mimi naamini ili mtu uweze kufurahia mahusiano huna budi kuwa na mtu unayempenda kwa dhati. mimi ni msichana wa miaka 30 nimejaliwa kusoma vizuri maana sasa niko katika mchakato wa kuchukua PHD, nafanya kazi nzuri inayonitosheleza kwa mahitaji yote ya msingi kama msichana kwa shajo langu halali, lakini mpaka sasa sijajaliwa kumpata mwenza wa kweli jambo ambalo linanikosesha raha sana. kwa kifupi niko single
tatizo ambalo nimekuwa nikikumbana nalo nimekuwa nikipenda mtu jinsi alivyo lakini nimejikuta kati ya vijana wote wawili ambao nimebahatika kuwa nao hapo nyuma nikiamini walinipenda kwa moyo wa dhati kumbe hawakunipenda mimi kama mimi bali walinipenda kwa faida zao na nilichoambulia ni kukuta nimepangwa ni waongo wanawanake wengine hata baada ya kugundua mtu anajibaraguza eti ananipenda ni shetani alimpitia nikasamehe mara ya kwanza, ya pili ya tatu nikaona mhhh hapa natafuta kifo nikaachana na wa kwanza. wapili nae yakawa hayo hayo tena kibaya aliamua kutembea na rafiki yangu wa karibu niaamua mimi na yeye basi japo bado ananisumbua ila nilishafunga kurasa nao.
tatizo kuna vijana karibu watano ambao wamejitokeza kwangu wakisema wananipenda sana ila nikiangalia kati yao napata mashaka fulanifulani kama nikiamua kuanza uhusiano na mmoja wao hayatakuwa yaleyale? na kiukweli sijavutiwa sana kuwa nao kasoro mmoja wao ambae naona navutiwa nae kwa kiasi fulani ila nikiangalia mbeleni naona nitakwama kutokana na tofauti yetu ya kiimani maana yeye namwona ni muumini mzuri wa dini ya kiislamu na mimi ninaamini ninajitahidi kuwa muumini mzuri wa kikristu.
sasa nifanyeje? ilihali kwa sasa nataka mahusiano nitakayokuwa nayo yaishie kuw amke na mume na awe wa kufa na kuzikana. najitahidi kumwomba Mungu ila nazidi kuomba ushauri nifanyeje? maana nimeshumwa na nyoka nikiona nyasi nashtuka?