Shirika ndege KLM latimiza miaka 100 toka kuanzishwa na miaka 50 ya kutua Tz,ATCL inalo la kujifunza

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg


K L M R OYAL DUTCH ni shirika la ndege la Uholanzi,KLM ni kufupisho cha Koninklijke Luchtvaart Maatschappij,N.V.(Royal Aviation Company,Inc.)

Shirika la ndege la KLM litatimiza miaka 100 itakapofika Oktoba 7 mwaka huu, tangu kuanzishwa kwake 1919.

KLM ndio shirika pekee duniani linajiendesha kwa kutumia jina lake la asili (Original Name)

KLM ina kampuni tanzu ya mizigo inayofahamika kama Martin Air.Hii husafirisha mizigo sehemu mbalimbali za dunia.

KLM ina miruko 145 sehemu mbalimbali za dunia,Ulaya,Afrika,Amerika Kusini na Kaskazini pamoja na Asia na mabara mengine.

KLM ilianzishwa miaka 7 kabla ya kuzaliwa Malkia wa Uingereza Elizabeth II,

KLM ilianza kuwepo miaka 16 baada ya ndege ya kwanza iliyofanikiwa kuruka 1903 ya ndugu wawili Orville na Wilbur

KLM tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa ni idadi ya Maraisi wa Marekani 18 na Mawaziri Wakuu wa Uingereze 19 waliohudumu kwa nyakati tofauti,

KLM ilianza kuwepo kabla ya PanAm,Quantas,Delta na mashirika mengine ya ndege makubwa yaliyokuwepo na yaliyopo sasa,

KLM ilianzishwa kabla ya Airbus (1970) na Bombardier (1942), na McDonnell Douglas(1947) makampuni maarufu ya utengenezaji wa ndege duniani,

KLM Imepita kwenye misukosuko mikubwa ya dunia, mdororo wa uchumi wa 1929 na vita ya dunia ya mwaka 1939-45,

KLM imeshuhudia na kutumia mabadiliko ya teknolojia zote ya huduma za usafiri wa anga,

KLM ipo kabla ya kila kikubwa kinachohamishika kwenye ulimwengu wa sasa, ipo kabla ya UN, ipo kabla ya uhuru wa Afrika

KLM ndio ndege pekee iliyopo iliyohusika na ajali iliyouwa watu wengi zaidi katika historia ya Usafiri wa Anga. Ajali ya Tenerife iliuwa abiria 583 ikihusisha ndege ya shirika la Pan Am na KLM yenyewe katika uwanja wa Los Rodeos kwenye visiwa vya Kanari.

KLM ndio taswira ya mashirika ya ndege Duniani, kwao uzoefu ni Anga, kila shirika linataka kuwa kama #KLM

Kufikia mwaka 2016,KLM ilikuwa na "Code Sharing Partenerships" na mashirika zaidi ya 50 duniani,kwa Afrika ni Kenya Airways.KLM ni mwanachama wa Skyteam ambapo na Kenya Airways ni member pia.

Kwa Tanzania KLM hutua katika viwanja viwili karibu mara 6 kwa week na msimu wa watalii mara zote ktk wiki,KIA na JNIA.Mruko wake huwa ni Amsterdam-KIA-JNIA-Amsterdam.

Safari ya KLM kutoka Amsterdam mpaka KIA huwa ni masaa 8.5(Non-stop)Na baadae dakika 45 kati ya KIA na Dsm au zaidi.Katika eneo la Afrika Mashariki na kati,Tanzania ndio mahali inatua viwanja viwili tofauti.

Mwaka huu KLM inatimiza miaka 50 toka ilipoanza safari zake Tanzania.Ilitua kwa mara ya kwanza mwaka 1969 ikiwa na ndege ina ya McDonnel Douglas DC-8,na kwa muda mrefu baadae KLM ikawa inaleta ndege aina ya Airbus330-300 au Boeing777-200/300ER.

Ila kuanzia June 2019,KLM katika safari zake za siku 7 kwa week,siku 4 itakuwa inaleta B787-9(Dreamliner) badala ya B777-200ER na siku 3 zilizoalia italeta B777-300ER.

Martin Air,kaampuni tanzu ya mizigo ya KLM,hutua mara moja kwa kila week JNIA,ambapo ni Alhamisi au Ijumaa.Ni mruko wake huwa ni Amsterdam-J'burg-Dsm-Jomo Kenyata-Amtserdam.

Kufuatia Tanzania kuwa moja ya "destination" muhimu ya KLM,ndege moja ya KLM aina ya B777-200ER imepewa jina la "MOUNT KILIMANJARO".


Leo malimwengu hawamjui Albert Plesman,wanaijua KLM na hichi ndicho alichoiachia Dunia

Wakati Plesman anaanzisha KLM akiwa na miaka 30, mashirika ya ndege yalikuwa 16 tu ulimwenguni,kama Plesman atafufuka leo, atakutana na mashirika zaidi ya 5000 ya ndege yaliyopo sasa duniani kote,ikiwemo ATCL ya Tanzania.

Tuelewe kitu kimoja,ili udumu na uishi muda mrefu yakupasa uishi ukiwa unajua dunia inataka nini. KLM walifanikisha hilo kwa wakati, wapo na pengine wataendelea kuwepo,pamoja na ugumu wa uendeshaji wa biashara ya safari za anga wamejiweka katika njia yakufuatwa na kugombaniwa.

Ni matumaini yetu,katika miaka hii 50 ya KLM kuja Tanzania na miaka 100 toka kuanzishwa kwake,wadau wa usafiri wa anga,serikali na hasa shirika letu la ATCL na uongozi wake una cha kujifunza.Usafiri wa anga ni nembo ya Taifa,ni Utaifa na ni ishara ya ukuu wa Taifa katika ulimwengu wa anga.Tuwekeze kwa fikra endelevu na mipango dhabiti,ili tusiwe kama moto wa kifuu.Tuache misingi inayodumu hata sisi tutakapokuwa hatupo madarakani.
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    61.1 KB · Views: 87
Ubarikiwe mkuu barafu.. Raha sana kama unakuwa na akili na maarifa kama ya mkuu barafu.. Umahiri wa kuuliza maswali yenye tija na magumu kama mkuu Kiranga.. Na uwezo wa kuyaelezea mambo kwa kutumia taaluma na usomi kama Mkuu Malcom Lumumba.
 
Ndege ya mizigo inatwa Martin Air je ile inayokujaga jumapili ikiwa na mizigo tupu KLM Cargo ndo hio hio Martin Air au, bila kusahau natanguliza shukrani za dhati kwa mzee wangu kufanikisha mwanae kupanda dege hili...mara 2...1999 + 2002...Rest in Peace..Papa...
 
Oh! Ahsante kwa maarifa haya, nimewahi kupanda hii ndege mara 2 ila sikuwahi kujua kirefu chake.

Niliposhuka pale Amsterdam toka Dar na jidege lao kuubwa uwanja mzima yamejaa hayo, baadae nikapanda ndege yao nyingine kule wanaitaga City hopper kuelekea mkoa mwingine ndani ya Schengen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom