abudist
JF-Expert Member
- Oct 25, 2009
- 850
- 781
Wanigeria wazuia ndege ya KLM isiruke kutoka Amsterdam schiphol airport ili raia mmoja wa Nigeria aliyefungwa minyorororo ateremshwe. Mabishano na matakwa ya Wanigeria hao yalizuka baada ya kumuona raia huyo wa Nigeria akiwa amefungwa pingu na minyororo kama mtumwa au mnyama. Inasemekana alikuwa akirudishwa Nigeria sababu ya kutokuwa na karatasi za kuishi Uholanzi. Baada ya zogo kuzidi hatimaye jamaa aliteremshwa na askari akiendelea kuwa chini ya ulinzi. Na ndege ikaendelea na safari yake.