Lengo ilikuwa kupita tu lakini kanasa na hataki kutoa. Naona hanifai nifanyeje kuliepuka hili?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Mimi Sexless kazi yangu kubwa hapa mjini ni ukungwi. Natoa ushauri na kusaidia watu wa rika zote kutatua changamoto za mahusiano. Leo nimefikwa na mteja akanipa maelezo yafuatayo:

"Kuna siku nilikosea namba akapokea msichana, kwa bahati alikuwa mji ninaoishi. Mahusiano yakanzia hapo. Bado mdogo kiumri na hana mtoto, hajaharibiwa na mifumo ya maisha ya mjini. Hana vizinga wala hana makuu. Mm nikawa nakula mara moja moja.

"Dada aliishia form 2 (b), anajua kusoma na kuandika. Lkn akiandika sms hata mwandiko wa mke wa Babalevo una afadhali.

"Njoo kwenye mahesabu ya pesa sasa, hata kutoa chenji hawezi. Kuna siku kaja dukani kwangu, mteja katoa elfu 5 halafu kanunua soda 3 za 700 kila moja, akamrudishia 3500.

"Mimi kuona hivyo hata hamu ya kumuona ikanitoka. Utampa kazi gani mwanamke kama huyu? Mtafanya mishe gani na mwanamke kama huyu? Ana nidhamu, ana heshima na kila kitu lakini amekaa kienyeji mno.

"Bahati mbaya kanasa ujauzito na hataki kuutoa, na kwao kanitaja. Japo kwao hawanifahamu. Nifanyeje?"

Kungwi Sexless na mm naombeni mawazo ya kumshauri mteja wangu huyu.
 
Nimecomment bila kusoma ila Acha zinaa, huyo ndio mkeo kwani hata wewe ni wa kienyeji. Leeni Mtoto wenu kwani hakuna jipya humu duniani.
 
hata wewe hujui vyote!
kuna watu wanakuona mshamba pia!
hata mimi pia sijui vyote naonekana mshamba pia.
usiogope mapungufu yake utayazoea na yanaweza kutatulika kuliko kuingia huku kwa hawa unaowaona wazuri lakini km zimesoma za kutisha na kuna puti za ajabu.
komaa mambo yatakwenda hata mimi pamoja na kusoma biashara, biashara ya duka siiwezi
 
Ss mkuu mambo ya kukosea kurudisha chenchi c kawaida na labda mtaa anaokaa hzo soda zinauzwa 500 akajua na kwako wauza 500 .mpe muda na elimu ..


Kataa NDOA

Ni UTAPELI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom