Wangapi mnaona dola ikielekea juu ya dari kama mimi?

Wangapi mnaona dola ikielekea juu ya dari kama mimi?

hivi kuna brocker ambaye naweza kutrade hii pair! yaan hapo ni kubuy then unalog off hadi 2025 ndio unakuja kuchungulia
Hii labda u trade na commercial banks.. but kwa sababu hawana leverage itakuwa ngumu ku make a lot of money.. labda uweke mzigo mrefu.. say ununue usd 200k @ 2320 = Tzs 464 million kwa leo halafu after 3 years uje kuuza kwa 2800 = Tzs 560 million === profit ya Tzs 96 million..

Hiyo USD 200K uiweke kwenye fixed deposit revolving kwa wastani wa rate ya 2.5% per year === roughly USD 4000 kwa mwaka or usd 12k in 3 years in interest
 
Umeeleza vizuri. Tatizo lingine ni kutotambua maamuzi ya Serikali yanaathiri vipi shilingi.

Mfano, sheria mpya za madini zilizotungwa na nguli Prof. Kabudi zimezika sekta ya madini mpaka imembidi Rais akutane na wadau. Kwa nini hawakukutana na wadau kabla ya kutunga sheria? Madini ni sekta mojawapo inayoingizia nchi $ nyingi.

Mfano mwingine, suala la korosho. Nahisi sasa wameona ni bora kuuza kwa watu nje wapate $ kuliko kukurupuka na kusema kila mtanzania apate kilo mbili.

Ukija kwenye upande wa manunuzi, nchi inafanya projects kubwa (ndege, SGR, Stiegler Gorge, n.k.) kwa kulipa $ upfront. Hizi $ zote zinaenda nje ya nchi na hazitumiki hapa huku uzalishaji wa hizi projects zikichukua muda mrefu.

Mfano mwingine, "kuvamia" maduka ya kubadili fedha za kigeni kunasababisha hata wale wenye shilingi waanze kufikiria kununua fedha za kigeni na kimbilio la kwanza ni $.

Mwezi wa 4/5 dola moja itafika shilingi 2,450.
Asante sana mkuu.. tuko pamoja.. kumbe wengi tunaona
 
Hii labda u trade na commercial banks.. but kwa sababu hawana leverage itakuwa ngumu ku make a lot of money.. labda uweke mzigo mrefu.. say ununue usd 200k @ 2320 = Tzs 464 million kwa leo halafu after 3 years uje kuuza kwa 2800 = Tzs 560 million === profit ya Tzs 96 million..

Hiyo USD 200K uiweke kwenye fixed deposit revolving kwa wastani wa rate ya 2.5% per year === roughly USD 4000 kwa mwaka or usd 12k in 3 years in interest

Hapo inflation rate ibaki hiyo hiyo (unrealistic), la sivyo utapata hasara kubwa. Aache kusikiliza hawa wapambe wenye ushamba wa madaraka na kuteua watu wa kumuitikia "ndiyo mzee". La sivyo ataangusha uchumi.
 
Kuna mtu hapa namdenda dora 2500. Natamani akubali kunitumia kipindi hiki ili nipate faida

mwanza
 
Asante sana mkuu.. tuko pamoja.. kumbe wengi tunaona
Ni kweli wengi mnaona lakini tatizo ni kwamba wanaosema ni wachache sana. Tena wanaosema hadharani wakiwa na majina yao halisi ndiyo ni kama hawapo. Mitaani tunaulizana nini kinaendelea kwenye uchumi wetu hakuna anayetueleza sisi mbumbumbu wa elimu ya uchumi.

Kinachoonekana kwa tusio wataalamu wa uchumi ni kwamba watu wanakopa mikopo waniangiza kwenye biashara zinakufa kwa kukosa wateja, kodi zinashindikana kulipwa, gharama za kuendesha maisha zimekuwa kubwa sana na hakuna mtu anayejua hatima yetu kiuchumi itakuwaje.

Umezungumzia udhibitiwaji wa mfumko wa bei kutokana na udhibiti wa bei ya vyakula, lakini jambo hilo kwa upande mwingine limetufanya sisi wakulima tuone maisha yamekuwa kama tupo Jehanamu. Kwa bei ya mahindi ya sasa kwa mfano, inahitaji uuze kati ya magunia matatu mpaka manne ili upate mbolea mfuko mmoja ambao utautumia kwenye Hekari moja tu ya mahindi. Hapo suluhisho ni nini?
 
Mleta mada yuko sahihi sana lkn nafikiri "Volume of Exports" pia imepungua mno sambamba na "Foreign Direct Investment" ambayo imepungua kutokana na sera tatanishi na ambazo sio rafiki kwa wawekezaji.

Vile vile kukatwa kwa misaada na wadau wa maendeleo pia inachangia ila hali itakuwa mbaya mno pale serikali ikifanya "Debt Servicing with Forex" huku inayoingia ikiwa kidogo hapo ndipo shilingi itakaporomoka zaidi.

Hii tabia ya kujidai kuwatunishia misuli haya mataifa ya magharibi ni kujitia kitanzi tu kwani Russia walijaribu na pesa yao Ruble ikaporomoka kutoka 32 mwaka 2010 hadi 65.60 kwa Dola moja leo hii.

Iran nayo mwaka 2010, 1 USD = 7,504 Iran Rial na leo hii 1 USD = 42,103 IRR, huku waajemi hao wakiendeleza mnyukano na Marekani. Hivyo mahasimiano haya yana gharama kubwa sana kwa uchumi wa nchi yoyote ile.
 
Mabeberu Vs Sisi Nani ataibuka mshindi? Kama wachina tunaowategemea kwa misaada yao "isiyo na masharti" wanawapigia magoti Mabeberu, sisi ndiyo vita yao tutaiweza?
 
Kumbukumbu imenipotea kidogo, lakini aidha wiki iliyopita au wiki ya nyuma yake nilimsoma Governor akiongelea suala la Dola na stability ya Benki kuu kudhibiti hilo na kuwatoa hofu uma kuwa Benki kuu inatambua mtiririko unaoendelea na kuna reserve ya miaka 4 na miezi kadhaa juu ya kiwago cha East Africa.

Kiufupi niliweka kando ile taarifa maani niliona kuna habari haijawekwa wazi labda pia sababu ya kutofahamu sana mambo ya uchumi.

Tangu mwaka jana mwishoni nimekuwa nafatilia bei ya dola kila wiki kwa shilingi. Hizo rate ni za bureau de changes ila za kwenye mabenki ya biashara rate imeshafika 2400 kwa dola moja. hivo kufika mwezi wa tano kama hakutofanyika kitu basi dola moja kuinunua kwa Tsh 2600 haitakuwa ajabu.

Nimejikuta naifatilia dola sababu wakati wa likizo inakula shilingi yangu nnapokata tiketi, malipo ya huduma mbalimbali nikiwa nchi tofauti na Tanzania n.k. n.k.

Anyways, wacha nirudi kwenye mahaba kwaherini.

K' Matata.
 
View attachment 1008116

Nilitamani kuweka hichi kitu siku nyingi ila jana nimenunua dola kwa Sh 2325 nikaona hapana itabidi niweke ili bandiko la utafiti kidogo.

In short ni kwamba dola ipo kwenye kipindi muhimu sana kwa sababu huu ni wakati ambao inakuvuka highest high ya mwaka 2015 wakati rate ilipokuwa kwenye 2335 na kuvuka huku kuna maana moja kubwa sana kwangu kwamba 'Banki kuu haina nguvu tena ku stabilize the exchange rate in the economy' (in my OPINION)

Kipindi cha nyuma mwaka 2015 baada ya dola kufika around 2335 kama unavoona kwenye chart hapo juu, Banki kuu ilikuwa na mabavu ya kuongeza supply (ujasi) wa dola kwenye uchumi kutoka kwenye reserve ambayo ili hit moja kwa moja kwenye mabenk ambayo automatically ikashusha bei ya dola kwa momentum ambayo ni kubwa mpaka kwenye level ya 2000 kwa dola moja mwanzoni mwa mwaka 2016.

Unaweza ukashangaa nguvu hiyo imepotea vipi kwa wakati huu, kwanini wasifanye kama kipindi cha nyuma? its simple kuna mambo yafuatayo

1) Japo ni kweli kwamba Banki wanaweza kuwa na reserve ya dola ila wanakosa uthubutu kwa wakati huu kwasababu moja kubwa -- kuna uncertanties kubwa mno kwa sasa inayotishia inflow ya dola kwa wakati ujao. So automatically Bank kuu hawawezi kuthubutu kumwaga supply ya dola kwenye uchumi ili kuimarisha shilingi maana kufanya hivo ina maana wanajiweke kwenye hatar ya kukausha foreign reserve ya nchi which is dangerous kwa kipindi hiki. Ukikaukiwa dola halafu una external debt ipo kwenye dola maana yake unaiweka shillingi yako rehani coz itabidi uishushe zaidi ili uattract inflows za dola ambayo inaweza kuwa janga kubwa mnoo.

2) Ujasi wa fedha (TZS) kwenye uchumi bado sio wa kuridhisha namaanisha (money supply growth kwa kipindi hiki bado ipo kwenye record low.. so any attempt ya kuongeza dolla kwenye uchumi inamaana bank kuu watabidi kununua shillingi iliyopo kwenye uchumi ili dola iweze kuingia kwenye mzunguko na rate iweze kushuka.. But kulingana na hali ya uchumi ya sasa hivi, kupunguza supply ya shillingi maana yake ni kupunguza money supply growth ambayo directly inaenda ku hit ukuuaji wa uchumi kama tulivolalamika mwaka 2017 (utasakia laymen wanasema Magu kabana kumbe ni kwamba ujasi wa fedha haukui kwenye uchumi kama ilivokuwa kipindi cha nyuma)

Kuna issue nyingine kama
- Ukuuaji wa deni la taifa la nje by now ni kama USD 24 billion hivi... hii nayo inachangia pakubwa kuzorota kwa shillingi nazani ntajipanga next time kuelezea kwenye mada yake (mzozo wa madeni unaonukia Tanzania)
- Kuna issue ya nakisi katika account ya biashara .. na moja wapo ya mambo yanayosababisha hata issue pia ya korosho ipo maana imagine kama nchi ilikuwa ina uhakika wa kupata USD zaidi ya million 500 kila mwaka halfu automatikally haipo tena. (Hata hii ni sababu kwanini nimeona kwamba miaka mitatu ijayo dola inaweza kuwa zaidi ya 2500

Kwa hali ilivo hakuna matumaini hii dolla kwamba itakaa ishuke tena. It seems Banki kuu kama wamesalimu amri. Tegemeo lao pekee ni kwamba inflation ipo bellow 4% na hiyo inatokana zaidi na stabilization ya bei ya chakula.

Na tuzidi tu kuomba Mungu inflation inendelee kuwa hapa ilipo.. Ikianza kupanda na huku shilingi inaporomoka nadhani tutatafutana mpaka chini ya uvungu. Hao tunaowaita mabeberu nao nadhani hii point wanaingoja sana ifike. (Wale watu washenzi wewe usione wamekaa kimya)
Umeeleza kweli kabisa japokuwa Kuna sehemu umeziacha, jamaa hakuwa na talent ya uongozi hadi kufikia 2022 hali ya nchi itakuwa mbaya mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndo advantage za kusoma forex.

Kwa waliopata japo training ya wiki moja wamekuelewa to the maximum. Kwa wale wenzangu na mm ambao hatujagusa hiyo training na wala hatukuwahi kusoma mambo ya uchumi watapata tabu san kukuelewa.

Lkn kiukweli ulichoeleza hapo juu tuombe Mungu shilingi ipate nguvu, la sivyo we are finished.
Mkuu sh itapata wapi nguvu?
Production zote zilizokuwa zinaipa sh nguvu jamaa ameziua na anaendelea kuziua.
Huu ni msiba tayari, tuchimbeni kaburi tu no way

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom