Wangapi mnaona dola ikielekea juu ya dari kama mimi?

Wangapi mnaona dola ikielekea juu ya dari kama mimi?

View attachment 1008116

Nilitamani kuweka hichi kitu siku nyingi ila jana nimenunua dola kwa Sh 2325 nikaona hapana itabidi niweke ili bandiko la utafiti kidogo.

In short ni kwamba dola ipo kwenye kipindi muhimu sana kwa sababu huu ni wakati ambao inakuvuka highest high ya mwaka 2015 wakati rate ilipokuwa kwenye 2335 na kuvuka huku kuna maana moja kubwa sana kwangu kwamba 'Banki kuu haina nguvu tena ku stabilize the exchange rate in the economy' (in my OPINION)

Kipindi cha nyuma mwaka 2015 baada ya dola kufika around 2335 kama unavoona kwenye chart hapo juu, Banki kuu ilikuwa na mabavu ya kuongeza supply (ujasi) wa dola kwenye uchumi kutoka kwenye reserve ambayo ili hit moja kwa moja kwenye mabenk ambayo automatically ikashusha bei ya dola kwa momentum ambayo ni kubwa mpaka kwenye level ya 2000 kwa dola moja mwanzoni mwa mwaka 2016.

Unaweza ukashangaa nguvu hiyo imepotea vipi kwa wakati huu, kwanini wasifanye kama kipindi cha nyuma? its simple kuna mambo yafuatayo

1) Japo ni kweli kwamba Banki wanaweza kuwa na reserve ya dola ila wanakosa uthubutu kwa wakati huu kwasababu moja kubwa -- kuna uncertanties kubwa mno kwa sasa inayotishia inflow ya dola kwa wakati ujao. So automatically Bank kuu hawawezi kuthubutu kumwaga supply ya dola kwenye uchumi ili kuimarisha shilingi maana kufanya hivo ina maana wanajiweke kwenye hatar ya kukausha foreign reserve ya nchi which is dangerous kwa kipindi hiki. Ukikaukiwa dola halafu una external debt ipo kwenye dola maana yake unaiweka shillingi yako rehani coz itabidi uishushe zaidi ili uattract inflows za dola ambayo inaweza kuwa janga kubwa mnoo.

2) Ujasi wa fedha (TZS) kwenye uchumi bado sio wa kuridhisha namaanisha (money supply growth kwa kipindi hiki bado ipo kwenye record low.. so any attempt ya kuongeza dolla kwenye uchumi inamaana bank kuu watabidi kununua shillingi iliyopo kwenye uchumi ili dola iweze kuingia kwenye mzunguko na rate iweze kushuka.. But kulingana na hali ya uchumi ya sasa hivi, kupunguza supply ya shillingi maana yake ni kupunguza money supply growth ambayo directly inaenda ku hit ukuuaji wa uchumi kama tulivolalamika mwaka 2017 (utasakia laymen wanasema Magu kabana kumbe ni kwamba ujasi wa fedha haukui kwenye uchumi kama ilivokuwa kipindi cha nyuma)

Kuna issue nyingine kama
- Ukuuaji wa deni la taifa la nje by now ni kama USD 24 billion hivi... hii nayo inachangia pakubwa kuzorota kwa shillingi nazani ntajipanga next time kuelezea kwenye mada yake (mzozo wa madeni unaonukia Tanzania)
- Kuna issue ya nakisi katika account ya biashara .. na moja wapo ya mambo yanayosababisha hata issue pia ya korosho ipo maana imagine kama nchi ilikuwa ina uhakika wa kupata USD zaidi ya million 500 kila mwaka halfu automatikally haipo tena. (Hata hii ni sababu kwanini nimeona kwamba miaka mitatu ijayo dola inaweza kuwa zaidi ya 2500

Kwa hali ilivo hakuna matumaini hii dolla kwamba itakaa ishuke tena. It seems Banki kuu kama wamesalimu amri. Tegemeo lao pekee ni kwamba inflation ipo bellow 4% na hiyo inatokana zaidi na stabilization ya bei ya chakula.

Na tuzidi tu kuomba Mungu inflation inendelee kuwa hapa ilipo.. Ikianza kupanda na huku shilingi inaporomoka nadhani tutatafutana mpaka chini ya uvungu. Hao tunaowaita mabeberu nao nadhani hii point wanaingoja sana ifike. (Wale watu washenzi wewe usione wamekaa kimya)

Hiyo ya low inflation naamini inatokana na cooked statistical data. Mbona bei za vitu zinapanda? Tusubiri another three to six months muone kitakachotokea.
 
Noma sana mkuu! Wawekezaji wenyewe ndio hao wanakimbia maana Sera za uwekezaji awamu ya tano hazieleweki.

Leo hii nimeambiwa nitume invoice na client wangu mmoja anilipe ASAP. Analipa creditors wake na anahamia Rwanda (biashara yake hapa inafungwa). Mount Meru (Oil company) nao wame-relocate biashara yao kubwa Rwanda. Jiwe hajui alifanyalo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
The first time in ma life I hear that God will have to do something towards the shilling. Do yu expect him to pump in more shs? How soon?
 
Lisu we mbaya sana hadi Dola umeshuka kwa kutuchongea kwa mabebru aise naomba urudi achana na hizi harakati utatuua na njaa

Nadhani una maana kuwa shilingi ndio imeshuka na Dollar ndio imepanda thamani!! As long as no dollars will flow into our economy from whatever source, the shilling will depreciate. [Unaponunua $$$ kwa kutumia shilingi nyingi zaidi maana yake thamani ya shilingi inashuka]!!
 
Usipopenda kuambiwa kweli na wataalamu wa uchumi ukitamani kusifiwa tu unategemea nini?
.
.
Hayo ndo madhara ya akili ndogo kuongoza akili kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Takwimu zote hizo huwa natoa kwenye website ya BOT ... ninachofanya mimi ni analysis tu mkuu.. kwa hiyo hamna namna yoyote navunja sheria
No matter, Ww hujui kwa nn taarifa nyeti zinaandikwa kwa kiinglishi? Sasa Ww unatutafsria na kutudadavulia. Huo ni uchonganishi
 
Mleta mada yuko sahihi sana lkn nafikiri "Volume of Exports" pia imepungua mno sambamba na "Foreign Direct Investment" ambayo imepungua kutokana na sera tatanishi na ambazo sio rafiki kwa wawekezaji.

Vile vile kukatwa kwa misaada na wadau wa maendeleo pia inachangia ila hali itakuwa mbaya mno pale serikali ikifanya "Debt Servicing with Forex" huku inayoingia ikiwa kidogo hapo ndipo shilingi itakaporomoka zaidi.

Hii tabia ya kujidai kuwatunishia misuli haya mataifa ya magharibi ni kujitia kitanzi tu kwani Russia walijaribu na pesa yao Ruble ikaporomoka kutoka 32 mwaka 2010 hadi 65.60 kwa Dola moja leo hii.

Iran nayo mwaka 2010, 1 USD = 7,504 Iran Rial na leo hii 1 USD = 42,103 IRR, huku waajemi hao wakiendeleza mnyukano na Marekani. Hivyo mahasimiano haya yana gharama kubwa sana kwa uchumi wa nchi yoyote ile.
Russia waliweza ku Stablize kwa sababu wao wana Export mno Ges na mafuta na Natural resources zingine.

sisi sijui kama tuna expoer ile Gesi ya Mtwara hata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndo advantage za kusoma forex.

Kwa waliopata japo training ya wiki moja wamekuelewa to the maximum. Kwa wale wenzangu na mm ambao hatujagusa hiyo training na wala hatukuwahi kusoma mambo ya uchumi watapata tabu san kukuelewa.

Lkn kiukweli ulichoeleza hapo juu tuombe Mungu shilingi ipate nguvu, la sivyo we are finished.
Ameeleza vzr sana, but hiyo nguvu kwa Tsh itoke wp?
Tsh inahema coz of low inflation.
[emoji1] [emoji1] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji125] [emoji124] [emoji124]
Mkuu safari ni ndefu, bado ipo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chezea sanduku LA kura, poteza watu, minya Uhuru wa habari, minya demokrasia Lakini Uchumi ni kitu ingine...!

Hapana cheza na Uchumi~ utaumbuka
 
Uwezo wa kiongozi sio kuwa na maamuzi ya kununua vitu kama ndege, kusaini mikataba mikubwa mikubwa, n.k bali ni kuwa na uwezo wa kuifanya nchi yake iongeze uzalishaji na hivyo kukuza uchumi na kuongeza thamani ya local currency, n.k.
 
Mwaka 1980 USD ilikuwa Tsh 8
Mwaka 1989 ilikuwa USD mmoja karibu sh 120,
Mwaka 2005 ilikuwa kama Tsh 640
Mwaka 2014 ilikuwa kama Tsh1180
Ni wazi shillingi ilianguka tokea zamani bila brake.
Itazidi kubomoka hadi export na import ziwe sawiya.
Tuuze nje vitu vingi nje,fungua milango panua uwigo.
 
Back
Top Bottom