wanipendao siwapendi na nimpendae haonyeshi kunipenda kwa dhati nifanyeje?

Ukweli ni huu: wadada wengi wa kitz au kiafrika mkishasoma mnakuwa na maisha ya movie; unapoteza uafrika wako ambao ndio chimbuko la ndoa. Unakutana na demu siku ya kwanza ananyonya "barafu" na kumeza maziwa yake directly utamuoa huyo kweli? Haya ndio maisha ya movie! Pia unakuwa na un-attainable ambitions, mtu anaekusogelea akisikia anakula kona. Halafu huwa unafall in love easily, like one 9t standing huo ndio uzungu nausema. My advice, to get married in Africa by an African man be African lady, behave. Na sio una PhD una-network na darasa la saba, dereva au konda wa basi, fundi wa garage, mfagizi etc hata kama ni handsome hawezi kukuoa. Tafuta status yako, sio upo kwenye training na wasomi wenzako unampeleka konda wako anaekuchakachua mbele ya hao wasomi, watakudharau hati aliekuwa na nia anaifuta hapohapo. Fuata ushauri wangu, you will get married soon.

PHD student..............hapo dada lazima uwe muangalifu kidogo, hicho kisomo, kinatisha vijana wengi!!!!, Ukianza kujuana na kijana usimuulize kasoma mpaka wapi, nawe pia usimueleze kisomo chako.
 
PS: Dada mpendwa tafadhali soma kwa umakini hayo maneno ya "Philosopher" or the "Preacher" or "Qoheleth"; kama wewe Mkristo unajua ni Mithali 3:1ff; kama wewe muumini wa imani nyingine, still this wisdom might help you-yaani kila kitu kina wakati wake-so wait for you time to love, it shall surely come, but not out of desperation ila out of expectation...

Mkuu I believe ni Mhubiri 3:1ff...
 
Dada, we ni Mhaya!?? lol..maana hata jina lako linakaa kihivohivo..wakujisifusifu!
Kuwa mpole..na kama kweli wamwamini Mungu endelea kuomba..hakuna lisilowezekana kwake!
But first..jiangalie, jichunguze, do u have the qualities of a wife!??
Otherwise, hata celibacy ni lifestyle....
 
PHD student..............hapo dada lazima uwe muangalifu kidogo, hicho kisomo, kinatisha vijana wengi!!!!, Ukianza kujuana na kijana usimuulize kasoma mpaka wapi, nawe pia usimueleze kisomo chako.

Ndoa haina PHD wala JAMAA ZAKE..... nyie mnaoshauri kwa misingi ya elimu.... mnakosea... NIPO NAKUSUBIRI dada Ni PM nami nimejeruhiwa siwaamini wanawake... labda kwa story yako naweza kukuamini
 
Ndoa haina PHD wala JAMAA ZAKE..... nyie mnaoshauri kwa misingi ya elimu.... mnakosea... NIPO NAKUSUBIRI dada Ni PM nami nimejeruhiwa siwaamini wanawake... labda kwa story yako naweza kukuamini

Nakubaliana na hiyo red
 
ndugu yangu mimi siyo Mhaya lakini siamini kuwa Wahaya ni watu wa kujisifusifu kama ulivyosema, sipendi kutumia mapungufu ya mtu mmoja kuwahukumu watu wote. ninashukuru kwa ushauri wako nitaendelea kuufanyia kazi.
 
ninapenda kuwashukuru kwa moyo wa dhati wale wote walioweza kuacha majukumu yao na kuamua kutumia busara zao kunishauri pamoja na kuniombea, ninasema asanteni sana kwa ushauri maana nimeweza kufarijika kwa mawazo yenu ya msingi. kwa wale wachache walioandika kwa mtazamo hasi napenda kuwashukuru pia maana hayo ndio maoni na mtazamo wao ila napenda kuwaambia kuwa siku zote tujifunze kuona matatizo au furaha za wengine ni mafanikio yetu ama matatizo yetu pia kama wanadamu ambao ni wasafiri hapa ulimwenguni.
nazidi kuomba ushauri na maoni yenu ili viweze kunisaidia katika hali inayonisibu kwa sasa. Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki katika maisha yenu.
 
"Kwa kila jambo kuna majira yake,
Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa;

Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa kilichopandwa;

Wakati wa kuua, na wakati wa kuponya;

Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka;

Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe;
Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;

Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza;

Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;

Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona;

Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia;

Wakati wa vita, na wakati wa amani"

PS: Dada mpendwa tafadhali soma kwa umakini hayo maneno ya "Philosopher" or the "Preacher" or "Qoheleth"; kama wewe Mkristo unajua ni Mithali 3:1ff; kama wewe muumini wa imani nyingine, still this wisdom might help you-yaani kila kitu kina wakati wake-so wait for you time to love, it shall surely come, but not out of desperation ila out of expectation...

Hapo umenena Seniorita manake haya mambo hayana formula, bora kuweka Imani kwa Mungu tu dada yangu,
Kwani kujiingiza kwene uhusiano na mtu mwingine kichwa kichwa unaweza ukajikuta unajiongezea machungu na majeraha moyoni.

Wala swala la umri lisikusumbue, Kumbuka sisi hatuijui kesho yetu itakuwa je, lakini Mungu yeye anajua.
Ni kweli uko katika wakati mgumu, ni kweli unaumia lakini mtazame Mungu zaidi, afadhali akamtafuta Mungu huku ukifanya mambo yako,
wakati wa Mungu ukifika utashangaa mambo yanakuwa marahisi.
 
ndugu yangu mimi siyo Mhaya lakini siamini kuwa Wahaya ni watu wa kujisifusifu kama ulivyosema, sipendi kutumia mapungufu ya mtu mmoja kuwahukumu watu wote. ninashukuru kwa ushauri wako nitaendelea kuufanyia kazi.

au we mhehe? Mvuto unahusika pia. Nitakupm tuongee vizuri kama utakuwa tayari
 
Hakuna jibu zaidi ya lile la kumwomba Mungu kwa vile.
1. Hakuna formula ya kujua akupendaye
2. Mapenzi hayahusiani na shule, utajiri/umaskini au kabila.
 
Back
Top Bottom