Bin Mngereza
JF-Expert Member
- Sep 3, 2012
- 610
- 269
Kisima cha Giningi,Mzimu wa Kale,Duniani kuna Watu,Moja ya vitabu vizuri vilivyowahi kuburudisha na kuchangamsha akili wakati ule ni vile vya bwana Msa (Mohamed Said Abdullah). Kuna mtu anakumbuka SIRI YA SIFURI? Au niko mwenyewe?
Zaidi,Mimi nimekisoma kwa mara ya kwanza 1972Mambo ya kitambo kidogo miaka ya 1980'S,Hadithi zake zinasisimua sana mkuu
Duuh std 6Nina miaka 2
Kiongozi,kuna mwandishi anaitwa NICK CATER,kama sijakosea,ukisoma vitabu vyake,utabaini kuwa vitabu vya Musiba ni kama copy and paste.NATAFUTA NJAMA.kitabu kizuri sana
Nakufa,nakufa,wapo wapi wale wakuu waliotangulia mbele??siwaoni,wewe upo makumazahn??au umekwisha nitangulia sehemu ya mbele nisiyoijua mimi?,mahali panapozungukazunguka??Nasikia harufu ya damu,Naitwaaa!Ndipo alipoiinua inkosikazi yake,akaizungusha ,Ikawa kama inayotoa nuru ya dhahabu,,
Bulicheka!
Mgeni siku ya kwanza,Nakumbuka mgeni siku ya kumi tu
Nakufa !nakufa !lakini kitakuwa kifo cha kifalme! wako wapi waliotaka kuipanda ngazi kuu ?mbona siwaoni !upo wapi makumazahn? au umekwisha nitangulia katika sehemu ya kiza ninayo elekea ?damu inapofusha macho na sehemu inazunguuka! nasikia sauti ya maji! kisha akalitizama shoka lake la vita na kusema kwa heri inkosikazi! hapana tumeishi pamoja kwa muda mrefu hakuna mtu wa kuweza kukushika kisha akalizunguusha juu ya kichwa chake na kufanya mduara basi hapo alilishusha katika mwamba ule mtakatifu pigo moja lenye nguvu lile shoka likavunjika na baadhi ya sehemu ya ule mwamba hali ya kuwa nae akianguka huku kashika kipini cha shoka lile basi hivyo ndivyo alivyokufa yule mzee mzulu.Nakufa,nakufa,wapo wapi wale wakuu waliotangulia mbele??siwaoni,wewe upo makumazahn??au umekwisha nitangulia sehemu ya mbele nisiyoijua mimi?,mahali panapozungukazunguka??Nasikia harufu ya damu,Naitwaaa!Ndipo alipoiinua inkosikazi yake,akaizungusha ,Ikawa kama inayotoa nuru ya dhahabu,,
Yule mtu wa tatu alinifanya nimtizame zaidi na kugundua huyu si mkazi ila ni mzulu halisi kinywa cha ucheshi cha kizulu na macho madogo ya kahawia ila makali kama mwewe! japo kuwa nilikuwa sijamuona kwa muda wa miaka 12 nilimtambua na kumsalimia kwa sauti ndogo kwa lugha ya kizulu hujambo umslopogaaz basi yule mtu mkubwa nusura shoka lake la vita lianguke kaanza kunisalimia aah mkuu! mkuu baba! Makumazahn mwindaji akeshae hodari mwepesi rafiki muaminifu ambae risasi zake hazikosi shabaha muuwaji wa simba mla tembo mkuu ! mkuu baba !ama kweli ile methali ya kikwetu isemayo milima haikutani ila binadamu hukutana ni ya kweli kabisa na tena yenye busara tizama alikuja tarishi kutoka natal akalia na kusema makumazahn amefariki na nchi haitomuona makumazahn tena lakini tizama leo hii baba yangu katika nchi ngeni tena yenye harufu mbaya kama hii namuona tena makumazahn hakika ndie yeye bila shaka! Manyoya ya mzee mbweha yamekwisha ingia mvi! Lakini macho na meno yake bado ni makali vilevile kama zamani! Mkuu baba unakumbuka namna ulivyo pitisha risasi penye jicho la nyati aliekuwa akishambulia?Unakumbuka ,, unakumbuka Mkuu siku ulipoelekeza risasi yako kwenye sikio la Nyati aliyekuwa anashambulia unakumbuka?
Yaah hizi ni baadhi ya kauri za huyu jamaa mlinzi wa Ngazi kuu . hakika ni simulizi nzr sn.
Tulikuwa tumekaa mezani ni huzuni iliyotawala hata yule bibi mackenzie hakuja kujumuika nasi. Niseme sikuweza kula na ni ujio wetu umesababisha maafa kwa wenyeji wetu nikaomba radhi na kutoka nje nilikuwa nimekaa kwa muda mchache mara nikasikia sauti ya mwango kufunguliwa kisha kuna kitu kikapita kikiviringika mbele yangu na kutulia mbele kidogo nikajishauri nikifuate basi nikakishika kilikuwa ni kilaini tena chenye uvungu nikakiinua juu ili niweze kuona katika nuru ya mbalamwezi loh!mwamba mtakatifu ulipo vunjwa kwa pigo lililo nyooka !! ama kitabu hiki kilikuwa kitamu - hutaki kukiacha
Pamoja swahiba tunadokoa dokoa taratibuHadi raha thanks Guasa Amboni for the needful