heka moja niwastani wa gunia kumi mpaka kumi na mbili
hakika,na ubora wa ardhi pia yuko sawa kwenye makisio yake wakuu,jaribuni kutembea,...
 
ELIAS MICHAEL MORRIS

JF-Expert Member
Sep 26, 2016
384
500
Mkuu samahani ukikoboa mpunga Mkubwa gunia moja unapata kilo ngapi na na mpunga mdogo kilo ngapi.Wewe ni mwenyeji huko?
kwa kawaida ukikoboa mpunga gunia 1 unaweza kupata kilo 55 mpaka 65 na mda mwengine unaweza kupata hata zaid ya hapo inategemea na jinsi lilivyojazwa hilo gunia na upepetaji wa pumba kabla mpunga hujajazwa katika gunia
 
marion09

Member
Sep 26, 2012
62
95
Heka 6 gunia 70 mpaka 100 kweli? Wewe unacheza sio mkulima, mkulima wa kweli kila heka 1 gunia zaidi ya 45, Hivyo heka 6 ni zaidi ya gunia za mpunga 270.

Bila kuweka sawa hesabu nakuona tapeli mkuu kweli tena.
Anamaanisha ekari na sio hekta
 
kanyela mumo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,038
2,000
sijakata ila hayo ni maoni yenu na hesabu zenu ila sisi huku kwa kawaida heka ya mpunga mdogo inaweza kutoa gunia 18 mpaka 20 na mpunga mkubwa hutoa gunia 15 mpaka 18 inategemea na jinsi ulivyobeba maana kuna mengine huwa mapumba tu yasiyo na mchele ndani na kikubwa ni utapeli gani huo mnaozungumzia nyinyi wakati we unauona mzigo, unauchunguza ukishalizika nao ndio tunafanya biashara,
Hata hesabu zako zimedifa.. 15 kwa heka 6 sawa na 90. 18 kwa heka 6 sawa na 108 gunia.

Bado hesabu hujaweka sawa, nimetokea kwenye kilimo cha mpunga mkuu.
 
bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,567
2,000
Heka 6 gunia 70 mpaka 100 kweli? Wewe unacheza sio mkulima, mkulima wa kweli kila heka 1 gunia zaidi ya 45, Hivyo heka 6 ni zaidi ya gunia za mpunga 270.

Bila kuweka sawa hesabu nakuona tapeli mkuu kweli tena.
kuna watu mnajua kumzidi hata Mungu, kipindi kulikuwa na mafuriko sana yaliyopelekea kupotea mpunga mwingi katika mashamba, so si ajabu kuona hesabu zake zinakwenda hivyo.

mimi binafsi namuunga mkono kwa hesabu zake..kwani nimelima kwa miaka mingi na bado ninalima mpunga mpaka sasa.
 
ELIAS MICHAEL MORRIS

JF-Expert Member
Sep 26, 2016
384
500
kuna watu mnajua kumzidi hata Mungu, kipindi kulikuwa na mafuriko sana yaliyopelekea kupotea mpunga mwingi katika mashamba, so si ajabu kuona hesabu zake zinakwenda hivyo.

mimi binafsi namuunga mkono kwa hesabu zake..kwani nimelima kwa miaka mingi na bado ninalima mpunga mpaka sasa.
labda wewe unaweza ukatupa maelezo yako na wewe huwa unavuna gunia ngapi kwa huko uliko
 
ELIAS MICHAEL MORRIS

JF-Expert Member
Sep 26, 2016
384
500
Hata hesabu zako zimedifa.. 15 kwa heka 6 sawa na 90. 18 kwa heka 6 sawa na 108 gunia.

Bado hesabu hujaweka sawa, nimetokea kwenye kilimo cha mpunga mkuu.
mpunga una changamoto zake nyingi mno tena hasa kwa sisi tunaelima kienyeji enyeji, unaweza ukazaa mwingi tu ila ukawa mapepe/mapumba meng, pia kunA changamoto ya ndege waharibifu hao nao ni zaidi ya tatizo maana gharama ya watu wa kukulindia ndege ni kubwa hivyo tunashindana nao wenyewe ndiomaana nimetoa hesabu/makisio ya chini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom