wanipendao siwapendi na nimpendae haonyeshi kunipenda kwa dhati nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wanipendao siwapendi na nimpendae haonyeshi kunipenda kwa dhati nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mafanikio, Dec 7, 2010.

 1. m

  mafanikio Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 51
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  mimi naamini ili mtu uweze kufurahia mahusiano huna budi kuwa na mtu unayempenda kwa dhati. mimi ni msichana wa miaka 30 nimejaliwa kusoma vizuri maana sasa niko katika mchakato wa kuchukua PHD, nafanya kazi nzuri inayonitosheleza kwa mahitaji yote ya msingi kama msichana kwa shajo langu halali, lakini mpaka sasa sijajaliwa kumpata mwenza wa kweli jambo ambalo linanikosesha raha sana. kwa kifupi niko single

  tatizo ambalo nimekuwa nikikumbana nalo nimekuwa nikipenda mtu jinsi alivyo lakini nimejikuta kati ya vijana wote wawili ambao nimebahatika kuwa nao hapo nyuma nikiamini walinipenda kwa moyo wa dhati kumbe hawakunipenda mimi kama mimi bali walinipenda kwa faida zao na nilichoambulia ni kukuta nimepangwa ni waongo wanawanake wengine hata baada ya kugundua mtu anajibaraguza eti ananipenda ni shetani alimpitia nikasamehe mara ya kwanza, ya pili ya tatu nikaona mhhh hapa natafuta kifo nikaachana na wa kwanza. wapili nae yakawa hayo hayo tena kibaya aliamua kutembea na rafiki yangu wa karibu niaamua mimi na yeye basi japo bado ananisumbua ila nilishafunga kurasa nao.

  tatizo kuna vijana karibu watano ambao wamejitokeza kwangu wakisema wananipenda sana ila nikiangalia kati yao napata mashaka fulanifulani kama nikiamua kuanza uhusiano na mmoja wao hayatakuwa yaleyale? na kiukweli sijavutiwa sana kuwa nao kasoro mmoja wao ambae naona navutiwa nae kwa kiasi fulani ila nikiangalia mbeleni naona nitakwama kutokana na tofauti yetu ya kiimani maana yeye namwona ni muumini mzuri wa dini ya kiislamu na mimi ninaamini ninajitahidi kuwa muumini mzuri wa kikristu.

  sasa nifanyeje? ilihali kwa sasa nataka mahusiano nitakayokuwa nayo yaishie kuw amke na mume na awe wa kufa na kuzikana. najitahidi kumwomba Mungu ila nazidi kuomba ushauri nifanyeje? maana nimeshumwa na nyoka nikiona nyasi nashtuka?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu tutashuhudia wafu wengi wakifufuka!
   
 3. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  ngabu bana! sasa greti thinka hapa ndio umesaidia nini? mdada analia, ww unamfananisha na thriller ya wacko jacko .
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Unafanyia wapi phd yako
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  na wewe greti think hapa ndio umesaidia nini?
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  naongeza idadi ya post, si unaonaga ndio kwanza natambaa na buku tu, mazee una buku 20 halaf ni candidate wa JF presidential election. Mpe mistari mdada kabla hajavaa kenge mwengine
   
 7. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnh pole...endelea kutafuta,atafutaye hachoki...
   
 8. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo mi KENGE???????/////
   
 9. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  wewe kiherehere bana! kwani imekuwaje mkuu? mbona unaji name calling mwenyewe?
   
 10. s

  sirgeorge Member

  #10
  Dec 7, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana dada yangu kwa yaliyokusibu. Mi nikushauri kwa sasa usikurupuke kuingia katika mahusiano mapya ni vyema utibu kwanza madonda yalikutokea. Mara nyingi sisi wanaume hasa wabongo wanaangalia status yako na hivi umesema unafanya Phd. basi kila mtu atatokea kwa lengo la kutaka kukuoa japo ni kweli sio wote wenye nia hiyo (i mean ya kuangalia unafanya nn, kazi gani n.k).
  Kuna hii kitu ya kutokuwa waaminifu inatokea hasa kama mpo mbalimbali (distance relationship) ambayo hata mimi nalia nayo, hata mimi napoandika yalitonikea kwa girlfriend wangu ambaye yupo Tz. So nilichoamua kwa sasa ni kutulia kwanza nimalize kilicholeta kutafuta shule Europe. Cha msingi ni kuomba mungu akupatie mume bora. Na hilo la kiimani angalia pia usije ingia katika migogoro wa kifamilia lakini hili pia inategemea na msimamo wa mtu kwani linazungumzika.
  Kila la kheri
   
 11. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nahisi kama si muhimu sana kujua hilo. Dada anaomba asaidiwe ushauri kaka yangu......

  Mimi dada yangu mpendwa nakushauri umalize kwanza hiyo PhD yako, then mambo ya mapenzi yafuate. Najua sababu zilizosababu mahusiana ya mwanzo inawezekana ni muda wa kukaa na huyo unayetegemea awe wako wa milele ni mchache kutokana na majukumu yako ya shule. Nakuomba sasa usichanganye mambo ya shule na mapenzi kwa sasa....maana najua PhD student walivyokuwa so busy. Kulinga na status yako najua wanaume wengi wanakasumba ya kuwaogopa sana wanawake wenye elimu kama yako... Kwa sababu hiyo usijionyeshe sana kama unajua kila kitu ukiwa na mtu ambae unategemea kuwa atakuwa mwandani wako. Wanaume huwa hawapenda wanawake ambao ni much-know....

  Pia kuolewa dada inachangiwa na mambo mengi sana, ambayo ni pamoja na kusali kwa nia. Kama ni mkristu dada yangu, najua utakuwa unafahamu kuwa kuna sala maalumu kwa ajili kuomba kupata mme/mke mwema. Usidharau, jaribu pia kusali na unaweza kuona maajabu ya Mungu...

  Huo ndio ushauri wangu dada yangu mpenzi.....maana najua unavyoteseka na napenda sana upate mwandani wako. MIMI NAKUOMBEA KWA HILO....
   
 12. s

  seniorita JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "Kwa kila jambo kuna majira yake,
  Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.


  Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa;


  Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa kilichopandwa;


  Wakati wa kuua, na wakati wa kuponya;


  Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;


  Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka;


  Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;


  Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe;
  Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;


  Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza;


  Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;


  Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona;


  Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;


  Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia;


  Wakati wa vita, na wakati wa amani"

  PS: Dada mpendwa tafadhali soma kwa umakini hayo maneno ya "Philosopher" or the "Preacher" or "Qoheleth"; kama wewe Mkristo unajua ni Mithali 3:1ff; kama wewe muumini wa imani nyingine, still this wisdom might help you-yaani kila kitu kina wakati wake-so wait for you time to love, it shall surely come, but not out of desperation ila out of expectation...
   
 13. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  sirgeorge + mafanikio= jibu sahihi
   
 14. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  vipi wewe umeshampata?
   
 15. s

  sirgeorge Member

  #15
  Dec 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana pilipili manga, nilichoandika ni hali halisi yaliyotokea. Na kwa taarifa yako sihitaji relationship kwa sasa kama ulisoma vizuri nilichoandika.Hii stress ya shule tosha sana.

  Hope umenipata
   
 16. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  senkyu sirgeorge
   
 17. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole sana msomi yawezekana unapata tabu kutokana na elimu na maisha unayoyaendesha. Tatizo la wanaume watz wengi wanaogopa chalenji za wanawake wasomi wakiamini kuwa watawatawala. Pili ukiogopa kung'atwa na nyoka basi mapenzi c yako maana hakuna kipimo sahihi cha mapenzi na nani mkweli au tapeli. Vyote hvi vinatofautiana kati ya mtu na mtu. Bahati mbaya sana wewe ndo mpimaji na vigezo vyako cc washauri kwa tusiowajua wala kuwa na wasifu. Kumjua mtu vyema kwenye mapenzi ni mpaka umpe nafasi ya kukujeruhi baadaye. God Forbid. So my dr sis hapo yataka umakini wako na nguvu za mwenyezi Mungu.
   
 18. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Mie tayari babu... umechelewa!!!!!!
   
 19. mtanzaniahai

  mtanzaniahai Member

  #19
  Dec 8, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni huu: wadada wengi wa kitz au kiafrika mkishasoma mnakuwa na maisha ya movie; unapoteza uafrika wako ambao ndio chimbuko la ndoa. Unakutana na demu siku ya kwanza ananyonya "barafu" na kumeza maziwa yake directly utamuoa huyo kweli? Haya ndio maisha ya movie! Pia unakuwa na un-attainable ambitions, mtu anaekusogelea akisikia anakula kona. Halafu huwa unafall in love easily, like one 9t standing huo ndio uzungu nausema. My advice, to get married in Africa by an African man be African lady, behave. Na sio una PhD una-network na darasa la saba, dereva au konda wa basi, fundi wa garage, mfagizi etc hata kama ni handsome hawezi kukuoa. Tafuta status yako, sio upo kwenye training na wasomi wenzako unampeleka konda wako anaekuchakachua mbele ya hao wasomi, watakudharau hati aliekuwa na nia anaifuta hapohapo. Fuata ushauri wangu, you will get married soon.
   
 20. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kuna mada moja nilishaandika inahusu haya mambo watu hawakuchangia lakini haya mambo yapo sana lakini usikate tamaa umeambiwa kila jambo lina majira yake na wakati wake kwenye maisha kuna wakati wa kucheka na kulia be yourself acha kucheza dramma na atakuja anayefanana na wewe
   
Loading...